Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-16 16:53:53    
Maisha mapya ya wafugaji wa kabila la Wamongolia wa China

cri

Mji wa Erdos upo katika sehemu ya magharibi ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani wa China, ambako wanaishi watu wengi wa kabila la Wamongolia. zamani sehemu hiyo ilikuwa na hali mbaya na mazingira asili na hali duni ya kimaendeleo. Lakini hivi sasa wafugaji wa kabila la Wamongolia wametambua umuhimu wa mazingira asili, na kutekeleza miradi ya kuboresha mazingira, huku wameanza kupata maendeleo. Mwandishi wetu wa habari alitembelea kijiji cha Menkeqing kilichopo Erdos, na kujionea maisha mapya ya Wamongolia wa huko.

Alipokuwa akielekea kwenye kijiji cha Menkeqing, mwandishi wa habari aliona nyumba mbalimbali za wafugaji zikiwa zingezungikwa na miti. Kuingia kijijini alimkuta mfugaji mmoja aitwaye Xiao Selin, ambaye alikuwa amepaka lori kwa majani makavu ya mahindi na kutaka kuyasafirisha hadi zizi la kufuga ng'ombe. Alimkaribisha mgeni nyumbani na kumletea vyakula vilivyotengenezwa na maziwa. Nyumbani kwa mfugaji huyo mwandishi wetu wa habari aliona televisheni na chombo cha VCD, na mfugaji huyo alinunua simu ya mikono na lori, hali hiyo ilimshangaza mwandishi wa habari, kwani alifahamishwa kuwa miaka 10 iliyopita watu wa huko walikuwa wanaishi maisha duni tofauti na sehemu nyingi. Wakati huo kulikuwa hakuna umeme, simu wala barabara ya kuunganisha sehemu za nje, ambapo farasi walitumika katika shughuli za mashambani na mwasiliano na sehemu ya nje.

Ofisa mmoja wa huko Bw. Wang Ping alisema "Awali kijiji cha Menkeqing kilitengana na sehemu nyingine, kwani mbuga za huko zilimezwa na jangwa, mimea na barabara ziliharibika. Watu walipaswa kutembea kwa miguu au kwa kupanda farasi. Serikali iliwahi kukarabati barabara, lakini kutokana na ufugaji wa jadi kuharibu mazingira asili, baada ya kupita kwa upepo mkali wenye machanga, barabara hizo zikaharibika."

Ili kutatua tatizo hilo, serikali ya huko ilitenga fedha zaidi katika miradi ya kuboresha mazingira asili. Hatua ya kwanza ilikuwa kupanda miti, na iliyofuta ilikuwa kupiga marufuku ufugaji wa jadi wa kuwachunga mifugo kwenye mbuga mkubwa, badala yake iliwahamasisha wafugaji wafuge ng'ombe na mbuzi ndani ya zizi. Mradi mwingine ilikuwa ni ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, umeme na maji.

Mfugaji Xiao Selin alimwambia mwandishi wa habari kuwa, hatua hizo zilisaidia kuboresha mazingira ya huko. Alisema  "Kabla ya kutekeleza hatua ya kufuga mifugo zizini, mbuga zilikuwa si nzuri, lakini baada ya hatua hiyo kutekelezwa, mbuga zilianza kufufua, na sehemu zilizomezwa na jangwa kubadilika kuwa oasis. Hapo awali kulikuwa na hali duni ya mawasiliano, hakuna huduma za umeme, televisheni wala hatuna simu ya mikono. Katika miaka 10 iliyopita, maisha yetu yaliinuka, hivi sasa wastani wa pato la familia ya wafugaji ni kati ya Yuan elfu 30 na 40 kwa mwaka."

Mfugaji huyo alikumbusha akisema, mwanzoni wazee kadhaa walikuwa wakishikilia ufugaji wa jadi, hawakufurahia hatua ya kufuga ng'ombe na mbuzi zizini. Lakini baada ya kuina matokeo ya utekelezaji wa hatua hiyo, mbuga ulifufua mwaka hadi mwaka, wazee hao walifurahia hatua hiyo.

Katika nyumba ya mfugaji mwingine Bw. Alate ambaye ni jirani wa Bw. Xiao Selin, mwenye nyumba alikuwa akizungumza na rafiki yake kwa njia ya simu. Baadaye alimwambia mwandishi wa habari (sauti 4) "Kabla ya kuwa na simu, hatukufahamu mahitaji ya sokoni. Wakati huo tulikuwa tukichukua mifugo au nyama tukitembelea sehemu mbalimbali, tukifanya biashara ya kubahatisha. Hivi sasa tuna simu za nyumbani na simu ya mikono, ni njia nyepesi kwetu kufahamishwa mahitaji ya sokoni. Kwa kupia simu, nafahamu bei ya nyama na kama wanunuzi wapo. Halafu naweza kuamua kwenda sokoni au la."

Wafugaji wa kijiji hicho walieleza kuwa, kabla ya mwaka 1998 watoto wengi wa huko walikuwa wakiacha masomo kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi. Lakini hivi sasa pato la wafugaji limeongezeka na idadi ya watoto wanaosoma shuleni pia imeongezeka. Mwaka jana watoto 10 wa kijiji hicho walifaulu mitihani ya kuandikishwa na vyuo vikuu.

Si kama tu watoto waliotimiza umri wa kwenda shuleni walipata nafasi ya kusoma, bali pia wafugaji wenyewe wamejifunza mengi kutoka kwa vitabu, kwa hiyo mtizamo na maisha yao yamebadilika. Ofisa wa huko Bw. Wang Ping alisema "Naona mabadiliko makubwa yametokea hapa Menkeqing, mabadiliko hayo yametokea katika mazingira asili, zana za miundo mbinu na pia mtizamo wa watu wa huko. Hivi sasa hapa kwetu wanaume kwa wanawake, wazee kwa watoto, wote wana pilikapilika za kazi siku zote, hali ambayo ni tofauti kabisa na ile ya zamani. Hivi sasa watu wanaishi kwa kutimiza malengo yao mbalimbali. Lakini hapo awali burudani pekee za watu wa huko zilikuwa kupiga maji na wanaume walikuwa wanaonekana kuwa wamelewa kila siku."

Sambamba na kuinuka kwa kiwango cha maisha, watu wanahitaji burudani za aina mbalimbali. Hivi sasa njia mojawapo ya kujiburudisha kwa wafugaji wa huko ni kuimba nyimbo na kupiga muziki. Nyumbani kwa mfugaji Bw. Bater, wafugaji wanakutana mara kwa mara wakicheza muziki kwa kutumia seti moja ya kipaza sauti iliyonunuliwa kwa Yuan elfu 10 na serikali ya huko.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-16