Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-21 16:00:25    
Kipindi maalum cha chemsha bongo kuhusu vivutio vya utalii vya "Mkoa wa Sichuan, maskani ya Panda"

cri

Tukizungumzia Mkoa wa Sichuan, China, labda marafiki zetu wengi hawaujui, lakini kama tukitaja Panda, huenda watu wote wanaweza kufurahia wanyama hao wanaopendeza. Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi ya China ndio maskani ya wanyama Panda.

Mkoani Sichuan kuna vivutio vingi vya utalii. Ili wasikilizaji wetu waelewe zaidi mkoa huo na vivutio vyake, Radio China kimataifa imeanzisha kipindi maalum cha chemsha bongo kuhusu vivutio vya utalii vya "Mkoa wa Sichuan, maskani ya Panda", na kuanzia tarehe 27 Novemba Idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa kila Jumatatu kwenye kipindi cha "Safari nchini China" itatangaza makala moja ya chemsha bongo kuhusu vivutio vya utalii vya "Mkoa wa Sichuan, maskani ya Panda", tunawakaribisha wasikilizaji wetu washiriki katika kipindi hiki cha chemsha bongo.

Kama tunavyofanya kila mwaka, kila tukisoma makala moja tutatoa maswali mawili ili wasikilizaji wetu wajibu. Kipindi hiki cha Chemsha bongo kitamalizika tarehe 15 Aprili mwaka 2007, baadaye kamati ya uchaguzi ya Radio China kimataifa itawachagua wasikilizaji washindi wa nafasi za kwanza, pili na tatu na wa nafasi maalum, na washindi watakaopata nafasi maalum wataalikwa kuja China kutembelea mkoani Sichuan. Tunawakaribisha wasikilizaji washiriki kwenye chemsha bongo na tunawatakia mafanikio mema.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-21