Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-06 19:44:00    
China inashirikiana na Afrika badala ya kuitishia

cri

"Watu wa China ni wenzi wa dhati wa watu wa Afrika daima dawamu. China kuendeleza uhusiano na Afrika si kwa ajili ya kutaka maliasili za Afrika kama watu kadhaa wanavyofikiria." Maneno hayo yaliyosemwa waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao wakati alipofanya ziara katika nchi 7 za Afrika yanakubaliwa na nchi za Afrika kwa pamoja.

Huu ni mwaka wa 50 tangu China ianzishe uhusiano wa kibalozi na nchi za Afrika. Katika miaka 50 iliyopita, China ilizisaidia nchi za Afrika kuinua nguvu zao na kujiendeleza kwa kujitegemea, na nchi za Afrika ziliiunga mkono China kwenye masuala mengi muhimu ya kimataifa.

"China siku zote inashikilia kuwapatia ndugu wa Afrika msaada kadri iwezekanavyo bila ya masharti yoyote." Mambo mengi yamethibitisha maneno hayo aliyosema Bw. Wen Jiabao kwenye ufunguzi wa mkutano wa baraza la kwanza la ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika ya Kusini. China imeisaidia Afrika kutekeleza miradi karibu 900 ya maendeleo ya uchumi na jamii; baada ya baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika kuanzishwa miaka 6 iliyopita, China imefuta madeni ya yuan bilioni 10.5 kwa nchi 31 za Afrika; katika miaka mitatu ya karibuni China imetoa mafunzo ya kiufundi kwa elfu 10 wa sekta mbalimbali kutoka nchi za Afrika; na madaktari elfu 16 wa China wamewatibu wagonjwa milioni 240 wa Afrika.

Nchi husaidiana, China haiepuki kusema inaihitaji Afrika. Mwenyekiti Mao Zedong aliwahi kusema, Marafiki wa Afrika waliisaidia China kuingia kwenye Umoja wa Mataifa. Nchi wananchama 53 wa Umoja wa Mataifa ni nchi za Afrika, ambazo zinachukua asilimia 28 ya viti kwenye baraza la Umoja wa Mataifa. Nchi za Afrika ziliiunga mkono China kwenye masuala ya Taiwan na haki za binadamu, na wakati China ilipogombea nafasi ya kuandaa michezo ya Olimpiki na maonesho ya Shanghai.

Bw. Wen Jiabao alipokumbuka ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika aliwambia viongozi wa nchi za Afrika, "Mimi nakuja kuwatembelea jamaa na marafiki zangu." Na viongozi wa nchi za Afrika walisema, "Umerudi nyumbani."

Urafiki kati ya ndugu wa China na Afrika unawatia moyo, na ushirikiano wa kiwenzi wa dhati kati ya China na Afrika ni wa kufurahisha.

  

Thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilikuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 10 kwa mara ya kwanza mwaka 2000, na baadaye thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili iliongezeka haraka, mwaka 2005 thamani hiyo ilifikia dola za kimarekani bilioni 39.8, ambayo ni mara 800 ya thamani ya miaka 50 iliyopita. Ujumla wa thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi za Afrika umefikia dola za kimarekani bilioni 1.18, China imeanzisha makampuni zaidi ya 800 barani Afrika, na China imekuwa mwenzi mkubwa wa tatu wa kibiashara wa Afrika baada ya Marekani na Ufaransa.

Maendeleo ya amani ya China yamewatia moyo watu wa Afrika na kuwapatia maarifa. Watu wengi wa Afrika wametambua thamani maalum ya maarifa ya China. Mwanachuo maarufu wa Nigeria Femi aliandika makala akisema, mageuzi ya kiuchumi nchini China yanafanyika mbele ya macho yetu. Mwujiza huo umeonesha kuwa, nchi moja ambayo inajiamini, kuamua kufanya juhudi na kufikiria mustakabali wake inaweza kupata mafanikio makubwa. Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola alisema, msimamo wa China unaendana na hali halisi na mahitaji ya maendeleo ya Afrika. China inaipatia Afrika msaada, na kuanzisha uhusiano unaolenga kusukuma mbele ushirikiano wa kusaidiana bila masharti yoyote.

China inakaribishwa na nchi za Afrika, lakini inashukiwa na kusudiwa na nchi za magharibi, na maneno mabaya yanasikika mara kwa mara. Nchi hizo zinasema China inanyang'anya nishati ya Afrika, na vitendo hivyo ni ukoloni mpya. Vyombo vya habari vya nchi kadhaa zikiwemo Marekani, Ufaransa na Japan vinasema China inafanya hivyo dhidi ya athari ya Marekani barani Afrika, na kutaka kuikalia na kuizingira Afrika.

Maneno hayo yanayopotosha ukweli wa mambo ni usemi wa "tishio la China" barani Afrika, na yamekwenda kinyume na historia na ukweli wa mambo, na yana makusudi maalum.

Katika sekta ya biashara, hivi karibuni China imeongeza kununua bidhaa kutoka Afrika. Mwaka 2005 thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilikuwa ni dola za kimarekani bilioni 39.8, thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka Afrika ni dola za kimarekani bilioni 21.1, ambayo ni kubwa kuliko thamani ya bidhaa zilizouzwa barani Afrika. China imechukua hatua nyingi ambazo zinasaidia maendeleo ya Afrika. Kwa mfano, kuanzia mwezi Januari mwaka huu, China imefuta ushuru wa bidhaa 190 kutoka nchi 30 zilizo nyuma zaidi kiuchumi za Afrika, baadaye thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi hizo iliongezeka kwa mara moja.

Makampuni ya China yameharakisha hatua za kuwekeza barani Afrika, na yamezipatia nchi za Afrika teknolojia, na kutoa mafunzo kwa wataalamu; bidhaa nzuri zenye bei nafuu za China zimeongeza aina za bidhaa katika masoko ya Afrika na kuinua kiwango cha maisha ya watu wa huko. Kwa mfano, wataalamu wa kilimo wa China walikwenda Mali kushirikiana na watu wa huko kupanda mboga, wakazi wa huko hawana haja ya kununua mboga kutoka nchi za nje, na bei ya mboga ilipungua kwa nusu.

China ni nchi kubwa inayoendelea, Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea. Uchumi wa China na Afrika unasaidiana, na unaweza kupata maendeleo makubwa. Ushirikiano wa dhati kati ya China na Afrika hauzuiliwi na umbali mkubwa uliopo kati ya sehemu hizo na nguvu nyingine. Hali ya urafiki, wenye usawa na kunufaishana kati ya China na Afrika itaendelea kusonga mbele.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-06