Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-14 16:01:05    
Mustakabali mzuri wa ushirikiano wa nishati wa nchi za Asia ya mashariki

cri

Katika miaka ya karibuni, ongezeko la uchumi wa Asia ni kubwa zaidi kuliko kiwango cha wastani duniani, ambapo thamani ya biashara kati ya nchi za Asia ya mashariki zikiwemo China na Japan, pia inaongezeka kwa mfululizo. Hivi sasa suala la nishati limekuwa changamoto inayoikabili dunia yetu, ambapo nchi na sehemu za Asia ya mashariki zinaimarisha ushirikiano kwenye eneo la nishati, na mustakabali wa ushirikiano wa nishati hakika utakuwa mzuri zaidi katika siku za baadaye.

Ushirikiano wa biashara wa Asia ya mashariki umekuwa sehemu yenye hamasa kubwa zaidi katika ushirikiano wa Asia, ambayo inahimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya sehemu hiyo. Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya biashara kati ya nchi za Asia ya mashariki imezidi nusu ya jumla ya thamani ya biashara ya nchi hizo, wakati thamani ya uwekezaji kati ya nchi za Asia ya mashariki inachukua theluthi mbili za jumla ya thamani ya mitaji iliyowekezwa. Lakini wakati uchumi unapokuzwa kwa haraka, tatizo la nishati linazidi kubwa.

China ni nchi kubwa kwenye sehemu ya Asia, na uchumi wake ulikuwa na ongezeko la kasi kwa miaka mingi, na imekabiliwa shinikizo kubwa la nishati. Mwaka jana, serikali ya China ilitoa sera za kujenga jamii ya kuokoa rasilimali na kuhifadhi mazingira ya asili, kubadilisha mtindo wa ongezeko la uchumi, si tu kusisitiza kuokoa nishati nchini China, bali pia inashiriki kwenye ushirikiano wa nishati duniani.

Suala la nishati siyo suala linalozikabili nchi zinazoendelea kama China peke yake, bali ni suala linalozikabili nchi zote za dunia. Naibu kiongozi wa taasisi ya nishati ya serikali Bw. Xu Dingming amesema, uendelezaji na matumizi ya nishati endelevu ni njia pekee ya utatuzi wa suala la nishati duniani. Alisema,

"Pamoja na maendeleo ya uchumi wa dunia, suala la nishati na mazingira limekuwa kubwa, endapo suala hilo halitatatuliwa ipasavyo, siyo tu kwamba lengo la maendeleo endelevu la jamii ya binadamu litashindwa kutimizwa, bali pia mazingira ya kuishi kwa binadamu na ubora wa maisha vitaathiriwa vibaya. Rasilimali za nishati endelevu ni nyingi, ni safi na zinaweza kutumiwa milele. Kuimarisha uendelezaji na matumizi ya nishati endelevu ni njia pekee ya utatuzi wa matatizo ya nishati na mazingira yanayokuwa makubwa kila siku inayopita, na pia ni njia pekee ya kutimiza lengo la kupata maendeleo endelevu kwa jamii ya binadamu."

Serikali ya China imetambua umuhimu na haraka ya suala la nishati. Tarehe 1 mwezi Januari mwaka huu, China ilianza kutekeleza "sheria ya nishati endelevu" na kubuni sera 12 zinazofuatana na sheria hiyo. Aidha idara ya hifadhi ya mazingira ya taifa ya China inavihamasisha viwanda vitumie teknolojia ya kuokoa nishati kwa shughuli za kudhibiti vitu vya uchafuzi na utoaji vitu vya uchafuzi wa viwanda.

Ili kuimarisha uokoaji wa nishati, mwezi uliopita kamati ya kudumu ya bunge la umma la taifa ilishauri kutoza kodi ya matumizi hadi kwa nishati isiyo endelevu na bidhaa husika yakiwemo makaa ya mawe ili kuzuia matumizi ya ovyo ya nishati na uchimbaji wenye uharibifu na kuhimiza viwanda kuzingatia kubana matumizi ya nishati. Naibu spika wa bunge la umma la taifa Bw. Li Tieying alisema, lengo la hatua hiyo ni kudhibiti ongezeko la kasi la sekta inayotumia nishati kwa wingi. Alisema,

"Kufanya haraka kutoza kodi ya mafuta ya petroli, na kutunga sera za fedha za kuhimiza matumizi ya bidhaa zinazookoa nishati; Kutoidhinisha ujenzi wa miradi isiyolingana na kigezo cha matumizi ya nishati ili kuzuia ongezeko kubwa la sekta inayotumia nishati kwa wingi. Licha ya hayo, tutaendeleza nishati mpya na nishati endelevu, kusisitiza sera za kiuchumi mbinu za kuokoa nishati, kuanzisha utaratibu wa 'anayebana matumizi ya nishati anafaidika', kuweka matumizi ya fedha ya kuokoa nishati katika bajeti ya serikali ili kuwa na uhakika wa kifedha wa kutimiza lengo la China la kuokoa nishati."

Katika miaka ya hivi karibuni, China iliweka "mpango wa maendeleo ya nishati endelevu wa kipindi kirefu na cha wastani" na moja ya maudhui muhimu ni kujifunza uzoefu wa nchi za nje wa uendelezaji wa matumizi ya nishati endelevu, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa nishati na kujenga mfumo imara wa nishati wa uchumi wa China. Naibu kiongozi wa Naibu kiongozi wa taasisi ya nishati ya serikali Bw. Xu Dingming alisema, kutokana na kuongeza kutegemeana kwa uchumi wa China na wa nchi nyingine za Asia ya mashariki, hivyo katika upande wa nishati ushirikiano unatakiwa kuwa mkubwa zaidi kuliko ushindani. Alisema,

"Ili kuhakikisha usalama wa nishati wa dunia, tunatakiwa kuanzisha na kutekeleza ushirikaino wa kunufaishana, maendeleo ya pande nyingi na usalama wa nishati mpya wa uhakika. Tumekuwa tukishirikiana na Asia ya mashariki na Asia ya kaskazini mashariki katika suala la nishati, katika miaka ya karibuni tumekuwa na maingiliano mengi na Japan na Korea ya Kusini, tunakaribisha nchi za Asia ya mashariki kushiriki kwenye uendelezaji wa nishati endelevu ili kuhakikisha usalama wa nishati wa Asia ya mashariki."

Bw. Xu Dingming alisema, maendeleo ya China yanahusiana sana na ya Asia ya mashariki, thamani ya biashara kati ya China na nchi za Asia ya mashariki inachukua kiasi cha 60% ya jumla ya thamani ya biashara ya China, na uwekezaji wa nchi na sehemu za Asia ya mashariki nchini China inachukua zaidi ya 60% ya jumla ya mitaji iliyowekezwa na nchi za nje.

Kwa kuwa uokoaji nishati na hifadhi ya mazingira nchini China viko katika kipindi cha mwanzo, uendelezaji na matumizi ya nishati endelevu vinakumbwa na baadhi ya matatizo ya kimasoko na kiwango cha chini cha teknolojia, hivyo serikali ya China inahimiza kampuni za nchi za nje ziwekeze zaidi kwenye eneo hilo. Mtafiti wa ngazi ya juu wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa nishati ya Japan Bw. Akihiro Kuroki anaona kuwa, mustakabali wa soko la uokoaji wa nishati nchini China ni mzuri, na kuna nafasi kubwa ya kufanya ushirikiano kwenye eneo la uokoaji wa nishati kati ya China na Japan. Alisema,

"Hivi sasa kuna mradi mmoja unaotekelezwa kati ya pande mbili za China na Japan, mradi huo ni kuhusu kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati. Hivi sasa China ni muhimu sana kwa kuinua ufanisi wa nishati kwenye sehemu ya Asia ya mashariki."

Kutokana na kufuata mpango wa maendeleo ya nishati endelevu wa China, katika miongo kadhaa ijayo China itaendeleza nishati endelevu, ambayo itainufaisha China na kuleta fursa kwa kampuni nyingi za Asia ya mashariki.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-14