Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-06 20:22:22    
NATO yakabiliwa na changamoto kubwa baada ya kukabidhiwa jukumu kamili la kulinda amani nchini Afghanistan

cri

Tarehe 5 Oktoba NATO ilikabidhiwa na jeshi la Marekani jukumu la kulinda amani katika sehemu ya Mashariki ya Afghanistan, hatua ambayo inamaanisha kuwa sasa NATO itawajibika kulinda usalama kote nchini Afghanistan. Msemaji wa NATO siku hiyo alisema ingawa hakuna upinzani mkali wa wanajeshi wa Taliban katika sehemu ya mashariki ya Afghanistan kama ilivyo katika sehemu ya kusini ya nchi hiyo, lakini kikosi cha NATO kitaendelea kujizatiti na kuwa tayari kupambana wakati wowote. Wachambuzi wanaona kuwa baada ya kulipuka kwa vita vya Afghanistan miaka mitano iliyopita, kikosi cha NATO bado kinapaswa "kuwa tayari kupambana wakati wowote", hii inaonesha hali mbaya ya usalama nchini Afghanistan na changamoto kali itakayoikabili NATO katika siku zijazo.

Mwanzoni Marekani ilipoanzisha vita vya Afghanistan, ilikuwa na imani ya kuupindua utawala wa Taliban, kuangamiza kundi la kigaidi na kupata ushindi wa vita hivyo kwa kutegemea mashambulizi makubwa ya ndege, askari wachache wa kikosi maalumu na wapelelezi wachache. Lakini muda si mrefu baada ya kulipuka kwa vita, Marekani na nchi washirika zililazimika kuongeza kutuma wanajeshi wengi zaidi nchini Afghanistan. Wakati huo huo Marekani ilianzisha vita vingine nchini Iraq, kwa hiyo ikashindwa kufuatiliwa ukarabati wa Afghanistan. Hadi kufikia mwaka 2004 jumuiya ya NATO ilipokubali kuchukua jukumu la jeshi la Marekani, hali ya usalama nchini Afghanistan ilikuwa mbaya sana.

Jukumu la kikosi cha NATO nchini Afghanistan ni kulinda amani na kuisaidia serikali ya Afghanistan kutekeleza ukarabati wa nchi hiyo, na kuwaangamiza wanamgambo waliobaki wanaotishia usalama wa Afghanistan. Lakini kama ofisa wa NATO alivyokiri, ni kuwa vitendo vya kijeshi nchini Afghanistan ni changamoto kali zaidi kuliko nyingi inayoikabili NATO, hususan jeshi la Uingereza lilipokabidhiwa udhibiti wa sehemu ya Kusini ya Afghanistan lilikumbwa na upinzani mkubwa kupita kiasi. Mkuu wa jeshi la Uingereza alisema wanajeshi wake walikuwa wanashambuliwa na wanamgambo wa Taliban na makundi mengine kila siku, ambapo katika muda usiozidi wiki moja, wanajeshi 23 wa NATO waliuawa na wengine 80 kujeruhiwa, idadi ambayo iliweka rekodi katika historia ya NATO. Hali mbaya ya usalama hata ilimbidi kamanda wa majeshi ya nchi washiriki za Ulaya ya NATO Bw. James Jones atake kuongeza nguvu ya mashambulizi ya ndege. Vyombo vya habari vya Uingereza vilisema jukumu la NATO nchini Afghanistan limebadilika kwa kufanya mapambano badala ya kusaidia ukarabati.

Mbali na ukali wa mapigano, ukarabati wa Afghanistan pia ulikumbwa na tatizo jipya kwamba, ili kujipatia lishe wakulima wa nchi hiyo walipanda kiasi kikubwa cha mipopi, na licha ya mji mkuu Kabul, sehemu kubwa za nchi hiyo inadhibitiwa na wababe wa kivita na magendo wa dawa za kulevya. Kutokana na hali hii, kikosi cha kulinda amani nchini Afghanistan kilitoa maombi mara kadhaa ya kuongeza kutuma wanajeshi nchini Afghanistan, lakini nchi nyingi hazikufurahia kuitikia maombi hayo zikihofia kushambuliwa na magaidi. Mwezi Septemba mwaka huu Jumuiya ya NATO ilifanya mkutano wa kujadili suala la kuongeza wanajeshi nchini Afghanistan, lakini mkutano huo ulimalizika bila maendeleo yoyote. Hivi sasa NATO ina wanajeshi elfu 32 nchini Afghanistan, ambao nusu yao ni wa Marekani, na wengine wanatoka Uingereza, Canada na Denmark, ambapo wanajeshi wa nchi nyingine ni wachache sana ambao wanakaa katika sehemu ya kaskazini ya Afghanistan yenye hali yenye utulivu zaidi.

Hivi sasa NATO imekabidhiwa udhibiti wa hali ya usalama kote nchini Afghanistan, lakini imeshindwa kuonesha imani kubwa kama hapo awali ilipokabidhiwa jukumu la kusaidia ukarabati wa Afghanistan. Makala ya gazeti la Uingereza "The Spectator" inasema, kama NATO inataka kuiokoa Afghanistan kwa moyo wa dhati, inapaswa kufanya bidii kwa miongo kadhaa, ambapo inapaswa kutumia fedha nyingi zaidi na kutuma wanajeshi wengi zaidi, lakini hata kama itafanya hivyo si lazima kuwa itapata mafanikio.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-06