Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-01 21:17:18    
Mapishi ya vichipukizi vya mianzi na uyoga

cri

Mahitaji:

Vichipukizi vya mianzi gramu 150, uyoga gramu 50, mchuzi wa chaza kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, kiasi kidogo cha chumvi, sukari, M.S.G, maji ya wanga, na mafuta ya ufuta

Njia:

1. osha uyoga , ukate uwe vipande vipande. Kata vichipukizi vya mianzi viwe vipande vipande. Chemsha maji, weka vipande vya vichipukizi vya mianzi kwenye maji ya moto, halafu vipakue.

2. washa moto kisha tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya uyoga na vichipukizi vya mianzi kwenye sufuria, mimina mafuta ya chaza, mchuzi wa sosi, tia chumvi, sukari, M.S.G, korogakoroga na mimina maji kidogo, chemsha kwa dakika 5, halafu mimina maji ya wanga, korogakoroga, mimina mafuta ya ufuta, na upakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.