Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-31 15:38:05    
Barua 1031

cri
Msikilizaji wetu Mogire O. Machuki wa kijiji cha Nyankware S.L.P 4-0200 Kisiii Nchini Kenya, anasema katika barua yake kuwa ni imani yake kwamba wafanyakazi wa Idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa ni wazima, yeye ni mzima na anaendelea kusikiliza na kuvifurahia vipindi vya Radio China kimataifa kupitia KBC.

Anasema anaona mwaka 2006 anaona unaenda haraka sana, kulingana na rekodi yake ilifika tarehe mosi septemba 2006, idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa ilikuwa imetimiza miaka 46 tangu iasisiwe mwaka 1960. Hii ni ishara kwamba Idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa kwa zaidi ya miongo minne imepiga hatua kadha wa kadhaa mpaka kufikia ilipofikia sasa.

Lengo lake ni kuwahimiza wasikilizaji wenzake kuwa, ni vizuri wakizidi kuitangaza Radio China kimataifa bila kujali mipaka wala rangi. Ndoto itatimia iwapo siku moja akipita mitaani na kukuta kila mtu akisikiliza matangazo ya Radio China kimataifa. Utamaduni na historia ya China ni vitu vinavyoavutia mno, na kwa vile watu wengi wa na kiu ya kuifahamu China ndani na nje, radio China kimataifa ni daraja muafaka lenye uwezo wa kipekee wa kutosheleza kiu hiyo.

Anasema Vipindi vya Radio China Kimataifa kama alivyowahi kudokeza hapo awali, vinaendelea hatua kwa hatua kuwapa wasikilizaji ukaribu na nchi ya China kwa ujumla. Lakini anasema ombi lake ni kwamba iongezwe nguvu kazi maradufu na ikiwezekana hata vipindi view vinasikika nyakati za asubuhi hapo Afrika Mashariki na kati. Vipindi kama vile Tazama China, Ijue China bado ni vifupi. Ushirikiano mzuri kati ya Radio China Kimataifa na wasikilizaji wake kwa kweli umekomaa na tena ni wa jadi, kama sio ushirikiano wa karibu kati ya Radio China na wasikilizaji wake, basi Radio China Kimataifa isingefikia hapa ilipo sasa, ni imani yake kuwa ushirikiano huo utadumu milele.

Daima huwa anafurahi anaposikia barua za maoni na salamu zikisomwa hewani kutoka kwa wasikilizaji wapya kutoka sehemu mbalimbali duniani, anasema hiyo ni changamoto ya kipekee, na tuzidi kuwathamini na kuwaenzi. Pia anasema anapenda kutuarifu kuwa, zawadi alizotumiwa kutokana na chemsha bongo ya mwaka jana zimefika ingawa bado hajazichukua kutoka katika ofisi ya posta huko Kisii. Imekuwa vigumu sana kwake kwa sababu ya ushuru alioambiwa kulipa wa dola za kimarekani 25 kabla ya kukabidhiwa kifurushi hicho. Huenda zawadi hiyo itaendelea kuhifadhiwa huko mpaka apate fedha za kulipia ushuru. Anaomba ingefaa Radio China Kimataifa ibadilishe mfumo wa kutuma vifurushi kwa wasikilizaji haswa wa Kenya, iwapo kwa siku za baadaye tutatuma zawadi hizo kwa Kituo chetu cha Nairobi Kenya au ubalozi wa China Nairobi halafu zawadi hizo iwasilishwe posta ya Kenya, hakutakuwa na gharama na itakuwa vyema.

Tunasikitishwa sana na hali hiyo aliyokutana nayo Bwana Machuki, kweli labda zawadi yenyewe siyo yenye thamani kubwa, hatujui ni kwanini kifurushi hicho kinatakiwa kulipiwa dola za kimarekani 25, labda wao wanadhani ndani kuna vitu vyenye thamani kubwa! Siku nyingine tukifanya hivyo hakika tunazingatia kwa makini uliyotushauri, hapa tunaomba Bwana Machuki atuelewe. Na kama Bwana Machuki atashindwa kukichukua kifurushi hiki hakuna ubaya sana, siku nyingine tunachukua njia nyingine kumzawadia tena.

Msikilizaji wetu Mwalimu J. Mwana wa Otieno wa Ingati Kwendo Paramena S.L.B 7 Bunyore anapenda kuchukua fursa hii kutoa pongezi wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa kwa jinsi tunavyowatendea wasikilizaji wenu. Anasema yeye binafsi anaridhika na vipindi vya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa ambavyo vinamvutia hata akiwa kazini, hospitali kila siku, anawatakia kila heri. Bw Mwana wa Otieno anaiomba Radio China kimataifa iongeze muda wake wa matangazo walau kwa masaa matatu kwani muda wa saa moja ni mfupi sana. Pia anaona kitu kingine ambacho kinaweza kuboresha vipindi vya Radio China kimataifa ni Chemsha Bongo, na zawadi ambazo zitaipamba Kenya na Afrika ya Mashariki yote, na mwisho anawatakia wafanyakazi wote amani.

Tunamshukuru msikilizaji wetu Mwalimu J. Mwana wa Otieno kwa barua yake inatutia moyo, tutaendelea na juhudi za kuchapa kazi ili kuwarisha zaidi wasikilizaji wetu.

Msikilizaji wetu Philip Machuki wa kijiji cha Nyankware, S.L.B 646 katika barua yake kwanza kabisa anatoa salamu nyingi akitarajia kuwa wafanyakazi wote wa radio china kimataifa ni wazima. Anasema anapenda kutumia fursa hii kutufahamisha kwamba amekuwa akifuatilia matangazo ya Radio China kimataifa siku hadi siku, na kadiri muda unavyokwenda ndio matangazo haya yanavyozidi kufahamika nchini Kenya. Anasema uzinduzi wa 91.9 Fm mjini Nairobi kwa kweli umebadilisha usikivu wa matangazo ya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa. Na kwa sababu hiyo matangazo haya yamepata ladha zaidi na ndio maana barua kutoka Kenya zimeongezeka.

Anaendelea kusema kwa kweli chemsha bongo ya mwaka huu imempatia fursa njema ya kufahamu mengi kuhusu Radio China Kimataifa, ni lini ilianza, watangazaji wake, na mengi yanayowahusu wasikilizaji. Anaomba kuwa kama ikiwezekana makala ya nne ya Chemsha Bongo itachapishwa kwenye jarida la daraja la urafiki, kwani kufanya hivyo watakuwa na kumbukumbu njema sana juu ya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa, na mwisho anawatakia wafanyakazi wote wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa afya njema na maisha marefu na kama atapata fursa ya kuwa wa kwanza katika chemsha Bongo hivi karibuni ataonana nasi.

Tunamshukuru Philip Machuki kwa barua yake, tunaona shauri lake ni nzuri, siku hizi tuna kazi nyingi sana, hivi karibuni Mkubwa wa Wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hapa Beijing hivi karibuni, kila siku tuna kazi nyingi, hivyo uchapishaji wa jarida dogo la urafiki umeahirishwa kwa muda mrefu. Tuombe radhi kutoka kwa wasikilizaji wetu.

Msikilizaji wetu Ali Hamis Kimani wa Alaro shule ya Msingi, S.L.B 61-40224 Othoro, Kadongo nchini Kenya, anatoa salamu nyingi kutoka kwake na kwa familia yake akitegemea kuwa wafanyakazi wote wa Radio China Kimataifa hatujambo na tunachapa kazi vilivyo, dhumuni la barua yake ni kutoa shukrani kwa huduma nzuri na maridhawa. Hivi majuzi amepokea jarida la China Today, bahasha zilizolipiwa na kadi za salamu, anashukuru kwa yote. Yote yaliyomo katika zawadi hizo yanamfurahisha hususan picha inayoonesha "Vivutio vya delta ya mto lulu" Ama kweli inashangaza sana kuona kijiji kilichojengwa juu ya maji. Ni matumaini yake kuwa siku moja atapata fursa ya kutembelea China iliyojaa maajabu mengi na mazuri. Anamaliza kwa kuomba Mungu aendelee kutupa afya njema na yeye anaendelea kusubiri kwa hamu matokeo ya Chemsha Bongo ya mwaka huu.

Msikilizaji wetu Richard Chenibei Mateka wa S.L.B 65, Kapkateny Mlima Elgoni Nchini Kenya, anasema yeye ni mzima wa afya na anatarajia kuwa sisi wafanyakazi wote wa Radio China kimataifa tuna afya njema. Msikilizaji huyu alizaliwa mwaka 1973 huku Mlima Elgoni, alipomaliza masomo ya shule ya msingi alijiunga na shule ya sekondari ya Kapsokwaony. Alipomaliza kidato cha nne alijiunga na chuo cha utalii cha huko mjini Nakuru ambapo alisoma kwa mihula miwili tu kutoka na matatizo ya karo.

Anasema kutokana na matatizo hayo alikwama kidogo kuendelea na masomo. Hata hivyo sasa hivi anaendelea kufutilia matangazo yetu kila siku na pia anafurahi kutuarifu kuwa barua tunazomtumia huwa anazipata kwa wakati. Hii ni hali nzuri kwa yeye kwani anasema huko Mlima Elgon gharama za kutumia Kompyuta na kutembelea tovuti ni kubwa. Ni matumaini yake kuwa idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa itazidi kung'ara na kuwanufaisha wasikilizaji wake, kwani China na Kenya zinategemeana kimaendeleo.

Tunawashukuru wasikilizaji wetu Ali Hamis Kimani na Richard Chenibei Mateka kwa barua zao. Ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu wengi watatuletea barua kutoa maoni na mapendekezo yao ili kutusaidia kuboresha vipindi vyetu.

Idhaa ya kiswahili 2006-10-31