Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-25 19:31:37    
Usalama wa matumizi ya dawa nyumbani

cri

Watu wengi wamezoea kuweka akiba ya dawa za kawaida nyumbani, wakipatwa na magonjwa madogo kama vile mafua, hawana haja ya kwenda hospitali. Lakini kutokana na matumizi ya ovyo ya dawa, baadhi ya watu si kama tu hawaponi magonjwa yao wanapotumia dawa hizo, bali pia wanadhuru maisha yao. Lakini tunapaswa kuwa na akiba ya dawa gani nyumbani na njia ipi inafaa kuhifadhi dawa hizo? na tunapaswa kujua ujuzi gani wa kimsingi kuhusu matumizi ya dawa?

Kwa kawaida, kila familia ina kisanduku kimoja cha dawa, ni dawa gani zinahifadhiwa kwenye kisanduku hicho? Mwandishi wetu wa habari aliwahoji wapita njia mitaani.

Mkazi wa kwanza alisema, "nyumbani kwangu kuna dawa za kuondoa maumivu, nyingine ni kutibu magonjwa ya mishipa ya damu kwenye moyo, na kutibu dalili za mzio (allergic)."

Mkazi wa pili alisema, "dawa za nyumbani kwangu zote ni za kutibu mafua."

Mahojiano hayo yanaonesha kuwa, dawa za aina ya kwanza zinazohifadhiwa nyumbani ni za kutibu mafua, ya pili ni za kuua vijidudu. Basi kwa kawaida familia zinatakiwa kuweka akiba ya dawa gani? Mdaktari wa hospitali kuu ya jeshi ya Beijing Bw. Liu Duanqi alieleza:

"kwa jumla kuna kanuni kadhaa kuhusu akiba ya dawa zinazopaswa kuwekwa nyumbani. Ya kwanza ni kuwa inafaa kuchagua dawa bora lakini hakuna haja ya kuweka akiba ya dawa nyingi. Kwa kawaida, kiasi cha dawa zinazoweza kudumu kwa siku 3 hadi 5 kinatosha. Kanuni ya pili ni kuwa akiba hiyo inatofautiana kutokana na majira,hali halisi ya sehemu na watu. Kwa sababu katika majira ya siku za joto, dawa za kuzuia mbu ni za lazima, lakini katika majira ya siku za baridi, inafaa kuweka akiba ya dawa za kikohozi. Hali hiyo pia inatofautiana kwenye sehemu mbalimbali, kwa mfano, kama unaishi katika miji mikubwa, kuna maduka mengi ya dawa, basi hakuna haja ya kuweka akiba kubwa ya dawa nyumbani. Aidha, akiba hiyo pia inategemea hali ya afya ya jamaa za famila yako."

Mbali na suala la kiasi gani cha akiba ya dawa kinatakiwa kuwekwa, sisi pia tunapaswa kuzingatia mambo mengi.

Kwanza, sanduku la dawa nyumbani linapaswa kushughulikiwa mara kwa mara, kwa kawaida linashughulikiwa kila baada ya miezi mitatu na sita, tunapaswa kuondoa dawa zilizopitwa na wakati na kubadilisha baadhi ya dawa.

Ya pili, dawa zinapaswa kuwekwa mahali mwafaka. Haifai kuwekwa kwenye sanduku la karatasi au droo, kwa kuwa katika sanduku la karatasi, dawa zinaweza kupatwa na unyevunyevu; na kama dawa ziwekwa kwenye droo, vumbi linaweza kupenya na kuchafua dawa. vyombo bora vya kuhifadha dawa ni vinavyotengenezwa kwa chuma au plastiki. Sanduku la dawa linapaswa kuwekwa mahali pakavu panapopitisha hewa na pasipo na mawnagaza wa jua wa moja kwa moja kwenye jua. Baadhi ya dawa maalum zinatakiwa kuhifadhiwa katika hali ya baridi. Aidha, jambo lililo muhimu zaidi ni kwamba sanduku la dawa linapaswa kuwekwa kwenye eneo lisilofikiwa kwa urahisi na watoto.

aidha, kuhusu matumizi ya dawa, daktari wa hospitali kuu ya jeshi ya Beijing Bi. Zhou Shuming alisema,

"watu wanapaswa kuzoea kusoma maelekezo ya matumizi ya dawa kabla ya kuzitumia. Kama tunavyojua, hivi sasa dawa moja inaweza kuwa na majina mengi tofauti, kama hauzifahamu kikamilifu kabla ya kuzitumia, huenda unaweza kutumia dawa aina moja mara mbili au kukosea kuzitumia."

Kwa mfano, mtu mmoja alitumia dawa za aina 5 ndani ya saa moja kutokana na kuumwa meno, lakini kwa kuwa hakusoma maelekezo kabla kuzitumia, hakujua kuwa dawa hizo zote alizozitumia zote ni za kuondoa maumivu, hatimaye mtu huyo alipatwa na tatizo la dharura la kupoteza uwezo kwa figo.

Mbali na ujuzi huo kuhusu hifadhi ya dawa, bado kuna mambo mengi yanayopaswa kuzingatiwa kabla ya kuzitumia. Ya kwanza, unapaswa kuangalia dawa kwa makini kabla ya kuzitumia. Ingawa baadhi ya dawa bado ziko ndani ya muda wa matumizi, lakini kama rzimebadilika rangi, haziwezi kutumika tena.

Muda wa matumizi ni ukomo wa juu kwa matumizi ya dawa uliopendekezwa na viwanda vya dawa. Lakini kwa sababu mbalimbali, zikiwemo kutohifadhiwa vizuri au kutosafirishwa kwa njia mwafaka, baadhi ya dawa zinaharibika kabla kufika kwa muda wa mwisho wa matumizi ya dawa hizo. Hivyo kama hali hiyo ikitokea, usitumie dawa kama hizo.

Aidha, usinywe pombe wala kuvuta sigara wakati wa kutumia dawa. Kwa sababu dawa zinafanya kazi kwa njia ya kitu kimoja kinachoitwa enzyme, lakini pombe na nicotin zote zinaweza kubadilisha ufanisi wa kitu hicho, hivyo hali hiyo inaweza kusababisha dawa ipoteze ufanisi na hata kuweza kusababisha madhara, hasa haiwapasi watu hawapaswi kunywa pombe baada ya kutumia dawa ya usingizi. Wakati wa kumeza dawa, ni afadhali kutumia maji, wala usitumie juisi, chai au maziwa. Kwa sababu alkali ya chai, protein kwenye maziwa na asidi kwenye juisi zote zinaweza kuathiri dawa na kubadilisha ufanisi wake.