Tokea mwezi Aprili mwaka 2003, kutokana na ombi la Umoja wa Mataifa, China imetuma wanajeshi 3975 wa ulinzi wa amani kwenye maeneo matatu ya kubeba majukumu nchini Liberia na Sudan. Hivi karibuni waandishi wetu wa habari walioko Nairobi Kenya walikwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Liberia kuwatembelea wanajeshi wa China wanaolinda amani huko.
Kila siku asubuhi kutokana na sauti ya tarumbeta ya jeshi, maofisa na askari wa kikosi cha uhandisi cha China wanaanza kutekeleza jukumu lao la ulinzi wa amani. Kikosi hicho kinakaa kwenye peninsula moja nyembamba kando ya Ziwa Kivu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wakazi wa huko wenye uchangamfu wanaiita peninsula hiyo kuwa ni "peninsula ya China".
Katika zaidi ya miaka mitatu iliyopita, China imetuma vikosi 6 vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vikiwemo vikosi vya askari wa uhandisi na madaktari, ambapo askari wa kikosi cha uhandisi cha China walikamilisha kazi zaidi ya 100 kama vile ukarabati na ulinzi wa barabara, majengo ya kuegesha ndege, na kuteketeza silaha na risasi, na wametoa mchango mkubwa kwa ajili ya kutuliza hali ya huko na kutekeleza jukumu la Umoja wa Mataifa. Naibu Kiongozi wa kikosi cha 6 cha askari wa uhandisi Bwana Wang Dongsheng alisema:
Tulifanya ukarabati wa viwanja kadhaa vya ndege ambavyo vyote ni sehemu muhimu za kimkakati. Baada ya kukamilisha ukarabati wa viwanja vya ndege tulilisaidia jeshi la ulinzi wa amani la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kulinda utulivu wa eneo zima.
Kazi nzuri walizofanya askari wa uhandisi wa China zinasifiwa sana na maofisa wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Kiongozi wa kikosi cha 6 cha askari wa uhandisi wa China Bwana Di Dianxi alisema:
Mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu tulipata amri ya kututaka tukae kwenye sehemu inayoelekea kwenye Bonde la Kalungu, lakini tulishinda taabu na kupiga kambi katika siku mbili tu baada ya kufika huko, kamanda mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo alipopata habari aliwasifu wanajeshi wa China kuweza kupangwa huko kwa haraka.
Kikosi cha ulinzi wa amani cha China kilitumia muda wa mapumziko yao kulima kwenye ardhi iliyoachwa na kupanda mboga za aina mbalimbali, ndiyo maana sasa mboga walizopanda zinaweza kuwatosheleza, hata vikosi vingine vya ulinzi wa amani vinaweza kupata msaada wao.
Kuhusu uhusiano kati ya kikosi cha ulinzi wa amani cha China na vikosi vya nchi nyingine, Kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa amani cha Uruguay kilichoko karibu na kikosi cha ulinzi wa amani cha China nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo alisema:
Sisi ni majirani pia ni marafiki wazuri, uhusiano kati yetu na wanajeshi wa China ni mzuri zaidi, hata kila mara tunakula chakula katika kikosi cha uhandisi cha China, wakati wa kawaida tunacheza mpira kwa pamoja.
Na wanajeshi wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Pakistan, Bangladesh na Afrika ya kusini vilivyoko huko Kivu wote wanawachukulia wanajeshi wa China kama marafiki zao, hayo yote yanatokana na ustadi mzuri wa ufundi wa kikosi cha uhandisi cha China, na vitendo vya wanajeshi wa China wa kufuata nidhamu na maadili, na kuwa na uchangamfu na adabu.
Wimbo huu ni wimbo unaojulikana nchini China, lakini wimbo huu uliimbwa na mtoto mmoja wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo aitwaye Lawi, ambaye anaishi kwenye peninsula ya Kivu. Kutokana na mawasiliano na wanajeshi wa China, mtoto huyo anajua kuongea vizuri kichina. Alipokutana na waandishi wetu wa habari alisema:
Nafurahi kukutana nanyi, nina majina matatu ya kichina, najua kuongea kichina, wachina wanasema mimi ni rafiki yao. Naona wanajeshi wa China ni wazuri wanatusaidia kujenga barabara.
Katika miaka kadhaa ya kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wanajeshi wa China wametoa misaada mingi kwa wakazi wa huko, na vitendo vyao vya kufuata nidhamu vinaheshimiwa na kusifiwa sana na wakazi wa huko.
Idhaa ya Kiswahili 2006-10-30
|