Shughuli kubwa za maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika ya kusini zilianza tarehe 1 Novemba huko Pretoria, Afrika ya kusini.
Mliosikia ni muziki wa jadi wa China uitwao Maua ya jasmini uliopigwa kwenye ufunguzi wa shughuli kubwa za maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika. Shughuli hizo ziliandaliwa kwa pamoja na ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, wizara ya usanii na utamaduni ya Afrika ya kusini na ubalozi wa China nchini Afrika ya kusini, madhumuni yake ni kufanya maingiliano ya kiutamaduni ili kuongeza maelewano kati ya China na Afrika ya kusini. Mkurugenzi wa ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China Bwana Cha Wu alisema kwenye ufunguzi kuwa, maingiliano ya kiutamaduni ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika ya kusini, pia ni njia nzuri ya kuongeza maelewano kati ya wananchi wa China na Afrika ya kusini. Serikali ya China inapenda kufanya maingiliano mengi zaidi na nchi za Afrika ili kutimiza wazo la kupata maendeleo kwa amani, ustawi wa pamoja na kujenga dunia yenye masikilizano.

Bwana Li Xiangping wa ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China aliyeshughulikia shughuli hizo alijulisha sababu ya serikali ya China kuchagua Afrika kusini kuanzisha shughuli za maingiliano ya kiutamaduni, akisema:
China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na Baraza la Afrika ni bara ambalo nchi nyingi zaidi zinazoendelea ziko huko, na Afrika ya kusini ni nchi iliyoendelea zaidi kiuchumi barani Afrika, utamaduni wa nchi hiyo ni wa aina mbalimbali, hivyo nchi hiyo inasifiwa kuwa ni nchi ya "upinde wa mvua", Afrika ya kusini ni nchi kubwa barani Afrika, na China ni nchi kubwa barani Asia, hivyo uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni muhimu sana.
Bwana Li Xiangping aliongeza kuwa kuanzisha shughuli za maingiliano ya kiutamaduni nchini Afrika ya kusini pia kutokana na mahitaji ya kuendeleza urafiki wa jadi kati ya China na Afrika, na kuongeza maelewano kati ya wananchi wa China na Afrika ya kusini. Mwaka huu ni mwaka wa 50 tangu China na nchi za Afrika zianzishe uhusiano wa kibalozi, na vilevile ni mwaka wa nane tangu China na Afrika kusini zianzishe uhusiano wa kibalozi. Mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na mkutano wa 3 wa mawaziri itafanyika mjini Beijing. China na Afrika zilikumbana na ajali za kihistoria zinazofanana, na hivi sasa zinakabiliwa na jukumu la pamoja la maendeleo.

Meneja mkuu mtendaji wa Mamlaka ya Jumba la makumbusho ya historia na utamaduni la Afrika ya kusini lililoko Pretoria Bwana Makglo Makglo alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, maingiliano hayo ya kiutamaduni yanasaidia kuongeza maelewano kati ya wananchi wa China na Afrika ya kusini, ana matumaini kuwa China na Afrika ya kusini zitaimarisha zaidi ushirikiano kati ya sekta ya utamaduni. Alisema:
Naona ushirikiano kati ya Afrika ya kusini na China utaimarishwa siku hadi siku, kwani makubaliano husika yaliyosainiwa na serikali za nchi hizo mbili yameweza kutekelezwa.
Shughuli hizo za maingiliano ya kiutamaduni zitafanyika kwa mwezi mmoja nchini Afrika ya kusini, ambapo maofisa waandamizi watatoa hotuba, Maonesho ya sanaa na hazina za China na Maonesho ya picha zilizopigwa kwa kamera kuhusu hali ya China yatafanyika nchini humo, na vikundi vya muziki na ngoma za Enzi ya Tang, mchezo wa Gongfu, muziki na ngoma za taifa la China na kikundi cha kuonesha mavazi na mapambo ya makabila mbalimbali ya enzi mbalimbali ya China pia vitafanya maonesho yao huko Pretoria na Cape Town, aidha wiki ya filamu za China itafanyika kote nchini Afrika ya kusini kwa kupitia Kampuni ya utangazaji ya Afrika ya kusini. Kama alivyosema waziri wa usanii na utamaduni wa Afrika ya kusini Bwana Pallo Jordan, kwa kupitia shughuli hizo za maingiliano ya kiutamaduni, wananchi wa Afrika ya kusini wataijua zaidi China kuhusu utamaduni, sanaa na falsafa zake.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-02
|