Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-20 19:51:46    
Mapendekezo ya kujenga kanda ya Asia na Pasifiki yenye masikilizano yanafuatiliwa zaidi kwenye mkutano wa wakuu wa APEC

cri

Mkutano wa 14 usio wa rasmi wa wakuu wa Shirika la ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC umefungwa tarehe 19 huko Hanoi, mji mkuu wa Vietnam baada ya kutolewa kwa Azimio la Hanoi. Ofisa mwandamizi wa zamani wa China katika shirika hilo Bwana Wang Yusheng tarehe 20 alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, mkutano huo unasaidia maendeleo mazuri ya kasi ya Shirika la APEC, pia unasaidia kuhimiza kutatuliwa ipasavyo kwa matatizo makubwa na yenye taabu katika hali ya kikanda na kimataifa. Bwana Wang alisema mapendekezo aliyotoa rais Hu Jintao wa China kwenye mkutano huo kuhusu kujenga kanda ya Asia na Pasifiki yenye masikilizano yamekubaliwa na pande mbalimbali na kuchukuliwa kuwa lengo la pamoja la wanachama wa shirika la APEC.

Bwana Wang alisema mapendekezo hayo yanalingana na mahitaji ya maendeleo ya zama tulizo nazo na kuonesha nia na matumaini ya wananchi wa kanda hiyo. Alisema:

Kwa kufuata njia ya APEC yaani kutambua aina nyingi za utamaduni, kuruhusu kuchukua njia zenye unyumbufu, kufanya mashauriano kwa hiari na kwa kujiamulia, kuongeza wazo jipya kuhusu usalama kwenye msingi wa kuaminiana, ili kuondoa kabisa wazo la vita baridi, ndipo shirika la APEC lenye masikilizano litajengwa hatua kwa hatua, ambapo ukoo mkubwa wa APEC wenye masikilizano utaweza kuondoa kihalisi migongano mbalimbali yenye utatanishi, na kukabiliana na changamoto kwenye sekta ya usalama usio wa jadi, kusukuma mbele amani na maendeleo na kutimiza ustawi wa pamoja.

Wakati wa mkutano huo mikutano ya pande mbili mbili pia imetia nguvu mpya ya uhai kwenye kujenga kanda ya Asia na Pasifiki yenye masikilizano. Mkutano kati ya marais wa China na Marekani ni moja ya mikutano hiyo. Bwana Wang alisema mazungumzo kati ya rais Hu Jintao wa China na rais Bush wa Marekani ni yenye juhudi, ambayo yameonesha maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya China na Marekani katika miaka ya hivi karibuni. Alisema:

Katika mwaka mmoja uliopita tangu mkutano wa wakuu wa APEC ufanyike mwaka jana, uhusiano kati ya China na Marekani uko katika mchakato wa maendeleo mazuri. Hasa baada ya kukutana mara kwa mara kwa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, nchi hizo mbili zimeongeza maoni ya pamoja kuhusu masuala mengi makubwa, maoni hayo ya pamoja pia yanakaribia zaidi maslahi yale ya pamoja ya nchi hizo mbili. Katika hali hiyo, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, mazungumzo ya kimkakati wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili pamoja na mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na nchi hizo mbili yote yanapanuka siku hadi siku, ambapo hata vyombo vya habari vya Marekani pia vinaelekea kufuatilia zaidi maendeleo ya China.

Baada ya waziri mkuu wa Japan Bw Shinzo Abe kushika madaraka, amekutana na Rais Hu Jintao wa China mara mbili katika muda wa zaidi ya mwezi mmoja tu, hali hii yenyewe imeonesha juhudi mpya za kuuwezesha uhusiano kati ya China na Japan uendelee katika hali ya kawaida.

Aidha hali inayostahili kufuatiliwa ni kwamba, katika hali ambayo mazungumzo ya raundi ya Doha yamekwama, mkutano huo umetoa taarifa ukiahidi kuwa kila nchi mwanachama wa Shirika la APEC itafanya juhudi zake ili kuhimiza mazungumzo hayo yarudishwe tena. Bwana Wang alisema hayo ni matokeo makubwa pia ya mkutano huo. Alisema:

Viongozi wa nchi wanachama wa APEC wameeleza msimamo wao imara kuhusu suala hilo katika Azimio la Hanoi, na hata katika siku ya kufunguliwa kwa mkutano huo taarifa husika ilitolewa, naona hili ni jambo muhimu, mkutano huo umetoa mwito wa kuhimiza mazungumzo ya raundi ya Doha ili yaweze kufanikiwa.

Bwana Wang pia alisema, mkutano huo pia umefikia maoni ya pamoja kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-20