Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-11 18:08:28    
Wanasayansi wa Afrika ya kusini wafichua siri ya kuchoka

cri

Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Afrika ya kusini unabainisha kuwa kuhisi uchovu kwa binadamu ni kutokana na kichochezi cha kitu cha kikemikali cha ute (IL-6) wa chembe nyeupe za damu(white blood cell) kwa ubongo wa binadamu. Ugunguzi huo unatarajiwa kusaidia kupata njia ya kutibu baadhi ya ugonjwa ukiwemo ugonjwa wa muda mrefu wa hali mbalimbali za tatizo la kusikia uchovu mwilini.

Jarida jipya la Uingereza lijulikanalo "Wanasayansi Wapya" linasema kuwa kwa kawaida, watu wanaona kuwa kusikia uchovu ni misuli ya mwili wa binadamu kutoweza kufanya kazi katika hali ya kawaida kutokana na misuli kuchoka kupita kiasi. Lakini, mashahidi mengi yameonesha kuwa hata kabla ya misuli kuchoka kupita kiasi, ubongo wa binadamu umeashiria mtu kusikia uchovu ili kuzuia misuli kuathirika kutokana na kufanya kazi kupita kiasi.

Wanasayansi wa chuo kikuu cha Captown, Afrika ya kusini wamegundua kuwa ute (IL-6) ni gene za chembe za mwili (cell) zenye uwezo wa kazi nyingi, ambao unafanya kazi muhimu sana za kukinga virusi vya maradhi. Baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, ute huo utaweza kuongezeka kwa mara 60 hadi 100 kuliko hali ya kawaida. Kupiga sindano za ute huo mwilini mwa mtu mwenye afya nzuri, mtu huyo atasikia uchovu.

Wanasayansi walifanya majaribio kwa wachezaji 7. Kabla yao kukimbia kwa mita elfu 10, walipiga sindano za ute-6 kwa wachezaji wa kikundi kimoja, wakati wachezaji wa kikundi kingine walipigwa sindano za dawa ya kufariji tu, kisha wanarekodi matokeo yake. Baada ya wiki moja, vikundi hivyo viwili vikabadilishana, na kufanya majaribio hayo tena. Matokeo yalidhihirisha kuwa wachezaji waliopigwa sindano za ute-6, walitumia kiasi cha dakika moja zaidi kuliko wale waliopigwa sindano za dawa ya kufariji. Katika mbio za mita elfu 10, tofauti ya dakika moja ni tofauti kubwa sana.

Watafiti wamesema kuwa baadhi ya wachezaji huwa wanasikia uchovu katika baadhi ya nyakati, na kushindwa kuonesha vilivyo uhodari wao, hali hiyo huenda inahusika na kuwa na ute-6 mwingi mwilini. Kutumia dawa ya kuzuia ute usifanye kazi, mtu atasikia kupungua kwa uchovu mwilini, na kupunguza hali ya ugonjwa unaohusika.

Hata hivyo, wataalamu wamesema kuwa kutokana na kazi nyingine unazofanya ute wa aina hiyo mwilini mwa binadamu, njia hiyo huenda italeta athari nyingine mbaya, hivyo wanasayansi wanapaswa kufanya majaribio kwa uangalifu na makini kabla dawa ya kuzuia ute wa aina hiyo kutumika rasmi.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-11