Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-31 16:02:31    
Serikali ya China yaimarisha udhibiti wa kuhusu uzalishaji chakula

cri

Naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya chakula ya serikali Bw. Qie Jianwei tarehe 25 mwezi Septemba kwenye mkutano wa 10 wa baraza la soko la chakula la China alisema, hivi sasa uzalishaji na usafirishaji chakula wa China umeingia kipindi kipya cha maendeleo, utaratibu wa usafirishaji chakula unaboreshwa hatua kwa hatua, mageuzi ya mashirika ya chakula ya taifa yanaendelezwa kwa kina na uwezo wa udhibiti wa mpango mkuu wa serikali kuu kuhusu uzalishaji chakula unaimarishwa hatua kwa hatua.

Bw. Qie Jianwei alisema kutokana na mazingira bora ya sera za serikali, hali ya hewa na masoko, uzalishaji chakula ulikuwa na ongezeko kubwa katika miaka miwili iliyopita, mazao ya chakula ya majira ya joto na mpunga vimepata mavuno mazuri mwaka huu, wakati uzalishaji chakula katika majira ya mpukutiko unatarajiwa kuwa na mavuno mazuri pia. Kutokana na ongezeko la chakula, tatizo la upungufu wa chakula limepungua kwa kiwango kikubwa, hata hali ya chakula kuzidi mahitaji inatokea kwenye baadhi ya sehemu. Hivyo serikali inatekeleza sera ya kuweka kikomo cha chini cha bei ya kununua chakula kutoka kwa wakulima kwenye baadhi ya sehemu ili kutuliza bei ya chakula kwenye masoko na kulinda hamasa ya wakulima kuzalisha chakula.

Hivi sasa nafasi ya mashirika ya chakula ya serikali kwenye soko la chakula nchini China inapungua hatua kwa hatua, lakini mashirika hayo yanabeba jukumu la utekelezaji wa sera za serikali na udhibiti wa soko la chakula na kuonesha mwelekeo wa sera za serikali kuhusu chakula.

Bw. Qie Jianwei alisema "kanuni za soko ni kanuni za uchumi za kimsingi zinazofuatwa na serikali katika kazi kuhusu chakula, aliongeza kuwa mbinu za kiuchumi ni mbinu muhimu za udhibiti wa uzalishaji chakula kwa mpango wa serikali kuu, hivyo tunatakiwa kufanya utafiti zaidi kuhusu masoko, kufahamu masoko na kudhibiti masoko."

Baadhi ya wataalamu wamesema katika siku za baadaye, serikali itahimiza ushirikiano kati ya mashirika ya chakula ya serikali na mashirika ya chakula ya sehemu za uzalishaji chakula na uuzaji chakula, na kujenga mfumo wa mtandao wa usafirishaji chakula wa China nzima. Tutaimarisha ushirikiano kati ya bandari na mashirika ya chakula ya serikali kuu likiwemo shirika la akiba ya chakula la China, kampuni ya chakula ya China, pamoja na mashirika makubwa ya chakula ya sehemu ya kaskazini mashariki mwa China ikiwemo kampuni ya chakula ya mkoa wa Jilin, kuimarisha uwezo wake, kudumisha vyanzo vya chakula, kujenga mfumo wa kisasa wa usafirishaji chakula na kuimarisha nguvu za ushindani za mashirika makubwa ya chakula ya serikali kwenye soko la chakula.

Idhaa ya kiswahili 2006-10-31