Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-19 14:58:58    
Mwimbaji wa kabila la Wauzbek anayejikita kwenye shughuli za ufadhili

cri

Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur upo sehemu ya kaskazini magharibi mwa China, ni mkoa wanakoishi watu wa makabila mbalimbali wakiwemo Wauzbek wanaojulikana kwa uhodari wa kuimba na kucheza ngoma. Bw. Xiamili Xiakeer ni mwimbaji maarufu atokaye kabila la Wauzbek, mbali na kuwa mwanamuziki pia anajihusisha na shughuli za utoaji misaada.

Xiamili alizaliwa mwaka 1958 katika familia moja iliyojulikana kwa kuimba na kucheza ngoma huko wilaya ya Qitai, mkoani Xinjiang. Baba yake mzazi ni m-uzbek na mamae mzazi ni wa m-uygur. Xiamili ni mtoto wa nne kati ya watoto 6 wa familia hiyo, alikuwa anapenda kuimba na kucheza ngoma tangu alipokuwa mtoto. Alipokuwa na umri wa miaka mitano, alishiriki kwenye sherehe ya kuimba na kucheza iliyoandaliwa wilayani Qitai. Baba yake alimweka jukwaani, ambapo muziki ikisikika mtoto huyo alikuwa akicheza ngoma tatu kwa mfululizo.

Xiamili alijiunga na jeshi alipokuwa kijana. Tabia yake ya kupenda kuimba ilimfanya awafundishe askari wenzake namna ya kuimba wakati wa mapumziko. Mbali na hayo alianza kutunga nyimbo zinazohusu maisha ya jeshini.

Mpaka hivi sasa Xiamili ametunga nyimbo mbalimbali 200 hivi, na albamu zake za nyimbo alizoimba si kama tu zinajulikana nchini China, bali pia zinauzwa vizuri katika nchi za kigeni zikiwemo Japan na Singapore.

Hivi sasa Bw. Xiamili anaendelea kulitumikia jeshi na kupewa sifa ya mchezaji wa ngazi ya kwanza ya taifa. Mara kadhaa anatembelea vikosi vinavyolinda sehemu za mpakani kuwaburudisha wanajeshi wenzake kwa nyimbo. Alisema "Miongoni mwa wasanii wenye sifa ya wachezaji wa ngazi ya kwanza ya taifa, mimi ni wa kwanza kutembelea peke yangu vituo mbalimbali vya mpakani. Kila mwaka katika siku za mapumziko ya siku ya mwaka mpya ya Kichina, nakwenda vituo vya mpakani kuimba nyimbo kwa wanajeshi wa huko. Mwaka huu ulikuwa ni mwaka wa 7 tangu nianze kufanya hivyo. Mpaka sasa nimeshawaburudisha kwa nyimbo askari wenzangu kwa mara zaidi ya 100."

Siku nyingine wakati wa mapumziko ya siku ya mwaka mpya wa Kichina, Bw. Xiamili alipokuwa njiani kwenda kituo cha mpakani kilichopo mlimani gari lililombeba lilishindwa kupanda mlima kutokana na barafu kuganda barabarani. Mwimbaji huyo aliamua kupanda mlima akiwa na ala ya muziki aina ya kodiani bila kujali theluji na barafu. Alipofika kwenye kituo, viatu vyake vilikuwa vimelewa majimaji, mwenyewe akatetemeka kutokana na baridi kali. Askari mmoja aliposhuhudia alikuwa akitumia nguo yake nzito akazungusha miguu ya Xiamili na kuikumbatia ili kuipa ujoto. Kitendo hicho cha askari kilimtia moyo sana Xiamili kiasi ambacho hata akatokwa na machozi. Siku hiyo akisimama chini ya mwangaza wa mwezi, alikuwa anawaburudisha askari hao kwa zaidi ya saa moja.

Mbali na kuimba, Bw. Xiamili pia anajishughulisha na kutoa msaada kwa wengine, yeye anasaidia familia zenye shida za kiuchumi mara kwa mara. Mwaka 2002 alichaguliwa kuwa balozi wa utoaji msaada wa kwanza wa mkoa wa Xinjiang.

Dada Namanguli wa kabila la Wauygur aligunduliwa kuugua saratani ya damu mwaka 2003 alipokuwa na umri wa miaka 18, ambapo familia yake ilikuwa haina uwezo wa kumtibu. Bw. Xiamili akifahamishwa tukio hilo, alitanguliwa kutoa mchango wa Yuan elfu 3, baadaye alimtembelea msichana huyo na kumletea mchango mwingine wa Yuan elfu 10, fedha alizopata kutokana na kushiriki kwenye maonesho ya sanaa. Katika misaada ya Bw. Xiamili na wahisani wengine, dada Namanguli sasa amepata nafuu.

Kutokana na kutumia fedha zilizotolewa na mwimbaji huyo dada mwingine Rexidan Younusi alifanyiwa upasuaji wa kubadilishwa figo, upasuaji huo ulipata mafanikio. Msichana huyo alisema "Tunatumai kuwa wangejitokeza watu wengine wengi mfano wa Bw. Xiamili, tutafurahi sana. Hata katika siku za mapumziko, yeye alikuja kunitembelea, hatua hiyo ilinitia moyo sana. Namshukuru sana."

Kijana Rijipu Reheman ni mwanafuzni wa chuo kikuu cha Hetian cha Xinjiang. Kutokana na umaskini, alishindwa kulipa ada za masomo. Xiamili akisoma maelezo kuhusu kijana huyo kwenye magazeti, aliamua kumsaidia Yuan elfu 4 na mia 9 kutoka kwa akiba yake.

Alipozungumzia tukio hilo, Bw. Xiamili alisema "Nilimpa msaada kijana huyo, alitiwa moyo sana, akaniandikia barua, na babae akiwa na machozi aliniambia kuwa, mimi ni kama baba wa kijana huyo. Baada ya kuhitimu kwenye chuo kikuu, kijana huyo aliamua kurudi kwenye kijiji na kuwatumikia wanakijiji wenzake."

Nyumbani kwa Bw. Xiamili kuna kabati moja iliyojaa vitabu mbalimbali vinavyohusu muziki, historia, mashairi na fasihi. Mwimbaji huyo alieleza kuwa anapenda kufanya mambo mawili tu baada ya kazi, moja ni kusoma na lingine ni kuwasaidia watu wenye shida. Alisema anaona kusoma ni muhimu sana ili kwenda sambamba na wakati. Na kwa jambo lingine anaona ni afadhali awe mtu anayetumikia jamii.

Idhaa ya kiswahili 2006-10-19