Mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na Mkutano wa 3 wa mawaziri ilifanyika kwa ushindi kuanzia tarehe 3 hadi 5 Novemba, ambapo marais, viongozi wa serikali au wawakilishi wao wa China na nchi 48 za Afrika walijadili mikakati ya ushirikiano na kutafuta maendeleo ya pamoja ya siku zijazo, mkutano huo umefungua ukurasa mpya wa urafiki.
Gazeti la Renminribao la China tarehe 6 limetoa makala ya mhariri ikisifu sana mkutano huo. Makala hiyo imesema miaka 50 iliyopita, China mpya ilianzisha rasmi uhusiano wa kibalozi na nchi za Afrika. Katika miaka mingi iliyopita China na Afrika zilihurumiana na kuungana mkono katika mapigano ya kujipatia uhuru na ukombozi, kulinda mamlaka ya nchi na kujenga nchi. Katika kipindi kipya cha kusitawisha uchumi na kutimiza maendeleo kwa China na nchi za Afrika, pande mbili ziliamua kufanya mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, tukio hilo lina umuhimu wa kihistoria wa kufuata nyayo za siku zilizopita na kufungua ukurasa mpya.
Chini ya kauli mbiu ya urafiki, amani, ushirikiano na maendeleo, Mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulipitisha Azimio la mkutano na mpango wa utekelezaji wa mkutano wa baraza hilo, kuthibitisha kuendeleza uhusiano wa aina mpya wa kimkakati na kiwenzi, na kufanya mpango kabambe kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo.
Makala hiyo ya mhariri imeeleza kuwa, mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika umezidisha urafiki wa jadi kati ya wananchi wa China na Afrika, ambapo viongozi wa China na nchi za Afrika walipokumbusha mambo yaliyopita, waliona kwa kauli moja kuwa urafiki kati ya wananchi wa China na Afrika umetia mizizi sana mioyoni mwa wananchi wa China na Afrika, huu ni mali ya pamoja ya pande hizo mbili yenye thamani, hivyo wamedhamiria kukuza zaidi urafiki huo siku za mbele.
Mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika umeongeza nguvu mpya kwa ushirikiano kati ya China na Afrika. Rais Hu Jintao alitangaza hatua 8 za China za kuimarisha ushirikiano halisi na nchi za Afrika, akieleza hisia za urafiki za serikali ya China na wananchi wake kwa wananchi wa Afrika na kueleza matumaini ya dhati ya kusukuma mbele maendeleo ya pamoja ya China na Afrika, hatua hizo zimesifiwa na viongozi wa nchi za Afrika. Pande hizo mbili zimekaza nia ya kutumia fursa, kupanua ushirikiano, kusaidiana na kuleta manufaa kwa wananchi wa pande hizo mbili.
Mkutano huo umehimiza ujenzi wa utaratibu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Pande mbili za China na Afrika zimekubali kuimarisha zaidi ushirikiano ndani ya baraza hilo, ili baraza hilo lioneshe umuhimu wake zaidi katika kuanzisha mazungumzo ya pamoja na kufanya ushirikiano halisi. '
Makala hiyo imesema mkutano huo umevumbua wazo jipya kuhusu ushirikiano kati ya kusini na kusini. China ni nchi kubwa kabisa inayoendelea na Afrika ni bara ambalo nchi nyingi kabisa zinazoendelea ziko huko. China na Afrika kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa aina mpya wa kimkakati na kiwenzi, na kufanya juhudi za kutafuta maendeleo na ustawi wa pamoja, hayo ni majaribio mapya ya ushirikiano kati ya kusini na kusini, ambayo yanasaidia kuhimiza mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea.
Makala hiyo imesema mkutano huo umevutia macho ya walimwengu, ushirikiano kati ya China na Afrika ni sehemu muhimu ya kazi ya dunia nzima ya kuendeleza ushirikiano, China na Afrika kutimiza maendeleo ya pamoja hakika zitatoa mchango mkubwa kwa amani na maendeleo ya dunia.
Makala hiyo imesema, mkutano huo umeanzisha mustakabali mpya wa ushirikiano kati ya China na Afrika, China itaendelea kuziunga mkono nchi za Afrika katika mambo yao ya kulinda amani, na kuendeleza uchumi, na nchi za Afrika zina matumaini ya dhati kwamba China itapata mafanikio makubwa zaidi katika ujenzi wa nchi, pande hizo mbili zikishikirikiana kwa dhati hakika hali mpya ya urafiki na ushirikiano itaonekana katika nyanja mbalimbali.
|