Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-08 19:42:58    
Mapishi ya viazi mbatata na maharagwe marefu

cri

Mahitaji:

Viazi mbatata gramu 200, pilipili nyekundu moja, maharagwe marefu gramu 10, chumvi gramu 5, sukari gramu 20, kiasi kidogo cha maji ya wanga, juisi ya chungwa gramu 30.

Njia:

1. kata viazi mbatata, pilipili nyekundu, maharagwe marefu yawe vipande vipande, weka vipande vya viazi ndani ya maji ya wanga.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria tia vipande vya viazi mbatata vikaange mpaka viwe na rangi ya hudhurungi kasha vipakue.

3. washa moto tena tia vipande vya pilipili nyekundu na maharagwe marefu, korogakoroga, halafu mimina maji kidogo, juisi ya chungwa, chumvi, sukari, korogakoroga, tia vipande vya viazi mbatata, korogakoroga, baada ya kuchemka, mimina maji ya wanga, korogakoroga, kisha ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.