Lugha siku zote ni kama "daraja" la kufanya maingiliano kati ya wananchi wa nchi mbalimbali. Kutokana na jinsi mawasiliano ya kibiashara na kiutamaduni yanavyoongezeka siku hadi siku kati ya Morocco na China, ndivyo kujifunza lugha ya Kichina kunavyofuatiliwa zaidi na watu wa nchi hiyo.
Hivi karibuni waandishi wetu wa habari walitembelea Kituo cha utafiti wa China na Morocco kilichoko katikati ya Mji Casablanca nchini Morroco. Mmoroco Bwana Shams Din Hajrawi aliyewahi kusoma nchini China na kupata shahada ya tatu, alishirikiana na wenzake kadhaa wenye nia ya kuhimiza maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Morocco kuanzisha kituo hicho cha utafiti.
Naibu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kituo hicho Bwana Abdul Elah Jamie aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, nia ya kuanzisha kituo hicho ni kukidhi mahitaji ya mawasiliano ya kibiashara yanayozidi kuongezeka siku hadi siku kati ya Morocco na China. Alisema:
Kazi kuu ya kituo chetu hasa ni kufundisha lugha ya Kichina na utamaduni wa China kwa wamoroco wanaoshughulikia kazi katika viwanda na wafanyabiashara, kwani wanataka kufanya biashara na kununua bidhaa nchini China. Kituo chetu kinachagua vitabu vya kujifunza lugha ya Kichina vinavyowafaa wamoroco, kati ya wasomi wa Morocco na wa China wanashughulikia kazi hiyo, Dk Hajrawi ameonesha umuhimu wake mkubwa katika kuchagua vitabu vinavyowafaa wamoroco kujifunza Kichina.
Kaimu wa mkurugenzi wa kituo hicho Bibi Eham Iadad alisema:
Baada ya kuanzishwa kwa kituo cha utafiti wa China na Morocco, kituo hiki kimejenga mazingira ya kuzifanya nchi hizo mbili zielewe utamaduni wa kila upande. Kwa kweli kila upande hauelewi sana utamaduni wa upande mwingine, hivyo kituo chetu kimejenga mazingira kwa ajili ya maingiliano ya utamaduni kati ya pande hizo mbili.
Bwana Jamie alisema kwa kawaida ni taabu kubwa kwa wamoroco kujifunza lugha ya Kichina, lakini hali inayotushangaza ni kuwa hivi sasa wamoroco wengi zaidi wanakuja kwenye kituo chetu kujifunza lugha ya Kichina, na watu wengi zaidi wameahidi kufanya juhudi ili kujifunza lugha ya Kichina. Alisema:
Lugha ni chombo kisichokosekana katika mawasiliano kati ya China na Morocco. Kituo chetu kinawasaidia wamoroco kujifunza lugha ya Kichina. Na kituo chetu pia kinaungwa mkono na serikali za Morocco na China, hii imetutia moto sana. Maofisa wa serikali za China na Morocco wengi wametembelea kituo chetu. Na ubalozi wa China nchini Morocco umetuletea majarida na vitabu vingi vinavyohusu kujifunza Kichina.
Bwana Jamie ameeleza imani yake kuwa, kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kutakuwa kazi yenye matumaini makubwa, kwani Morocco na nchi za Afrika zinataka kuelewa uzoefu wa China wa kuendeleza kwa njia ya amani, katika siku za baadaye nchi za Afrika zitashirikiana zaidi na China. Alisema:
Mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hivi karibuni, hii ni fursa muhimu kwa nchi za Afrika na Morocco kuimiarisha uhusiano na China. Majukumu makubwa ya China ni kujipatia maendeleo kwa amani, haya pia yanahitajiwa barani Afrika na nchini Morocco. Nina imani kubwa kwamba katika siku za baadaye China itakuwa karibu zaidi na nchi za Afrika. Ndiyo maana tumeanzisha kituo hiki cha kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina, ili lugha iweze kutusaidia kufanya mawasiliano na China. Morocco, nchi nyingine za kiarabu na Afrika bado hazielewi sana hali ya China, tunapaswa kuwaelewa wachina, kujua namna wachina wanavyoweza kuifanya nchi yao ipate maendeleo ya haraka, hasa hayo ni maendeleo ya amani, tunatakiwa kufanya vizuri sawasawa na wachina.
Konsela wa ubalozi wa China nchini Morocco Bwana Wang Baoyi aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, upande wa China umeanzisha shughuli mbalimbali zinazohusika katika sekta ya maingiliano ya utamaduni kati ya China na Morocco.
|