Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-15 16:50:33    
Mapishi ya steki ya kuku

cri

Mahitaji

Nyama ya kidari cha kuku gramu 300, chumvi kijiko kimoja, chembechembe za kukolea ladha kijiko kimoja, unga wa pilipili manga kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, yai moja, ufuta gramu 20, unga vijiko vitano

Njia

1. pigapiga nyama ya kidari cha kuku kwa kisu, halafu uiweke kwenye bakuli moja, tia chumvi, chembechembe za kukolea ladha, unga wa pilipili manga, kasha mvinyo wa kupikia, korogakoroga.

2. koroga yai, halafu chovya nyama ya kidari cha kuku kwenye yai na unga.

3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe nyuzi ya asilimia 50, weka nyama ya kidari ya kuku kwenye sufuria, ikaange mpaka pande mbili za nyama ya kidari cha kuku ziwe rangi ya hudhurungi, kasha ipakue.

4. kata nyama ya kidari cha kuku iwe vipande vipande na uviweke kwenye sahani. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.