Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-04 19:59:04    
Mapishi ya doufu yenye ladha ya samaki na pilipili hoho

cri

Mahitaji:

Doufu gramu 600, paja la ash gramu 50, uyoga gramu 50, pilipili hoho gramu 10, vipande vya tangawizi, na vitunguu saumu kila kimoja gramu 5, vipande vya vitunguu maji gramu 15, chumvi gramu 3, M.S.G gramu 2, unga wa pilipili manga gramu 1, mchuzi wa sosi gramu 10, siki gramu 5, sukari gramu 3, kiasi kidogo cha maji ya wanga, mvinyo wa kupikia, ute wa yai.

Njia:

1. kata doufu iwe vipande vipande,mimina maji kwenye sufuria na tia chumvi,tia vipande vya doufu kwenye sufuria, washa moto chemsha maji kwa dakika 2, halafu pakua vipande vya doufu mpaka vipoe. halafu tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya doufu vikaange, halafu vipakue. Weka tundu katika kila vipande vya doufu. Kata paja la ash na uyoga vipande vipande, weka vipande hivyo ndani ya tundu kwenye doufu. Weka vipande vya doufu kwenye sahani, weka sahani hiyo kwenye sufuria yenye maji, chemsha maji, mpaka yachemke kasha pakua.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria tia pilipili hoho na vipande vya tangawizi na vitunguu saumu korogakoroga, halafu mimina maji tia sukari, mchuzi wa sosi, siki, maji ya wanga, korogakoroga, tia vipande vya vitunguu maji, ipakue na mimina kwenye doufu. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-04