Tarehe 4 Oktoba, mkupuo wa kwanza wa wanafunzi waliosoma lugha ya Kichina walihitimu masomo ya Chuo cha Confucius cha Nairobi Kenya. Sherehe ya kuhitimu masomo ilifanyika kwa shangwe. Balozi wa China nchini Kenya Bwana Zhang Ming, Mkuu wa Chuo cha Confucius wa upande wa Kenya Bwana Esac Mbeki na Mkuu wa chuo hicho wa upande wa China Bibi Song Lixian kwa pamoja waliwakabidhi vyeti vya kuhitimu masomo kwa wanafunzi 18, na wanafunzi watano miongoni mwao ambao walipata mafanikio mazuri katika masomo pia walipewa barua ya ajira kutoka kwa kampuni moja ya utalii iliyowekezwa na wafanyabiashara wa China.
Katika miezi 10 iliyopita, Chuo cha Confucius cha Nairobi kikiwa chuo cha kwanza cha Confucius barani Afrika, mbali na kufanikiwa kuhitimisha masomo ya mkupuo wa wanafunzi waliosoma lugha ya kichina, chuo hicho pia kimekuwa kituo mafunzo ya lugha ya Kichina nchini Kenya, ambacho kimekuwa kama daraja la kueneza utamaduni wa taifa la China na kuzidisha urafiki kati ya China na Kenya.
Tokea tarehe 29 Aprili mwaka huu rais Hu Jintao wa China alipokutana na waalimu na wanafunzi wa Chuo cha Confucius cha Nairobi huko Nairobi Kenya, chuo hicho kilijulikana sana nchini China na nchini Kenya. Wakati huo watu waliotazama televisheni walishangazwa na wanafunzi wa chuo hicho ambao waliongea kwa kichina sanifu, hata walikuwa hawawezi kuamini kuwa wakati huo wanafunzi hao walikuwa wamejifunza lugha ya Kichina kwa zaidi ya miezi minne tu.
Mafanikio hayo hakika yalipatikana kutokana na juhudi za waalimu wa Chuo cha Confucius cha Nairobi, ambao walifanya bidii kadiri wawezavyo katika mafunzo yao. Siku moja Mwanafunzi Bi.Hailun alipotoa hotuba katika chuo alitaja njia ya mafunzo ya walimu ya kuwafurahisha. Alisema baada ya kusoma sauti nne za lugha ya Kichina, amejua kutofautisha maneno ya kichina Tang yaani Supu, Tang yaani Sukari, Tang yaani kulala, na Tang yaani ujoto mkali.
Hakika mafanikio waliopata wanafunzi pia yalitokana na bidii zao wenyewe. Katika Chuo cha Confucius, wanafunzi walitumia fursa zote kujifunza Kichina, kila wakikutana wachina huwa wanaongea nao kwa hiari ili kufanya mazoezi ya kuongea kwa Kichina.
Katika darasa la Kichina kuna wanafunzi 25, mmoja kati yao amepata udhamini wa kusoma nchini China, wanafunzi 18 wamepitia mtihani, na wengine 6 walishindwa, Bi. Song Lixian alisema kama kiwango cha wanafunzi hakijafikia kigezo, hawawezi kupata vyeti vya kuhitimu masomo. Alisema hivi sasa wanafunzi wengi wanataka kujifunza lugha ya Kichina, kwa wao waalimu kazi muhimu zaidi ni kutoa mafunzo kwa hatua madhubuti, ili wanafunzi wajifunze vizuri lugha ya Kichina, na wanapaswa kuwajibika.
Katika Chuo cha Confucius cha Nairobi, mafunzo ya lugha ya Kichina yanahusiana zaidi na mafunzo ya utamaduni wa China, hivyo chuo hiki kimekuwa kama kituo kidogo cha utamaduni wa China. Chuo hiki mara kwa mara kiliwapangia wanafunzi kutazama filamu za kichina, kuonja chakula cha kichina, kuandika maandiko ya Kichina, na kuchora michoro ya kichina, hayo yote si kama tu yamewasaidia wanafunzi kujifunza vizuri lugha ya Kichina, bali pia yamewawezesha wanafunzi waelewe vilivyo utamaduni wa China.
Katika Chuo cha Confucius cha Nairobi, wanafunzi walipoulizwa kuwa kwanini wanachagua kujifunza lugha ya Kichina, wengi walijibu, "Napenda utamaduni wa China", "Nataka kuijua zaidi China". Na wanafunzi waliohitimu masomo ya Kichina, wengi wao wanataka kuendelea kusoma lugha ya Kichina ama kupata fursa ya kusoma nchini China, na kuelewa vizuri zaidi utamaduni wa China ili kuhudumia maingiliano na ushirikiano kati ya Kenya na China.
Idhaa ya Kiswahili 2006-10-05
|