Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-25 19:45:20    
Mapishi ya bilinganya na paja la nguruwe lililokaushwa

cri

Mahitaji:

Paja la nguruwe lililokaushwa gramu 50, bilinganya gramu 150, pilipili mboga moja, pilipili hoho moja, tangawizi gramu 5, chumvi gramu 10, M.S.G gramu 5, sukari gramu 2, mchuzi wa soya kijiko kimoja, mchuzi wa chaza kijiko kimoja na maji ya wanga

Njia:

1. kata paja la nguruwe lililokaushwa liwe vipande, kata bilinganya iwe vipande virefu, kata pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi ya sentigred 60, tia vipande vya tangawizi, pilipili mboga, pilipili hoho, korogakoroga, tia vipande vya paja la nguruwe lililokaushwa, korogakoroga, tia vipande vya bilinganya, korogakoroga, tia chumvi, sukari, M.S.G, mimina mchuzi wa sosi, mchuzi wa chaza, korogakoroga, halafu mimina maji ya wanga korogakoroga na kabla ya kupakua mimina mafuta ya ufuta. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.