Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-24 21:10:53    
Je, ni nani anayefanya "ukoloni mambo leo" barani Afrika?

cri

Katika siku zilizopita, usemi kuhusu China inafanya "ukoloni mambo leo" barani Afrika si kama tu umeonekana katika gazeti la New York Times la Marekani, gazeti la Financial Times la Uingereza, bali pia hata maofisa kadhaa wa serikali na washauri wa serikali pia waliulaani uhusiano kati ya China na Afrika. Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa masuala ya Afrika katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bibi He Wenping alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, vyombo vya habari vya kiserikali vya nchi kadhaa vinaleta hoja ya China kufanya "ukoloni mambo leo" barani Afrika kwa sababu wanaona ushirikiano kati ya China na Afrika umedhuru maslahi yao barani Afrika. Alisema:

Katika miaka kadhaa ya hivi karibuni mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika yanaendelea kwa kasi, zamani makampuni makubwa ya mafuta ya nchi za magharibi pamoja na mambo ya siasa, uchumi na kijeshi ya nchi za magharibi yalikuwa na ushawishi mkubwa sana barani Afrika. Nchi hizo zinapoona ushindani kutoka China zinauchukiza na kuhofia kupoteza maslahi yao, ni sababu ya kimsingi kabisa kwa nchi hizo kutuhumu uhusiano kati ya China na Afrika.

Bibi He Wenping alisema, hakuna msingi hata kidogo kusema China inafanya "ukoloni mambo leo" barani Afrika, kwani hakuna historia yoyote ya ukoloni kati ya China na Afrika, China na Afrika zote zilikumbwa na uchungu wa uvamizi wa ukoloni, pande zote mbili zilikuwa na hisia sawasawa.

Bibi He Wenping alisema, nchi za magharibi zinadai kuwa China kufanya "ukoloni mambo leo" barani Afrika, kwanza zinasema ati China inanyang'anya nishati za Afrika. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, kabla ya China kufika barani Afrika, mapema kwa miaka mingi zaidi nchi za magharibi zilifanya uchimbaji na kunyang'anya maliasili nyingi za nishati za Afrika. Na hivi sasa nchi za magharibi na makampuni makubwa ya kimataifa bado yanaongeza uwekezaji katika sekta ya nishati barani Afrika, na kupanua uagizaji wa mafuta kutoka nchi za Afrika. Hivi sasa uagizaji wa mafuta wa China kutoka nchi za Afrika haujafikia theluthi moja ya ule wa Marekani. Na hali inayostahili kufuatiliwa ni kwamba, uchimbaji wa mafuta wa nchi za magharibi barani Afrika ni uchimbaji wa kunyang'anya, kwa mfano, zilipochimba mafuta ghafi nchini Nigeria, zilisababisha uchafuzi mkubwa sana kwa mazingira ya huko, na kuzidisha migongano kati ya wakazi wa huko na makampuni ya mafuta. Lakini sera ya uchimbaji wa mafuta ya China inatilia maanani ushirikiano wa kunufaishana. Bibi He alisema:

China inazisaidia nchi za Afrika kujenga seti za majengo ya kusafisha mafuta, kuongeza uwezo wa kuyatengeneza, madhumuni ni kuzisaidia nchi za Afrika ziendeleze nguvu zao bora za maliasili kuwa uwezo wa kudumisha maendeleo endelevu katika sekta ya uchumi. Nchi za magharibi zinatuhumu kuhusu China kupata sehemu kadhaa kuchimba mafuta barani Afrika, lakini mbona hazitaji zaidi kuwa China pia imetoa msaada wa dola za kimarekani bilioni 4 kuzisaidia nchi za Afrika kujenga miundo mbinu, kwani China si kama tu inatilia maanani kujipatia maslahi, bali pia inazingatia kuziwezesha nchi za Afrika ziinue uwezo wao wa kiuchumi na kiwango cha teknolojia za uzalishaji.

Kuhusu usemi wa nchi za magharibi ati bidhaa za viwanda vya China zenye bei nafuu zimekalia soko la barani Afrika, Bibi He alikiri kuwa, hali hiyo kweli iko katika soko, lakini hii ni hali isiyoepukika kutokana na utandawazi wa uchumi duniani, lakini wakati huo huo tungeona juhudi ziletwazo na hali hiyo:

Bidhaa za matumizi ya lazima zenye bei nafuu za China zimeinua moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja kiwango cha maisha ya wananchi wa nchi za Afrika na kuongeza uwezo wao wa ununuzi. Aidha kutokana na ongezeko kubwa la biashara kati ya China na Afrika, ongezeko la uchumi wa baadhi ya nchi za Afrika limefikia asilimia 6 kwa mwaka. Na waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao alipofanya ziara barani Afrika ametangaza kuwa China itachukua hatua za kudhibiti uuzaji wa nguo barani Afrika ili bidhaa za nguo za Afrika ziweze kuongeza uwezo wake wa ushindani kwenye soko. Bibi He alisema China na nchi za Afrika zinafundishana katika ushirikiano kati yao, na vitendo vya China vimeonesha hali hiyo halisi.