Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-10 15:09:49    
Mkurugenzi wa WHO akabiliwa na changamoto kubwa

cri

Bi. Margaret Chan kutoka Hong Kong ameteuliwa rasmi kuwa mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO kwenye mkutano uliofanyika tarehe 9 mjini Geneva. Katika miaka ya karibuni magonjwa ya kuambukiza yamekuwa yanatokea mara kwa mara na kuhatarisha maisha ya binadamu, kwa hiyo Bi. Margaret Chan atakabiliwa na changamoto kubwa kupambana na hali hiyo.

Hadi leo binadamu bado hawajashinda ugonjwa wa kifua kikuu uliodumu kwa miaka mingi, na katika miongo kadhaa ya karibuni magonjwa kama Ukimwi, ugonjwa wa ebola, ugonjwa wa maini, Sars, homa ya mafua ya ndege na magonjwa mengine zaidi ya 30 yanahatarisha maisha ya binadamu, zaidi ya hayo vijidudu na virusi vya magonjwa vinaenea na kukwamisha maendeleo ya jamii. Yote hayo ni tatizo la kiafya linalofuatiliwa sana na jumiya ya kimataifa, na WHO itakayoongozwa na Bi. Margaret Chan inapaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo.

Hivi sasa, homa ya mafua ya ndege pamoja na homa ya mafua ya binadamu ni tishio kubwa kwa binadamu. Mara nyingi wataalamu wanasisitiza kwamba homa ya mafua ya binadamu pengine italipuka ghafla bila watu kujua kabla na kusababisha hasara kubwa kwa maisha ya binadamu na mali. Kwa hiyo, WHO inapaswa kuanzisha mfumo wa utabiri na kuandaa hatua mfululizo ili kupambana na hali hiyo. Bi. Margaret Chan alisema atajitahidi kusukuma utafiti wa chanjo na hasa chanjo ya homa ya mafua ya ndege, ataimarisha uwezo wa WHO katika kupambana na milipuko ya magonjwa duniani.

Ukimwi ni janga kubwa la binadamu. Kutokana na ugonjwa huo baadhi ya nchi za kusini mwa Afrika zimepoteza mafanikio yaliyopatikana katika miongo kadhaa, na wastani wa miaka ya kuishi umekuwa mdogo kuliko miaka 30 iliyopita, lengo la kuwapatia matibabu watu milioni 3 wenye virusi vya Ukimwi kabla ya mwishoni mwa mwaka 2005 lilishindwa kutimizwa. Watu wanaona kwamba ugonjwa huo hauwezi kudhibitiwa duniani bila maendeleo kutapatikana katika pande tatu kwa pamoja yaani tiba, kinga na uenezi wa elimu kuhusu ugonjwa huo. Zaidi ya hayo magonjwa kama kifua kikuu, malaria, polio, udhibiti wa uvutaji sigara na magonjwa sugu pia ni matatizo muhimu kwenye ratiba ya WHO.

Bi. Margaret Chan aliwahi kusema akichaguliwa kuwa mkurugenzi wa WHO kazi yake nyingine muhimu ni kusaidia nchi zinazoendelea kuboresha mfumo wa afya. Umaskini unadhuru afya na afya mbaya inasababisha watu kuwa maskini. Shirika la Afya Duniani WHO lina jukumu kubwa la kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa, WHO ina jukumu zito. WHO ina jukumu la kusaidia nchi maskini kuimarisha uwezo wao wa kuwa na maendeleo endelevu, kuimarisha harakati za afya na kuongeza fedha katika mambo ya afya, ili kupunguza kiasi cha vifo vya watoto, kuboresha afya ya wajawazito, kupata maji safi na mazingira mazuri ya afya. Baada ya kuteuliwa Bi. Margaret Chan aliposema atatumia hali ya afya barani Afrika kama ni kigezo cha kazi ya WHO alipigiwa sana makofi.

Bi. Margaret Chan pia alisema, WHO ina haja ya kufanyiwa mageuzi ili kuinua ufanisi wake. Kwenye mkutano mkuu wa WHO baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi Bi. Margaret Chan alisema, huu ni wakati wake wa furaha sana, lakini naona kuwa ana jukumu kubwa. Alisema anatambua kuwa kazi yake inahusiana moja kwa moja na afya ya binadamu, na alipopongezwa alisema ana hakika kwamba atafanikiwa katika kazi yake aliyopewa na WHO.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-10