Wakuu wa nchi, viongozi na maofisa waandamizi wa serikali kutoka nchi 48 za Afrika hivi karibuni waliwasili Beijing, China kushiriki kwenye mkutano wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika. Kwenye mkutano huo, rais Hu Jintao wa China akiiwakilisha serikali ya China alitangaza hatua 8 mpya za kisera za kuunga mkono maendeleo ya nchi za Afrika, na juu ya msingi huo waziri mkuu wa serikali ya China Bw. Wen Jiabao alitoa pendekezo la kuhimiza maendeleo ya uchumi na biashara ya China na Afrika. Sasa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika umeingia kipindi kipya.
Katika miaka ya karibuni, maingiliano ya kiuchumi na kibiashara yanafanya kazi muhimu za kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi za Afrika. Hivi sasa China imekuwa mwenzi wa tatu mkubwa katika shughuli za biashara za Afrika. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2005, jumla ya thamani ya uwekezaji wa China imefikia dola za kimarekani milioni 6,270 na kujenga viwanda vya aina mbalimbali zaidi ya 800 barani Afrika. Thamani ya biashara kati ya China na Afrika inatarajiwa kuzidi dola za kimarekani bilioni 50 mwaka huu. Aidha serikali ya China inatoa misaada ya kiuchumi isiyoambatana na masharti yoyote ili kuzisaidia nchi za Afrika kufanya ujenzi wa miundo-mbinu na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii.
Katika muda wa mkutano wa wakuu wa nchi wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika, pia ulifanyika mkutano wa 2 wa wanaviwanda wa China na nchi za Afrika, ambapo waziri mkuu Wen Jiabao alisema pande mbili za China na Afrika zinatakiwa kuimarisha maingiliano ya kiuchumi na kibiashara,
"China na Afrika zinatakiwa kuboresha kwa mfululizo muundo wa biashara na kujitahidi kufikisha thamani ya biashara kati ya China na Afrika hadi dola za kimarekani bilioni 100 mwaka 2010. China inahamasisha viwanda vya China kuwekeza katika nchi za Afrika, kuzipatia nchi za Afrika teknolojia na uzoefu wa usimamizi, vilevile inakaribisha viwanda vya Afrika vije kuwekeza nchini China. China itaongeza misaada hatua kwa hatua kwa nchi za Afrika kulingana kiwango cha maendeleo yake, kuzisaidia nchi za Afrika kukuza maendeleo ya uchumi na jamii."
Bw. Wen Jiabao alisema China itaendelea kufungua masoko na kusamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazosafirishwa kwa China na chi zilizoko nyuma kabisa kiuchumi za Afrika, na kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika; kuongeza miradi ya msaada kwa Afrika, hususan ile inayohusika na maisha ya watu ikiwemo ya kilimo, matibabu, elimu na hifadhi ya mazingira. China itazidisha utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi wa Afrika, na kuimarisha ushirikiano wa biashara ya huduma ikiwemo utalii, mambo ya fedha na mawasiliano ya habari ili kuleta ulingano wa biashara kati ya China na Afrika.
Serikali ya China inakuza maingiliano ya kiuchumi na kibiashara na nchi za Afrika kwa kufuata kanuni za kunufaishana na kuhimiza ushirikiano wa viwanda vya pande hizo mbili, jambo hilo linapongezwa na serikali na watu wa nchi mbalimbali za Afrika. Kwenye mkutano wa wakuu wa Beijing waziri mkuu wa Ethiopia Bw Meles Zenawi, ambayo ni nchi mwenyekiti mwenza wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika, alisema, maendeleo ya dunia yanahusiana na Afrika na China, na ushirikiano kati ya Afrika na China unaweza kunufaisha watu wa pande zote mbili.
"Naona tumekabidhiwa majukumu makubwa, tunatakiwa kuboresha mazingira ya kuziwezesha sekta za viwanda kuhimizana na kuongeza biashara na uwekezaji ili kunufaisha watu wa pande mbili. China na Afrika zinaweza kutimiza lengo la kunufaishana kwa kutumia ubora wao.
|