Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-03 19:59:47    
Tangazo

cri

Kabla ya kuwasomea barua tulizopokea kutoka kwa wasikilizaji wetu, leo kwanza kabisa kwa furaha kubwa tunapenda kuwaarifu wasikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo wa Klabu ya wasikilizaji wa CRI ya Kemogemba wa huko Tarime Mara Tanzania, na Bw Mutanda Ayub Sharifu wa Bungoma Kenya kupata nafasi ya ushindi maalum kwenye shindano la chemsha Bongo la Mimi na Radio China kimataifa, tunawapongeza sana.

Kwa kuwa mumepata nafasi ya mshindi maalum, kuna mambo mengi ambayo mnatakiwa kuyafanya ili muweze kupata ya kutembelea China. Kwanza ni kuwa mnatakiwa muwe na pasipoti haraka na muweze kufanya utaratibu wa kuomba visa za ruhusa ya kuja kutembelea China, hivyo tunahitaji mtutumie fax ya ukurasa wa pasipoti zenu kwenye jina na namba ya pasipoti ili tuweze kushughulikia mambo yanayohusu safari yenu kuja kutembelea China, namba yetu ya Fax ni 00861068892593.

Wiki iliyopita tulimwandikia barua pepe msikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo wa Tarime kumwarifu jambo hili, lakini mpaka sasa bado hatujapata barua pepe kutoka kwake. Tunawaomba Bw Ngogo na Bw Sharifu mnaposikia taarifa hii tuwasiliane mara moja, na tunaomba mtutumie namba zenu za simu na muwasiliane nasi kwa barua pepe haraka iwezekanavyo, anuani yetu ya barua pepe ni: swlbj@yahoo.com.cn. Tunawaomba wasikilizaji wetu wengine mnaowafahamu Bw Sharifu na Bw Ngogo muwafikishie taarifa hii, taarifa hii ni muhimu sana na ya haraka.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-03