Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-09 17:43:52    
Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu

cri

Tukifunga safari kutoka Changchun, mji mkuu wa mkoa wa Jilin, baada ya muda wa saa moja na nusu tu, tutafika kwenye bustani ya misitu ya taifa ya Diaoshuihu ya Changchun. Katika bustani hiyo kuna mapango ya mawe ya chokaa, ambapo milima, mto, misitu, pango na mawe vinapatana na kuonesha mandhari nzuri ya ajabu inayowavutia watalii kwenda huko kufanya udadisi juu ya mapango ya chokaa lenye miujiza.

Wakiingia kutoka mlango wa bustani, watalii wanaweza kuona mbele ni mlima mrefu zaidi wa sehemu ya Changchun wenye mwinuko wa mita 711 kutoka usawa wa bahari. Ndani ya bustani, njia ya mlimani ni yenye vipengele vingi, kando moja ya njia ni miamba mirefu, na kando nyingine ni miti mingi mirefu iliyokua tangu zamani sana. Mwongozaji wa watalii Bi.Wang Li alituambia kuwa, njia hiyo iitwayo "Buyunya" ni njia ya lazima ya kuelekea kwenye Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu. Alisema:

Njia hiyo Buyunya, maana yake ya kichina ni kwamba, kutembea katikati ya mawingu na ukungu, kwani kila asubuhi saa 9 na saa 10 hivi, ukungu mwingi hutanda kwenye sehemu hiyo, hivyo watu wakitembea kwenye njia ya kuelekea kwenye mapango ya mawe ya chokaa, ni kama wanapitapita kwenye mwanya wa mawe mithili ya kutembea peponi.

Watalii wakipanda ngazi ya njia ya mlimani, watafika kwenye mlango wa Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu. Maana ya Diaoshuihu ya kichina ni kwamba umbo la mapango hayo ni kama birika moja linaloning'inia juu chini. Wakiingia kwenye mapango hayo, mara wanaweza kusikia baridi kali, inasemekana kuwa joto ndani ya mapango ni nyuzi kati ya sentigredi 6 na 7 katika majira manne ya mwaka, na wakati wa siku za baridi, ndani ya mapango hali ni kama siku za mchipuko nje.

Njia nyembamba ndani ya mapango inaweza kuwawezesha watu wawili kutembea bega kwa bega, kando mbili za njia hiyo kuna sanamu 500 za buddha zenye kimo sawasawa na binadamu, sanamu hizo zina sura mbalimbali tofauti. Mwongozaji wa watalii Bi. Wang Li alisimulia hekaya kuhusu Mapango ya chokaa ya Diaoshuihu. Alisema:

Inasemekana kuwa, wakati wa zama za kale katika nchi isiyo na matata kulikuwa na watawa elfu moja, ambapo mtawa mmoja alitaka kuzusha vurugu kwa fikra ya dini ya kibuddha, mfalme wa nchi hiyo aliamua kuwaua watawa hao 1000, wakati huo watawa 500 miongoni mwao wenye uwezo wa ajabu waliondoka na kuelekea kwenye mlima Dalazishan wenye mandhari nzuri na kukaa ndani ya Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu.

Watalii wakipita kwenye sanamu za buddha na njia yenye urefu wa mita 158, ambapo wanaweza kuona pia mawe ya chokaa yenye sura mbalimbali tofauti, nguzo za mawe na mianzi ya mawe, watajihisi kama wapo katika mandhari iliyosimuliwa kwenye hekaya. Bi. Wang Li alisema:

Bustani nzima inaitwa bustani ya mawe, ambapo mawe ya chokaa yenye sura mbalimbali tofauti yanadondosha matone ya maji, na kila baada ya miaka elfu moja, mawe hayo yanaweza kukua na kuongezeka kwa urefu wa sentimita moja. Hivyo mapango hayo ya mawe ya chokaa yaliundwa baada ya miaka milioni 200, hivyo kila jiwe la chokaa lina thamani kubwa.

Baada ya kupita kwenye njia yenye urefu wa mita 158, watalii watafika kwenye pango kubwa zaidi la mawe ya chokaa ndani ya Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu. Ndani ya pango hilo, kwa upande mmoja, sanamu ya Buddha Mile Laughing Buddha, yaani Buddha anayecheka yenye urefu wa mita 18, na mwilini mwa sanamu hiyo kuna sanamu za watoto 100 wanaochezacheza kwa furaha. Na mwanga unamulika moja kwa moja kutoka kwenye tundu la mraba kwenye dari la pango hilo hadi utosi wa kichwa cha sanamu Mile Laughing Buddha, zamani mkazi wa kijiji kilichoko karibu na pango hilo Bwana Mao Ren alipogundua tundu hilo la mraba ndipo mapango ya mawe ya chokaa yalipogunduliwa kutokana na hayo. Bwana Mao alisema:

Mwaka 1983 mimi na wenzangu kadhaa tuligundua tundu la mraba kwenye mlima huu, tuliona ndani kama kuna kisima, tulikuwa na hamu ya kuingia kwenye kisima hicho kutazama hali halisi, tukafungwa na kamba tunaingia ndani.

Kamba yenye urefu gani?

Mita 120.

Ndani kuna mwangaza au ni giza?

Giza sana, tulichukua tochi lakini hatukuweza kuona mbali, ambapo tuliona mawe ya chokaa yenye sura mbalimbali na rangi tofauti ambayo yalituvutia sana.

Inasemekana kuwa, Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu ni mapango yaliyoko kwenye mwinuko mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari, maporomoko ya maji ndani ya mapango hayo ni marefu zaidi, na eneo la mapango hayo ni kubwa zaidi.

Baada ya kutembelea kwenye mapango hayo ya mawe ya chokaa, watalii wakisimama kwenye Kilele cha mlima, wanaweza kuona milima mingi inayoegemeana inaonekana kama imesisima kwenye ngazi mbalimbali. Na kwenye bonde la mlima, nyumba moja moja zilizojengwa kwa matofali mekundu zimetapakaa kwenye sehemu hiyo iliyofunikwa na miti na majani, ambapo mabwawa mawili madogo yanaonekana kama nyota zinazomeremeta. Mtalii kutoka Changchun Bwana Li Zhiqiang alisema:

Sikufikiri kama mapango makubwa ya mawe ya chokaa yako katika sehemu ya kaskazini mashariki y4a China, mandhari ya maumbile ndani ya mapango hayo ni nadra kupatikana duniani. Hasa sehemu ya kaskazini ya China ina uhaba wa maji, hivyo si rahisi kuundwa kimaumbile kwa mapango hayo ya mawe ya chokaa. Sehemu hiyo kweli ina mandhari nzuri ya kupendeza.

Idhaa ya kiswahili 2006-10-09