Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-23 20:48:11    
Sababu ya kudumisha ongezeko la uchumi kwa miaka mfululizo barani Afrika

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, hali nzuri ya ongezeko la hatua madhubuti imeonekana katika uchumi wa Afrika. Wachambuzi wanaona kuwa, hali hii inatokana na mazingira ya uchumi wa dunia nzima yanayoendelea vizuri, amani na hali ya mambo ya kanda ya Afrika inayotulia, bei za nishati na bidhaa zilizotengenezwa kwa hatua ya mwanzo zinazopanda juu kwenye soko la kimataifa na marekebisho mwafaka wa sera ya uchumi wa nchi za Afrika.

Takwimu zilitolewa na Shirika la fedha la kimataifa IMF zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 1995 hadi 2003, uchumi wa Afrika unadumisha kimsingi ongezeko la kufufua uchumi la mwendo wa kati na chini, na wastani wa ongezeko la mwaka ni asilimia 3.5. Ongezeko la uchumi wa Afrika lilipanda na kuwa asilimia 5.3 mwaka 2004, na mwaka 2005 lilifikia asilimia 5.4, na shirika hilo limekadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa Afrika litalingana na lile la mwaka jana, na mwaka kesho linatazamiwa kufikia asilimia 5.9.

Ufufuzi wa hatua ya madhubuti wa uchumi wa dunia nzima umejenga mazingira mazuri kwa ajili ya kuongezeka kwa uchumi wa nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, mahitaji ya bidhaa za Afrika zilizotengenezwa kwa hatua ya mwanzo yameongezeka kwenye soko la kimataifa, ambapo bei za bidhaa hizo inapanda, hali hii imehimiza ongezeko la uchumi wa Afrika. Hivi sasa utoaji wa mafuta ghafi barani Afrika unachukua zaidi ya asilimia 10 ya ule wa jumla wa dunia nzima. Wakati huo huo mapato ya uuzaji wa madini yasiyo za chuma, kahawa na chai wa nchi za Afrika yameongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa nchi ambazo uuzaji bidhaa unapungua katika miaka ya hivi karibuni, misaada kutoka nje inayoongezeka siku hadi siku pia imepunguza athari mbaya kutokana na kupungua kwa mapato yao ya uuzaji bidhaa nje. Mwezi Septemba mwaka huu Benki ya Dunia ilitoa taarifa ya utafiti ikidhihirisha kuwa, China na India zimeongeza biashara na uwekezaji na nchi za Afrika, hali hii imeleta fursa mpya na nguvu kubwa kwa ongezeko la uchumi wa Afrika na kuongeza nafasi za ajira katika nchi za Afrika.

Mwelekeo wa amani na utulivu barani Afrika pia umetoa uhakikisho mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. Mwanzoni mwa karne iliyopita, Bara la Afrika lilikumbwa na vita na migogoro zaidi ya mara 30, ambayo ilisababisha hasara za dola za kimarekani zaidi ya bilioni 250. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uhimizaji wa jumuiya ya kimataifa, nchi za Sudan na Liberia zilizokumbwa kwa muda mrefu vurugu za vita zinaelekea kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe, na mwelekeo mzuri wa kuacha migogoro ya kimabavu na kutafuta amani umetokea barani Afrika.

Bei ya juu ya mafuta ghafi kwenye soko la kimataifa vilevile ni nguvu kuu ya kuleta ongezeko la haraka la uchumi wa nchi za Afrika zinazozalisha mafuta. Mwaka jana wastani wa ongezeko la uchumi wa nchi hizo ulifikia asilimia 8.

Kupanda kwa bei za bidhaa zisizo za nishati zilizotengenezwa kwa hatua ya mwanzo kumepunguza athari mbaya kwa kiasi fulani iliyotokana na bei kubwa za mafuta kwa nchi za Afrika zinazoagiza mafuta kutoka nje. Na kupanda kwa bei za madini kwenye soko la kimataifa kumeleta faida kwa nchi zinazozalisha bidhaa za madini kama vile Msumbiji, Zambia na Afrika ya kusini, na nchi nyingine kama vile Ethiopia, Sierra Leone, Rwanda na Uganda zimepata faida kutokana na kupanda kwa bei za kahawa.

Nchi nyingi za Afrika zimechukua sera mwafaka za uchumi na kufanya marekebisho ya miundo ya kiuchumi, hii imeongeza nguvu ya uhai kwa ongezeko la uchumi wa nchi hizo. Kwa kuwa hali ya usimamizi wa mambo ya fedha na ubadilishaji wa fedha umeboreshwa, msingi wa uchumi wa nchi za Afrika umeimarishwa, na uwezo wa nchi za Afrika wa kukabiliana na hatari za nje umeinuka kwa kiasi fulani. Wakati huo huo nchi za Afrika zimepata maendeleo makubwa katika kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza pengo la fedha.

Aidha nchi za Afrika pia zimeongeza nguvu za kuharakisha mchakato wa utandawazi wa uchumi wa kikanda, na kujitahidi kukabiliana na changamoto ziletwazo na utandawazi wa uchumi duniani. Yote hayo yamehimiza vizuri maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika.