Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-10 20:39:39    
Mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta za uchumi na biashara utaimarishwa zaidi

cri

Mkutano wa mazungumzo kati ya viongozi na wajumbe wa sekta za viwanda na biashara kutoka China na Afrika na Mkutano wa 2 wa wanakampuni wa China na Afrika ulifunguliwa tarehe 4 hapa Beijing. Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo akisema, wakati wa kuadhimisha mwaka wa 50 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Afrika uanzishwe, serikali ya China imetangaza hatua mpya za kufanya ushirikiano halisi na nchi za Afrika, ambapo mawasiliano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika utahimizwa zaidi.

Waziri mkuu Wen Jiabao alisema ushirikiano kati ya China na Afrika una nguvu kubwa na mustakbali mpana. Alisema: 

China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, pande hizo mbili zinaweza kusaidiana vizuri kiuchumi, zina nguvu kubwa ya kufanya ushirikiano, mustakabali wa ushirikiano ni mpana, tunapaswa kudumisha hali usawa kati yetu na nchi za Afrika, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana ili matokeo ya ushirikiano huo yalete manufaa kwa wananchi wa China na Afrika.

Waziri mkuu Wen Jiabao alitoa mapendekezo matano kuhusu kuinua kwa pande zote kiwango cha ushirikiano kati ya China na Afrika. Mapendekezo hayo yanahusu kupanua biashara kati ya pande hizo mbili, kujitahidi kuongeza thamani ya biashara kati ya China na Afrika ifikie dola za kimarekani bilioni 100. Pia amesema China itaendelea kufungua soko, kufuta ushuru wa forodha kwa bidhaa nyingi zinazosafirishwa na nchi za Afrika zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo na kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika; China itazihimiza kampuni za China ziwekeze katika nchi za Afrika, kuhamisha teknolojia na uzoefu wa usimamizi unaofaa kutumika barani Afrika, pia kuzikaribisha kampuni za Afrika kuja China kuwekeza na kujiendeleza; China itapanua hatua kwa hatua misaada yake kwa nchi za Afrika, hasa kutoa misaada kwa miradi ya kupunguza umaskini, miradi na matibabu na afya inayohusiana na maisha na uzalishaji wa nchi za Afrika; kuhimiza ushirikiano kati ya kampuni za China na Afrika na kuimarisha kazi ya kuzisaidia nchi za Afrika kutoa mafunzo kwa watu wenye ujuzi.

Bwana Wen Jiabao alisema ushirikiano kati ya China na nchi mbalimbali za Afrika unalenga kunufaisha kila upande. Misaada ya China kwa nchi za Afrika yote inatokana na mahitaji ya nchi za Afrika na kuamuliwa baada ya kufanya majadiliano, hii imefanya juhudi za kuchangia maendeleo ya Afrika. Alitoa mwito wa kuitaka jumuiya ya kimataifa ifanye juhudi za pamoja na kuendelea kuongeza misaada kwa Afrika. Alisema:

Siku zote tunaona kuwa, kuungana mkono na kusaidiana kati ya nchi na nchi kunaleta manufaa kwa kila upande, daima hatuwezi kusahau uungaji mkono wenye thamani wa nchi nyingi za Afrika kwa ajili ya China kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi. Tunapenda kufanya ushirikiano wa dhati na wa kunufaishana na nchi za Afrika ili kupata maendeleo kwa pamoja.

Hotuba ya waziri mkuu Wen Jiabao ilikubaliwa na viongozi wa nchi za Afrika na wanakampuni wa China na Afrika. Rais Paul Kagame wa Rwanda alipotoa risala alisema, Rwanda, soko la pamoja la kusini mashariki mwa Afrika COMESA pamoja na Bara zima la Afrika, zote zina matumaini ya kupanua zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na China.

Uzoefu wa China umetupatia mwangaza, ambapo tumepata mengi kutokana na uhusiano mzuri kati ya China na Afrika. Tunapenda kuimarisha uwekezaji na biashara kati ya Rwanda na China, kutimiza uwiano kati ya biashara na uwekezaji. Tunaishukuru serikali ya China kwa kufuta ushuru wa forodha kwa bidhaa kadha wa kadha za nchi za Afrika, na tunatumai kuwa pendekezo la kufungua soko litapanua zaidi ili nchi nyingi zaidi zinufaike na bidhaa nyingi zaidi ziingie kwenye soko.

Mfanyabiashara kutoka Uganda Bwana Vincent Seny alisema:

Safari hii nimekuja China kutafuta fursa ya biashara ili kupata wenzi wa ushirikiano nchini China, kwani ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika unapanuka zaidi siku hadi siku, nashughulikia biashara ya kilimo, hasa maua, kama nitapata wenzi wa biashara nchini China, nitauza maua ya Uganda nchini China.