Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-04 18:34:33    
Je, Palestina imekuwa karibu na vita vya wenyewe kwa wenyewe?

cri

Jeshi la Kundi la Fatah na la Kundi la Hamas yamepambana vikali huko Gaza tokea tarehe 1 Oktoba, hivi sasa mapambano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 12 na wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa. Mapambano hayo ni makali zaidi ndani ya Palestina katika miaka 10 iliyopita.

Tarehe mosi Oktoba watu wengi wa kikosi cha usalama cha Palestina wanaolitii Kundi la Fatah walifanya maandamano huko Gaza, wakilaani serikali inayoongozwa na Kundi la Hamas kutotoa mishahara kwa watumishi wa serikali. Kundi la Hamas lilituma askari elfu kadhaa wa jeshi lililoundwa na kundi hilo kuwafukuza waandamanaji, ambapo pande mbili zilipambana na kumwaga damu, na mapambano hayo yalienea kwa haraka kwenye sehemu ya magharibi ya Mto Jordan, Jeshi la serikali ya Hamas na ofisi nyingi ziliteketezwa na wafuasi wa Fatah.

Ili kupunguza hali ya wasiwasi, viongozi wa Kundi la Hamas na Kundi la Fatah tarehe 2 walitoa amri kuwataka askari wa kila upande warudi kwenye kambi zao, lakini mapambano bado yalitokea mara kwa mara, uhusiano mbaya kati ya pande hizo mbili ulipamba moto tarehe 3. Kundi la Al Aqsa lililo chini ya Kundi la Fatah siku hiyo lilitishia kuwa litawashambulia viongozi wa Hamas walioko nchini na ng'ambo, na upande wa Hamas umelilaani kundi hilo kwa kufanya kitendo cha uchokozi na kuzidisha hali ya wasiwasi. Kundi la Hamas hata limelilaani Kundi la Fatah kushirikiana na Israel kwa kuzusha vurugu.

Katika hali hiyo watu wengi wana wasiwasi kuwa mgogoro huo utaisogeza Palestina kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Lakini wachambuzi wanaona kuwa, hali ya Palestina bado inaweza kudhibitiwa, na kuna uwezekano wa aina mbalimbali wa kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe visitokee kwa pande zote.

Kwanza, mgogoro wa hivi sasa ulitokea kati ya majeshi ya makundi hayo mawili, na viongozi wa kisiasa wa Fatah na Hamas wote wanafanya juhudi za kudumisha hali ya utulivu. Waziri mkuu wa serikali ya utawala wa Palestina ambaye pia ni kiongozi wa Kundi la Hamas Ismail Haniyeh tarehe 3 alitoa mwito wa kuyataka makundi hayo mawili yadumishe umoja wa kitaifa na kuacha mgogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kabla ya hapo, Bwana Haniyeh pia alitoa mwito wa kuanzisha tena mazungumzo na Kundi la Fatah kuhusu kuunda baraza la mawaziri. Na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina ambaye pia ni kiongozi wa Kundi la Fatah Bwana Mahmoud Abbas pia ameahidi kuwa hataruhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe vitokee nchini humo.

Aidha sababu ya kimsingi ya mgogoro kati ya Kundi la Hamas na Kundi la Fatah ni migongano ya kisiasa katika pande hizo mbili kuhusu kuitambua Israel na masuala mengine, ambayo siyo migongano ya kitaifa kama ile iliyosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika sehemu nyingine nyingi duniani kwa hivi sasa. Katika utawala wake wa mamlaka ya serikali, Kundi la Hamas liliwekewa vikwazo vya kiuchumi na Israel na nchi za magharibi, ambapo limetambua kuwa linahitaji kushirikiana na Kundi la Fatah na nguvu nyingine za kisiasa, na mapambano ya kijeshi yaliyotokea katika siku hizi pia yameonesha kuwa, pande mbili za Hamas na Fatah zinalingana katika nguvu za kijeshi, kila upande hauwezi kuuangamiza upande mwingine.

Zaidi ya hayo wananchi wa Palestina hawataki kuzushwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Matokeo ya uchunguzi uliofanyika hivi karibuni yameonesha kuwa zaidi ya nusu ya wapalestina wana matumaini kuwa Kundi la Hamas na Kundi la Fatah yataunda serikali ya muungano.

Na juhudi za amani za jumuiya ya kimataifa pia zitazuia kwa kiasi fulani mgogoro ndani ya Palestina usipambe mto. Katika siku hizi Umoja wa Mataifa, Umoja wa nchi za kiarabu, na Marekani zote zinazitaka pande mbili zijizuie. Wachambuzi wanaona kuwa, bado kuna mwanga wa kuondolewa na kukomesha kwa mgogoro ndani ya Palestina.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-04