Katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira umekuwa ushirikiano wa sekta mpya kati ya China na Afrika, wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unafanyika, ushirikiano huo kati ya China na Afrika umejadiliwa zaidi.
Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa umefanyika kwa karibu wiki mbili huko Nairobi, Kenya, namna ya kuzisaidia nchi za Afrika zikabiliane na mabadiliko ya hali ya hewa, namna ya kuhifadhi mazingira, na kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto, ni masuala yanayofuatiliwa zaidi na nchi mbalimbali zinazohudhuria mkutano huo. Naibu mkurugenzi wa idara ya mikataba katika wizara ya mambo ya nje ya China Bwana Su Wei ambaye amehudhuria mkutano alisema, ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira una mustakbali mpana sana.
China na nchi za Afrika zimefanya ushirikiano katika mambo mengi kuhusu kuhifadhi mazingira, kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, China imeahidi kutoa dola za kimarekani bilioni 5 kwa ajili ya ushirikiano kati ya pande hizo kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira, fedha hizo zimeweka msingi mzuri wa ushirikiano huo. China imepata mafanikio mengi na uzoefu mwingi katika kazi za kuhifadhi mazingira, baada ya kubadilishana maarifa na uzoefu, na kutoa mafunzo kwa watu wa nchi za Afrika wanaoshughulikia uhifadhi wa mazingira, kuzisaidia nchi za Afrika ziongeze uwezo wa kuhifadhi mazingira, ushirikiano kati ya China na Afrika katika uhifadhi wa mazingira utasukumwa mbele zaidi.
Katika miaka ya hivi karibuni, idara za uhifadhi mazingira za China na nchi za Afrika zimeanzisha ushirikiano wenye ufanisi. Mwezi Oktoba mwaka 2003, idara kuu ya uhifadhi wa mazingira ya China ilizialika balozi zaidi ya 40 za nchi za Afrika zishiriki kwenye shughuli za China za uhifadhi wa mazingira zinazoelekea kushirikiana na nchi za Afrika. Mwezi Februari mwaka 2005, ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira ulianzishwa rasmi. Mwezi Machi mwaka 2006, kilizinduliwa rasmi "Kituo cha mazingira ya China na Afrika katika Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa", ambapo ushirikiano halisi wa kuhifadhi mazingira umefanyika kwa kina siku hadi siku kati ya China na nchi za Afrika. Ofisa wa wizara ya mazingira ya Togo Bwana Tomyeba Komi ambaye anayehudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa huko Nairobi, Kenya alisema, China na nchi za Afrika zina maoni mengi ya pamoja kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na suala la mazingira. Alisema:
Kuna ushirikiano mzuri kati ya China na nchi nyingi za Afrika, kwa mfano Togo imetuma watu wengi kushiriki kwenye semina mbalimbali ili kupata ufundi wa kilimo na ufundi wa kushughulikia taka. Kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, tuna ushirikiano barabara, tuna mapendekezo ya namna moja, na tuko katika hali ya namna moja, hivyo tunashirikiana kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na tunajadili kwa pamoja mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mjumbe kutoka Tanzania ambaye pia ni katibu wa ofisi ya makamu wa rais Bwana Bubaka Raja pia ameeleza maoni kama hayo. Alisema:
Siku zote tuko pamoja na China, tuna imani kuwa tutapata maendeleo ya pamoja, kwani wachina wanatujua, na sisi ni marafiki zao. Na muhimu zaidi ni kuwa tunapaswa kuelewa kuwa, tukihifadhi vizuri mazingira yetu, ndipo uchumi wetu unapoweza kuendelezwa.
Mjumbe wa Kenya Profesa wa Chuo kikuu cha Nairobi Bwana Richard Odingo alieleza matumaini yake kuwa mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira yataimarishwa zaidi, kwani ushirikiano huo utasaidia kuhifadhi mazingira na maendeleo endelevu ya China na Afrika, pia utachangia kazi ya uhifadhi mazingira duniani na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Alisema:
Ushirikiano kati ya China na Afrika ni thabiti sana, tunaamini kuwa ushirikaino huo utaimarishwa zaidi, tunatumai kuwa serikali ya China itaendelea kuunga mkono mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kuongeza maelewano kati yetu.
Idhaa ya Kiswahili 2006-11-17
|