Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-11 20:48:24    
Mapishi ya brokoli na korosho

cri

Mahitaji

Brokoli gramu 250, korosho gramu 150, karoti gramu 100, chumvi kijiko kimoja, M.S.G kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, kiasi kidogo cha maji ya wanga.

Njia

1. kata brokoli iwe vipande vipande, kata karoti iwe slesi.

2. chemsha maji, tia vipande vya brokoli na slesi za karoti, baada ya kuchemka, vipakue.

3. Washa moto tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi ya 30, tia korosho kaanga, mpaka ziwe na rangi ya hudhurungi, kisha pakua.

4. Washa moto tena tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya brokoli na karoti, korogakoroga, tia chumvi, M.S.G, sukari, korogakoroga, mimina maji kidogo, baada ya kuchemsha, mimina maji ya wanga, korogakoroga, tia korosho korogakoroga, halafu pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.