Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-15 14:42:49    
Tuwe macho na "utetezi wa kuwa na silaha za nyuklia' kurudia nchini Japan

cri

Tarehe 14 mkutano wa baraza la mawaziri la Japan ulipitisha jibu kwa chama kisichotawala cha Daichi kuhusu suala la Japan kuwa na silaha za nyuklia au la, jibu hilo linasema, "katiba ya amani ya Japan haipingi Japan kuwa na silaha za nyuklia, ili mradi tu silaha hiyo zitumike kwa ajili ya kujilijnda". Lakini jibu hilo linasisitiza kuwa "lakini serikali ya Japan haina mpango wa kujadili upya kuhusu kanuni tatu za kutodhibiti silaha za nyuklia". Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Japan kuonesha msimamo wake kwa maandishi kuhusu umiliki wa silaha za nyuklia nchini Japan.

Ukweli ni kwamba "utetezi wa kuwa na silaha za nyuklia" umekuwepo kwa muda mrefu nchini Japan, lakini kutokana na kuwa Japan ni nchi pekee iliyopatwa janga la silaha za nyuklia duniani, watu wa Japan wanapinga sana nchi yao kuwa na silaha hizo. "Utetezi wa kuwa na silaha za nyuklia" hauungwi mkono na watu wengi nchini Japan, lakini baada ya Korea ya Kaskazini kufanya majaribio ya silaha za nyuklia suala hilo limeanza kuzungumzwa tena nchini Japan.

Tarehe 15 mwezi uliopita, mkuu wa chama cha Jimintou Bw. Shoichi Nakagawa alisema, kuna haja ya kuzungumzia suala la Japan kuwa na silaha za nyuklia au la; Tarehe 18 mwezi huo waziri wa mambo ya nje Bw. Taro Aso alisema hivyo hivyo. Kuhusu suala hilo waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe alisema, kuwa na silaha za nyuklia sio chaguo la Japan na kanuni ya kutokuwa na silaha za nyuklia nchini Japan haitabadilika, lakini pia alisema, watu wana uhuru wa kutoa maoni, usemi wake huo ni sawa kuiachia nia ya kuwa na silaha za nyuklia iendelee na ienee zaidi.

Maoni kuhusu Japan kuwa na silaha za nyuklia yamesababisha wasiwasi katika nyanja za vyombo vya habari na siasa. Gazeti la Japan "Asahi Shimbun" lilichapisha makala ya mhariri ikisema, "Japan ikitaka kuwa na silaha za nyuklia, ni lazima ijitoe kutoka kwenye 'mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia', Japan ambayo ni nchi pekee iliyoshambuliwa kwa silaha za nyuklia itapoteza msimamo wake wa kuitaka dunia iteketeze silaha za nyuklia, na itapoteza imani ya jumuyia ya kimataifa." Gazeti la West Japan Daily pia lilichapisha makala ikisema, "kama Japan inaheshimu 'kanuni tatu za kutokuwa na silaha za nyuklia' ni kweli wala si udanganyifu, basi majadiliano kuhusu suala la kuwa na silaha za nyuklia hayafai kufanywa."

Sambamba na hayo, watu wa sehemu mbalimbali nchini Japan wanafanya maandamano ya kupinga maoni ya Japan kuwa na silaha za nyuklia. Kwenye mji wa Hiroshima mbele ya magofu ya mlipuko ya bomu la nyuklia watu walifanya maandamano ya kukaa wakitaka kuzifanya 'kanuni tatu za kutokuwa na silaha' ziwe za kisheria. Mkurugenzi wa shirikisho la waathirika wa silaha za nyuklia Bw. Sunao Toboi alisema, "Silaha haziwezi kuwaletea wanadamu furaha, mazungumzo kuhusu kuwa na silaha za nyuklia yamemalizika na yamepita. Waziri mkuu wa zamani wa Japan Bw. Shoichi Nokagawa anaficha sare ya kijeshi chini ya suti yake." Wakazi wa mji wa Nagasaki pia walifanya maandamano ya kukaa katika bustani ya amani mjini humo wakipinga 'utetezi wa Japan kuwa silaha za nyuklia'.

Wataalamu wanaona kwamba ni lazima watu wawe macho, kwa kawaida usemi kuhusu utetezi wa kuwa na silaha huwa wa kawaida, na baadaye utakuwa wa watu wengi na mwishowe utakuwa wa watu wote.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-15