Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-18 19:13:04    
Mapishi ya ngisi na pilipili hoho

cri

Mahitaji

Ngisi gramu 200, pilipili hoho gramu 50, tangawizi gramu 5, figili gramu 10, vitunguu maji gramu 5, vitunguu saumu gramu 5, mafuta ya pilipili hoho kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili

Njia

1. kata tangawizi, figili, vitunguu maji na vitunguu saumu viwe vipande.

2. chemsha maji, mimina mvinyo wa kupikia na vipande vya vitunguu maji na tangawizi baada ya kuchemka tia ngisi, korogakoroga kwa haraka kisha ipakue.

3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria tia pilipili hoho, vipande vya tangawizi, vitunguu maji, vitunguu saumu, figili, korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, tia chumvi na M.S.G, mimina maji kidogo korogakoroga, tia ngisi korogakoroga mimina maji ya wanga, korogakoroga, mwisho mimina mafuta ya pilipili hoho. Kisha ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.