Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-16 19:00:52    
"Wimbi la China" laikumba Misri

cri

Tangu waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao afanye ziara nchini Misri mwezi Juni mwaka huu, hususan katika siku ambapo mkutano wa viongozi wa nchi wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika unakaribia kufanyika, mwandishi wetu wa habari licha ya kuhisi hali ya hewa ya joto, pia anahisi hali ya shamrashamra kuhusu China.

Toka maofisa wengi wa ngazi ya juu kufanya ziara nchini China, watu kuwa na shauku kubwa ya kununua bidhaa za China hadi wamisri wengi kujifunza lugha ya Kichina, "Wimbi la China" limeikumba nchi nzima ya Misri.

Ofisa wa ngazi ya juu aliyekuwa wa kwanza kuitembelea China kati ya maofisa wengi wa Misri kuitembelea China hivi karibuni ni Bw. Mohammad Rasheed, waziri wa biashara na viwanda wa Misri, aliyefanya ziara nchini China mwanzoni mwa mwezi Septemba. Bw. Rasheed mwenye umri wa miaka 51 mwaka huu, ni mmoja kati ya viongozi muhimu waliobuni sera za mageuzi ya kiuchumi katika miaka ya karibuni nchini Misri. Kabla ya yeye kufanya ziara ya kuitembelea China kwa wiki moja kuanzia tarehe 4 Septemba, alisema Misri inatarajia kuanzisha uhusiano maalumu wa kiuchumi na kibiashara na Misri. Baada ya kurejea nchini alipohojiwa na mwandishi wa shirika la habari la Xinhua alisema, uchumi wa China ulipata maendeleo ya kasi katika miaka zaidi ya 20 iliyopita, China imekuwa mfano wa kuigwa kwa kuvumbua njia ya kujiendeleza. Misri inataka kujifunza uzoefu wa maendeleo wa China.

Kisha Bw. Abdul Rauf Lid, mwenyekiti wa baraza la mambo ya kidiplomasia la Misri aliongoza ujumbe kuitembelea China mwezi Septemba mwaka huu, na alipongeza sana maendeleo iliyoyapata China. Tarehe 9 mwezi Oktoba waziri wa uchukuzi wa Misri Bw. Mansoor alifanya ziara ya siku 4 nchini China, ambapo alikuwa na majadiliano na upande wa China kuhusu kuimarisha ushirikiano katika usafiri wa reli. Mbali na hayo, mawaziri watatu wa uwekezaji, mafuta na teknolojia ya mawasiliano ya habari wa Misri pia wataitembelea China katika siku chache zijazo.

Maofisa wengi wa ngazi ya juu kuitembelea China itatokea mwanzoni mwa mwezi Novemba, ambapo rais Hosni Mubarak wa Misri atashiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika hapa Beijing, na atafanya ziara rasmi ya kuitembelea China. Msaidizi wa waziri anayeshughulikia mambo ya Asia wa wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw. Hifune alisema, hii ni ziara ya 9 ya rais Mubarak nchini China, alisema huu ni wa mwaka wa 50 tangu Misri na China zianzishe uhusiano wa kibalozi, watu wote wa Misri wanazingatia sana kuendeleza uhusiano kati ya Misri na China.

Jambo la pili la "Wimbi la China" ni bidhaa ndogo ndogo zinazotoka China. Watu wa Misri wanapenda sana bidhaa nzuri za bei nafuu zinazozalishwa na China. Tofauti na hali ya miaka michache iliyopita ni kuwa hivi sasa magari ya China yakiwemo Chery na Geely, yanapendwa na watu wengi wa Misri.

Pamoja na "Wimbi la China" kupamba moto, hivi sasa watu wengi wa Misri wanaanza kujifunza lugha ya Kichina, hususan kufunguliwa madarasa ya lugha ya Kichina kwenye kituo cha utamaduni mjini Cairo, ambacho ni kituo cha kwanza kilichoanzishwa na China katika mashariki ya kati.

Hivi sasa watu wa Misri wanapoona watalii waliotoka China, wanapenda kuwasalimia kwa lugha ya Kichina, "Ni hao" au "Ni men hao".