Vyombo vya habari vya Marekani tarehe 8 adhuhuri vilitangaza matokeo ya uchaguzi wa kipindi cha katikati wa bunge la Marekani vilisema, Chama cha demokrasia cha Marekani kilipata viti zaidi ya 228 kwenye baraza la chini la bunge la Marekani, na kunyakua madaraka yake ya udhibiti kiliyopoteza katika uchaguzi wa mwaka 1994, ambapo Chama cha Republican kitakabiliwa pia na ushindani mkali kwenye baraza la juu la bunge la Marekani. Ushindi wa Chama cha demokrasia utaleta changamoto kwa sera za ndani na nje za Marekani.
Lakini kwa kweli changamoto ya kwanza imekikabili chama ha Republican, yaani waziri wa ulinzi wa taifa Bwana Donald Rumsfeld amelazimika kujiuzulu kutokana na shinikizo. Akiwa waziri wa ulinzi wa Marekani aliyeshika madaraka kwa muda mrefu zaidi kuliko wengine katika historia ya Marekani, Bwana Rumsfeld aliongoza vita dhidi ya Afghanistan na vita dhidi ya Iraq. Kutokana na uamuzi wake wa makosa, hali ya Iraq haikubadilika kuwa nzuri kutokana na kupinduliwa kwa utawala wa Saddam, badala yake hali hiyo inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, hata imefikia ukingoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na askari wa jeshi la Marekani nchini Iraq wamepata vifo na majeruhi makubwa, kweli wanakaa kwenye janga la kutojua kusonga mbele au kurudi nyuma. Kushindwa kwa Chama cha Republican, sababu kubwa moja ni kutokana na malalamiko mengi ya wapiga kura juu ya sera inayofuata serikali ya Bush kwa Iraq.
Kabla ya uchaguzi kufanyika wanachama wa Chama cha demokrasia walisema kama watapata ushindi katika uchaguzi, wataitilia shinikizo serikali ya Bush, na kutaka kumwondoa madarakani Rumsfeld. Hata baadhi ya wahafidhina na magazeti ya jeshi pia wamekosoa hadharani sera za Marekani kwa Iraq, na kutaka Rumsfeld ajiuzulu. Hivi sasa Chama cha demokrasia kimepata ushindi, katika hali hiyo ingawa Bwana Rumsfeld hapendi kujiuluzu, hana la kufanya tena ila tu kukabidhi ombi lake la kujiuzulu. Lakini kujiuzulu kwake hakutaweza kabisa kunyamazisha malalamiko mengi ya wapiga kura juu ya sera za serikali kwa Iraq, wapiga kura hao wanataka kubadilisha sera. Ndiyo maana huenda Bush atafanya marekebisho makubwa ya sera kuhusu suala la Iraq.
Mbali na suala la Iraq, ushindi wa chama cha demokrasia pia utaleta changamoto kwa sera ya serikali ya Bush kuhusu masuala ya mambo ya ndani, ambapo serikali ya Bush italazimika kuacha juhudi zake kadhaa za utekelezaji wa sera za ndani, zikiwemo sera ya kufanya mageuzi ya mfumo wa huduma za jamii, hata pamoja na hatua za kupunguza ushuru zilizopitishwa kwenye bunge la taifa.
Kwa ujumla Bunge la taifa la Marekani litakalodhibitiwa na Chama cha demokrasia huenda litaweza kumfanya rais Bush awe rais anayechechemea. Lakini watu fulani wanaona kuwa katika hali ya uwiano ya madaraka kati ya vyama viwili, vyama hivyo viwili huenda vitafanya ushirikiano wenye ufanisi zaidi, ili kuhimiza kihalisi matatizo sugu kama vile suala la wahamiaji haramu. Kwani kila upande hautaki kubeba lawama kuhusu uzembe wa kazi. Dalili kadhaa zimeonekana katika mazungumzo kati ya kiongozi wa chama cha demokrasia katika baraza la chini Bibi Nancy Pelosi na rais Bush, hao wawili walipoongea kwa njia ya simu wote waliahidi kutafuta ushirikiano bila kuzingatia tu maslahi ya chama kimoja, ili kukabiliana kwa pamoja masuala yanayoikabili Marekani.
Chama cha demokrasia kimetoa ahadi kama hiyo kwa sababu kimeona kuwa kimedhibiti baraza la chini la bunge la taifa, lakini hali hii inakisaidia pia inaweza kuleta matatizo kwake. Hali ya kukisaidia ni kuwa, chama hicho kitapata miaka miwili ya kupima sera zake ambazo zinawavutia wapiga kura au la ili kuendelea kuzifuata, na kufanya maandalizi ya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu. Lakini hali isiyokisaidia ni kwamba, kama chama cha demokrasia hakitafanya vizuri na kuwafanya wapiga kura wafe moyo, basi wapiga kura hao vilevile watakitupilia mbali chama cha demokrasia katika uchaguzi mkuu wa rais.
|