Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-22 16:44:43    
Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa China waeneza teknolojia ya matumizi ya gesi ya kinyesi

cri

  

Gesi ya kinyesi ni aina ya nishati safi ambayo inatolewa kutokana na kuoza kwa takataka, kwa kiwango kiasi inaweza kuchukua nafasi ya nishati nyingine zikiwemo mafuta, gesi ya kimaumbile na makaa ya mawe. Kwenye sehemu za vijijini, kinyesi cha binadamu na wanyama ya kufuga pamoja na takataka nyingine za maisha zote zinaweza kutumiwa kutengeneza nyesi ya kinyesi. Nishati hiyo inaweza kukidhi mahitaji ya nishati ya kupika na kuangaza. Hivi karibuni, mwandishi wetu wa habari alikwenda kwenye mkoa unaojiendesha wa kabila la waZhuang na kuona hali halisi ya matumizi ya gesi ya kinyesi huko.

Mwandishi wetu wa habari aliona, kwenye sehemu ambazo nishati hiyo inatumiwa kwa kiasi kikubwa, mazingira yameboreka na wakulima pia wamenufaika. Mkurugenzi wa ofisi ya kuondoa umaskini ya mkoa huo Bw. Hu Decai alieleza kuwa, hivi sasa manufaa mengi ya nishati ya gesi ya kinyesi yanaonekana kidhahiri, serikali ya huko imechukua shughuli za kueneza na kuendeleza matumizi ya nishati hiyo katika mpango wa jumla wa kuwasaidia wakulima wa huko kuondokana na umaskini. Bw. Hu Decai alisema,

"matumizi ya gesi ya kinyesi yana manufaa mengi, kwanza ni kutatua suala la nishati kwa wakulima wa huko, kupunguza hasara kwa misitu na kuboresha mazingira ya kiikolojia ya huko. Ya pili ni kuwa nishati hiyo ni safi sana, tena inatumia kinyesi cha wanyama wa kufuga, na takataka hizo zilizooza baada ya kutengeneza gesi ya kinyesi zinaweza kutumiwa kama mbolea mzuri wa kilimo. Aidha, matumizi ya gesi ya kinyesi yanaweza kurahisisha kazi ya nguvu kazi, hasa kwa wanawake."

Mkulima Lan Hualin anayeishi kwenye vitongoji vya mji wa Nanning mkoani Guangxi ana jamaa wanne katika familia yake, na familia yake inalima shamba lenye eneo la hekta mbili kwa mkataba wa kandarasi. Mbali na matumizi ya maisha, Lan Hualin pia alijenga nyumba yenye ghorofa mbili. Mwandishi wetu wa habari aligundua kuwa, nyumbani kwake hakuna jiko lililochafuliwa na moshi wa kuni kama iliyokuwa kwenye familia za kawaida za wakulima nchini China, na nyumba yake ni ya safi sana. Mke wa Lan Hualin alisema:

"napika kwa kutumia gesi ya kinyesi, na ni rahisi sana. Zamani tulikuwa tunachanja kuni mlimani. Hivi sasa hakuna haja ya kufanya hivyo tena. Badala ya kazi hiyo, tunaweza kufuga ng'ombe, kupanda mahindi na mipunga."

Wilaya inayojiendesha ya kabila la W ayao ya Gongcheng iko kwenye kusini mashariki ya mji wa Guilin mkoani Guangxi. Katika wilaya hiyo yenye wakazi laki tatu, kila familia ina bwawa dogo la gesi ya kinyesi, hata baadhi ya vijiji vimejenga bwawa kubwa la gesi ya kinyesi na kuipeleka gesi hiyo kwa kila familia kupitia bomba. Mwanakijiji Rong Wenxi alisema, familia yake inategemea gesi hiyo kuchemsha maji, kupika na kuangaza. Nishati hiyo si kama tu ni ya safi, bali pia ina gharama nafuu. Alisema:

"gesi ya kinyesi ni ya bei nafuu zaidi kuliko gesi ya kimaumbile, gesi ya kimaumbile inauzwa kwa yuan 92 kila pipa, na pipa moja hata haitoshi kwa mwezi mmoja. Lakini kwa gesi ya kinyesi, kila mwezi tunalipa yuan 32 tu."

Kuendeleza na kueneza gesi ya kinyesi kumeshaleta manufaa mkoani humo. Naibu mkuu wa idara ya misitu ya mji wa Guilin Bw. Jiang Ruohai alisema:

"mageuzi ya matumizi ya nishati yanayoendelea kwenye sehemu za vijini, pamoja na utumiaji na uenezaji wa gesi ya kinyesi zimewapunguzia wakulima wa huko kazi kubwa za kukata kuni, pia zimefanya eneo la misitu mjini humo kuongezeka kufikia asilimia 66.46 ya hivi sasa kutoka asilimia 37.07 ya mwaka 1980."

Mkoa unaojiendesha wa kabila la WaZhuang umepata mafanikio katika matumizi ya gesi ya kinyesi, si kama tu yanaleta manufaa kwa wakulima wa huko, bali pia yanaongoza njia mpya ya ujenzi wa vijiji. Wageni wengi wa nchi za nje walikwenda mkoani humo kufanya uchunguzi. Ofisa mmoja anayeshughulikia kazi ya kuondoa umaskini mkoani humo Bw. Li Fangzhen alieleza, mkoa wa Guangxi ukiwa ni mfano wa kuiga kwa kazi ya kuondoa umaskini nchini China, umepokea ujumbe wa uchunguzi kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea za Afrika. Bw. Li Fangzhen alisema:

"kama ninavyojua, hali ya hewa ya nchi za Afrika ni ya joto sana, ambayo inafanana na ile ya mkoa wetu. Hali hiyo inafaa kwa matumizi ya gesi ya kinyesi. Wageni kutoka nchi za Afrika wakikuja wanaonesha hamu kuwa hata wakajaribu kuiwaka mwenyewe."

Wasikilizaji wapendwa, kama mkipata fursa ya kutembelea China, karibu kutembelea mkoa wa Guangxia na kuona wenyewe jinsi matumizi ya gesi ya kinyesi yanavyoleta manufaa kwa watu wa huko.

Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza maelezo kuhusu Mkoa unaojiendesha wa kabila la waZhuang wa China waeneza teknolojia ya matumizi ya gesi ya kinyesi. Asanteni kwa kutusikiliza. Kwa herini!

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-22