Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-21 16:35:09    
Sekta ya uzalishaji mitambo ya sehemu ya kaskazini mashariki mwa China yapata maendeleo ya kasi

cri

Mwaka 2004 China ilianza kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki mwa China, ikinuia kurejesha ustawi wa zamani kwa kituo hicho cha kazi za viwanda. Tangu kuanza kutekelezwa kwa sera hizo na kufanya marekebisho ya muundo wa uzalishaji mali katika miaka miwili iliyopita, maendeleo ya uchumi ya sehemu ya kaskazini mashariki yalipata nafasi nzuri, hususan sekta ya uzalishaji mitambo ilikuwa na maendeleo ya kasi.

Sehemu ya kaskazini mashariki ni kituo cha kwanza cha kazi za viwanda kilichojengwa nchini China, ambacho sekta ya uzalishaji wa mitambo ilichukua nafasi muhimu sana katika uchumi wa China. Lakini tokea mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, kituo hicho kilichowahi kutoa mchango mkubwa kwa ujenzi wa mambo ya viwanda wa China, kiliachwa nyuma sana na sehemu ya pwani ya kusini mashariki ya China. Mkurugenzi wa ofisi ya ustawishaji wa sehemu ya kaskazini mashariki ya baraza la serikali Bw. Zhang Guoban alipofanya uchambuzi kuhusu chanzo cha kuzorota kwa kazi za viwanda za sehemu ya kaskazini mashariki, alisema,

"Kituo cha kazi za viwanda cha sehemu ya kaskazini mashariki kiliathiriwa sana na uchumi wa kimpango, uchumi wa kitaifa ulichukua karibu nafasi yote, na tofauti kubwa na miji inayotekeleza sera za ufunguaji mlango ya pwani ya kusini ni kuwa, bado inasitasita katika utekelezaji wa sera za ufunguaji mlango."

Utaratibu na mfumo wa kizamani unashindwa kuendana na maendeleo ya sasa, katika miaka ya 90 ya karne iliyopita viwanda vingi vya serikali vya sehemu ya kaskazini mashariki vilikuwa katika hali ya kutapatapa na kukabiliwa na mgogoro usiowahi kutokea. Bw. Zhan Xiaoming alikuwa mhandisi wa kiwanda No. 3 cha mitambo cha Shenyang baada ya kuhitimu masomo yake katika chuo kikuu mwaka 1986. Karibu kutimiza muda wa miaka 10 tangu aanze kazi, siku moja Bw. Zhan Xiaoming ghafla alisikia habari moja iliyomshtusha sana, kuwa kiwanda chao kimefilisika, yeye na wafanyakazi karibu elfu 10 wa kiwanda hicho wakakosa kazi. Alisema,

"Baada ya kuhitimu masomo yangu nilipewa kazi katika kiwanda hicho, nimefanya kazi kwa miaka mingi hapa, lakini hivi sasa kiwanda hicho kimeanguka, moyoni mwangu kumejaa uchungu, kwani nimefanyakazi kwa karibu miaka 10."

Bw. Zhan Xiaoming amefanya kazi kwa miaka 10 katika kiwanda hicho, ghafla kiwanda kinatoweka na tumaini lake limetokweka, anafadhaika sana na hana budi kufanya vibarua pamoja na baadhi ya marafiki zake. Aliishi hivyo kwa mwaka mmoja na nusu, siku moja ghafla alipata siku ya kiongozi wa zamani wa kiwanda kuwa kiwanda chao cha zamani kimeunganishwa na kiwanda No. 1 na kiwanda No. 2 vya mitambo, ambavyo pia viko katika hali yenye matatizo mengi vikitarajia kuondokana na hali hiyo mbaya. Bw. Zhao Xiaoming alirudi kwenye kazi yake ya zamani, lakini hali halisi ni kuwa alikuwa ni tu mwenye kukata tamaa, uzalishaji mali wa kiwanda ulikuwa katika hali ya kuwapatia wafanyakazi wake riziki tu, wachache waliorudishwa kazini walipata mshahara wa kimsingi, lakini wafanyakazi wengi bado hawakurudi kazini.

Bw. Zhan Xiaoming alimwambia mwandishi wa habari, wakati ule wao walisubiri kila siku wakitarajia kupewa misaada na serikali na kutarajia kuboreshwa mazingira ya uzalishaji mali. Hauchi hauchi kumbe umekucha, mwaka 2002 serikali ya China ilisema itasaidia sehemu ya kaskazini mashariki kuharakisha marekebisho na mageuzi ya kituo hicho cha kazi za viwanda. Mwaka 2004 serikali ya China ilifungua ofisi ya kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki, tokea hapo harakati za ustawishaji wa sehemu hiyo zilipamba moto.

Pamoja na mabadiliko ya mfumo na ufanisi wa viwanda kuwa mzuri, manung'uniko ya watu yanapungua, hivi sasa kitu kinachozungumzwa zaidi ni maendeleo ya viwanda, wafanyakazi wa sehemu ya kaskazini mashariki wamekuwa na imani na nguvu kutokana na sera za serikali za kustawisha kituo cha zamani cha kazi za viwanda. Mkurugenzi wa ofisi ya ustawishaji wa sehemu ya kaskazini mashariki ya baraza la serikali Bw. Zhang Guobao alisema,

"Ninaona mabadiliko makubwa ya kwanza ni ari ya watu, uvumbuzi wa utaratibu na uvumbuzi wa mfumo."

Baada ya jitihada za miaka kadhaa iliyopita, ongezeko la pato la nchini la mikoa mitatu ya sehemu ya kaskazini mashariki mwa China lilifikia 12.3% katika mwaka uliopita, likiwa ni kubwa kwa 2.8% kuliko wastani wa kiwango cha taifa, ongezeko la uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni lilifikia 89.5%, ambalo ni kubwa sana ikilinganishwa na wastani wa kiwango cha taifa.

Sekta ya uzalishaji mitambo ilikuwa nguvu kuu iliyohimiza maendeleo ya kasi ya uchumi katika miaka michache iliyopita kwenye sehemu ya kaskazini mashariki mwa China. Sekta ya uzalishaji mitambo inazingatiwa sana baada ya serikali kuamua kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki, na imepata maendeleo ya kasi kutokana na msaada wa sera nafuu za serikali. Katika maonesho ya kimataifa ya sekta ya uzalishaji mitambo yaliyofanyika hivi karibuni kwenye mji wa Shenyang, sehemu ya kaskazini mashariki mwa China, sekta ya uzalishaji mitambo ya sehemu hiyo ilionesha bidhaa zake za mitambo ya kisasa kabisa.

Kwenye maonesho hayo mwandishi wetu wa habari aliona roboti moja yenye akili iliyotengenezwa na kampuni moja ya sehemu ya kaskazini mashariki. Roboti hiyo inaweza kudhibitiwa na binadamu kutoka mbali, wakati ukiwa sehemu ya nje unaweza kuidhibiti kwa simu ya mkononi, unaweza kuitaka ikuambie hali ya nyumbani. Mwandishi wetu wa habari aliitumia ujumbe akitaka kujua hali ya hivi sasa ya nyumbani, baada ya roboti kupata ujumbe ilizindua mchakato husika na kupima hali ya mazingira ya huko, kisha ilitoa jibu.

Roboti ile ni moja ya bidhaa zilizooneshwa kwenye maonesho hayo ya kimataifa, ambazo zilizalishwa na sehemu ya kaskazini mashariki mwa China. Bidhaa nyingi zilizooneshwa kwenye maonesho zilikuwa mota za umeme, mitambo, vichwa vya magari-moshi na Transfoma. Mkurugenzi wa ofisi ya ustawishaji wa sehemu ya kaskazini mashariki ya baraza la serikali Bw. Zhang Guobao alitoa tathmini kuhusu maonesho hayo, akisema,

"Kwenye maonesho ya mwaka huu, niliona vitu vingi vya kisasa, watu wa sekta hiyo wanaweza kufahamu kiwango cha juu cha sekta ya uzalishaji mitambo ya China."

Naibu meya wa mji wa Shenyang Bw. Song Qi alisema, lengo la kufanya maonesho hayo ni kuhimiza maendeleo ya kasi ya sekta ya uzalishaji mitambo ya sehemu ya kaskazini mashariki mwa China.

"Kuandaa maonesho hayo kunaweza kuzikutanisha kampuni na viwanda vya kisasa vya uzalishaji mitambo hapa Shengyang, pamoja na bidhaa zake, ambapo vinaweza kuona upungufu wake ili kuchukua hatua kuinua kiwango cha uzalishaji mitambo cha China".

Habari zinasema katika siku za baadaye serikali ya China itaanzisha mazingira bora ya maendeleo kwa sekta ya uzalishaji mitambo na kuisaidia kwa sera nafuu.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-21