Rais Jacques Chirac wa Ufaransa na Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel tarehe 12 mwezi huu walisimamia kwa pamoja mkutano wa 7 wa pamoja wa mabaraza ya serikali za Ufaransa na Ujerumani huko Paris. Mkutano huo ulijadili masuala ya ushirikiano na usawazishaji wa sera wa pande mbili kwenye maeneo ya safari za ndege na za vyombo vya anga ya juu, nishati, ujenzi wa Ulaya na masuala yanayofuatiliwa zaidi duniani. Matokeo ya mkutano huo yanaonesha kuwa mashauriano na ushirikiano ni kitu muhimu zaidi katika uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa.
Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo wa pamoja, nchi mbili zote zilikabiliwa na suala ambalo kampuni ya Airbus itaingia hasara ya Euro bilioni 4.8 kutokana na kuahirishwa mara tatu kutoa ndege za Airbus A380. Kampuni hiyo inapaswa kupunguza wafanyakazi wake ili kupunguza hasara. Kwa kufuata mpango uliotolewa na mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni ya Airbus, kituo cha uzalishaji wa mabodi ya ndege ya Airbus A380 kitahamishwa mjini Toulouse, Ufaransa kutoka Hamburg nchini Ujerumani. Kufanya hivyo si kama tu upande wa Ujerumani utapoteza nafasi nyingi za ajira, bali pia faida ya viwanda vinavyozalisha vipuri kwa ajili ya Airbus itakabiliwa na tishio kubwa. Aidha kiwango cha utafiti wa teknolojia ya ndege ya Ujerumani pia kitaathiriwa. Baada ya mvutano, mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni ya Airbus aliondoka madarakani, na wadhifa huo ukachukuliwa na Karos, mwenyekiti wa pande wa Ufaransa wa usalama wa safari za ndege na kampuni ya safari za anga ya juu wa Umoja wa Ulaya. Baada ya kukabidhiwa wadhifa huo, Bw. Karos alibadilisha sera za zamani, akaunganisha viwanda vya kampuni hiyo na kupunguza wafanyakazi elfu 10 wa idara za uendeshaji shughuli za ofisini na utawala. Hivi sasa kampuni ya Airbus ina wafanyakazi elfu 55 kwenye sehemu nyingi duniani wakiwemo elfu 22 nchini Ufaransa na elfu 20 nchini Ujerumani.
Mchambuzi alisema katika hali ya namna hiyo, msimamo wa serikali ya Ufaransa na serikali ya Ujerumani kuhusu mpango wa upunguzaji wafanyakazi ni muhimu zaidi, ambapo uhusiano kati ya Ufaransa na Ujerumani unakabiliwa na changamoto kubwa. Baada ya kushauriana kwa asubuhi nzima, wakuu wa Ufaransa na Ujerumani Kwenye mkutano na waandishi wa habari walieleza uungaji mkono kuhusu mpango huo mpya wa Bw. Karos. Rais Chirac wa Ufaransa alisema mpango wa ustawishaji unatakiwa kutekelezwa kwa uwiano na viwanda viwili vilivyoko kwenye miji ya Hamburg na Toulouse, na kuzingatia ipasavyo maslahi ya viwanda vinavyozalisha vipuri vya ndege. Chansela wa Ujerumani Bw. Merkel alisema, mpango huo unatakiwa kutekelezwa kwenye msingi wa usawa, na kuhakikisha kadiri iwezavyo maslahi ya wafanyakazi wa pande mbalimbali. Kauli za pande mbili zimeweka msingi kwa utatuzi wa mgogoro wa hivi sasa wa kampuni ya Airbus na kuepusha athari kwa uhusiano wa nchi mbili.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, rais Chirac alisema baada ya siku chache, Ujerumani itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, Ufaransa itajitahidi kuisaidia Ujerumani kuhimiza ujenzi wa Ulaya katika kipindi chake. Bibi Merkel pia alisisitiza kuwa, mkutano huo umeweka msingi wa ushirikiano wao katika siku za baadaye, pia alitoa wito wa kutaka kuanzisha uhusiano wa utulivu na ushirikiano kati ya Ulaya na Russia kwenye eneo la nishati. Mapatano hayo kwenye msimamo na sera yanaonesha pia kukomaa kwa utaratibu wa mashauriano na ushirikiano kati ya Ufaransa na Ujerumani.
Utaratibu wa mkutano wa mabaraza ya serikali unaofanyika kila baada ya muda maalumu kati ya Ufaransa na Ujerumani ulianzishwa kutokana na pendekezo la pamoja la chansela wa zamani wa Ujerumani Bw. Gerhard Schroeder na rais Chirac wa Ufaransa.
|