Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-08 18:44:09    
Familia ya wakerkezi inayozingatia elimu

cri
Kabila la wakerkezi ni moja kati ya makabila 55 madogomadogo nchini China, ambao wengi wao wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, kaskazini-magharibi mwa China. Kabla ya kuasisiwa kwa China mpya, kutokana na tabia ya kuhamahama ya kabila hilo, asilimia 80 hadi 90 ya watu hao hawakujua kusoma wala kuandika, lakini baada ya maendeleo ya zaidi ya nusu karne, kabila la wakerkezi limepata maendeleo makubwa, na elimu inayachangia sana maendeleo hayo.

Hayo ni mahojiano yaliyofanyika kwenye familia moja ya kabila la wakerkezi. Kutokana na mahojiano hayo, mwandishi wetu wa habari amefahamu sana jinsi watu wa kabila la wakerkezi wanavyotilia maanani elimu.

Familia ya Bw. Abdu Kader ina watoto wanne: binti wa kwanza Alima amefaulu mtihani wa kujiunga na shahada ya pili ya lugha ya kiingereza kwenye Chuo Kikuu cha Xinjiang, binti wa pili Saweiya ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Ualimu cha Huazhong mjini Wuhan; binti wa tatu Gulmire anasomea kozi ya upashanaji wa habari kwenye Chuo kikuu cha Xinjiang; na mtoto wa kiume atajiunga na Chuo cha udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Shihezi cha Xinjiang. Bw. Abdu Kader akizungumzia kwa nini familia yake imeweza kuwa na wanafunzi 4 wa Chuo Kikuu, anasema:

"Kabila la wakerkezi ni kabila linalohamahama, watu wachache waliweza kusoma shuleni kutokana na hali mbaya ya kimaumbile na ukosefu wa fedha. Babu yangu hakuwahi kwenda shule, lakini alipambana na matatizo mbalimbali na kumhimiza baba yangu kusoma. Wakati huo, kulikuwa hakuna barabara kwenye sehemu hiyo, hali ambayo ilimfanya baba yangu kwenda shuleni kwa kutembea kwa miguu kilomita themanini hadi tisini kila siku. Hii inanifanya nijue kuwa kusoma ni jambo muhimu sana kwetu tangu nikiwa mtoto."

Kwa kuondoa matatizo mbalimbali, baba yake bw. Abdu Kader alikuwa mwalimu baada ya kuhitimu kutoka shule ya Ualimu.

Familia ya mke wa Bw. Abdu vilevile inatilia maanani sana elimu, mwaka huu watoto wachache wa kiume wa kabila la wakerkezi waliweza kujiunga kwenye shule za sekondari, kutokana na kukabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa jamii, wazazi wa mke wa Bw. Abdu walimhimiza asome na awe mwalimu wa shule ya awali baada ya kuhitimu.

Uzoefu huo unawafanya Bw. Abdu na mke wake wafahamu umuhimu wa elimu. Bw. Abdu anaona kuwa elimu ni muhimu sana ama kwa makabila au kwa nchi. Kutokana na maendeleo ya maisha ya wakerkezi, ana lengo la kuwahimiza watoto wake kupata elimu ya juu, ili watoe mchango kwa ajili ya maendeleo ya kabila la wakerkezi.

Lakini ingawa ni jambo la kufurahisha watu kwa familia moja kuwa na wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu, lakini ada ya masomo ni tatizo kubwa kwa familia ya Bw. Abdu yenye kipato cha chini. Bw. Abdu anasema:

"Binti yangu alizaliwa mwaka 1982, wakati huo mshahara wangu ulikuwa Yuan 58 kwa mwezi, na nilijadiliana na mke wangu tuwe tunatumia Yuan 30 kwa mwezi kama mfuko wa elimu. Hivi sasa mshahara wangu umefikia Yuan 2400, na tunahifadhi Yuan 150 kwa mwezi kama mfuko wa elimu kwa watoto."

Mke wa Abdu pia anasema:

"Tulikumbwa na matatizo mbalimbali wakati watoto wetu wanne walipokuwa wanasoma, hata tuliomba mkopo kutoka benki, hata hivyo tumejenga hatua kwenye nia yetu ya linahimiza watoto kwenda shule. Ingawa watu wa kabila la wakerkezi wanahimiza watoto wa kike kufanya kazi za nyumbani, lakini sikufanya hivyo, nafurahi sana kuona walifanya mazoezi ya nyumbani baada ya kumaliza masomo shuleni."

Hivi sasa watoto wa Bw. Abdu wamerithi mila na desturi za familia hiyo. Familia ya Binti wa kwanza Alima ilijifunza uzeofu wa wazazi wake na kuandaa mfuko wa elimu kwa mtoto, na kuweka Yuan 300 kwenye mfuko huo kwa mwezi.

Kutokana na juhudi mbalimbali, watoto wote wa familia ya Bw. Abdu wamepata elimu ya chuo kikuu, mbali na hayo kozi zao wanazosomea ni kozi zinazopendwa na watu wengi. Bw. Abdu alisema kozi wanazosomea watoto wake zinachaguliwa kutokana na mahitaji ya maendeleo ya China.

Bw. Abdu ana matumaini makubwa juu ya watoto wake. Anasema:

"Hivi sasa mtoto wangu mkubwa anasomea shahada ya pili, ni matumaini yangu kuwa watoto wangu wengine pia watapata elimu ya shahada ya pili, na halafu shahada ya tatu. Aidha natumai kuwa watoto wangu wote watarudi nyumbani kwetu na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya sehemu yetu."

Mbali na hayo, Bw. Abdu pia anawatakakuwa watoto wake wataweza kusoma katika nchi za nje, na kumiliki ujuzi na teknolojia za kisasa duniani, ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya China. Matumaini hayo yanaungwa mkono na watoto wenyewe.

Matumaini hayo yanaungwa mkono na watotowake. Alima anasema:

"Kiwango cha kiingereza cha watu wa nyumbani kwetu bado kiko chini, hivyo nina matumaini makubwa ya kuwasaidia wajifunze lugha ya kigeni, ili kuwasaidia wafahamu zaidi dunia, na kulitambulisha kabila letu kwa nchi mbalimbali duniani." Mtoto wa kiume Erisbek anasema:

"Watu wachache wa kabila letu wanafahamu udaktari, nataka kujifunza upasuaji ili niweze kutoa matibabu kwa watu wa kabila letu."