Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-22 20:09:26    
Mpango wa kinu cha majaribio cha nyuklia wazinduliwa rasmi

cri

Katika hali ya hivi leo, ambayo bei ya mafuta inapanda kwa mfululizo na rasilimali zinatumiwa kupita kiasi, binadamu wameanza kutathimini vitendo vyao kuhusu maendeleo na kuanza kufanya utafiti kuhusu aina mpya za nishati, ukiwemo kinu cha majaribo ya nyuklia (ITER). Tarehe 21 mwezi Novemba wawakilishi wa nchi 7 husika za Umoja wa Ulaya, China, Marekani, Japan, Korea ya Kusini, Russia na India walisaini mkataba wa majaribio ya pamoja na nyaraka husika mjini Paris, Ufaransa, hatua ambayo inaonesha kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa kinu cha majaribio ya nyuklia.

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa siku hiyo alisimamia sherehe ya kutiwa saini akiwa rais wa nchi kilichoko kinu cha nyuklia. Alipotoa hotuba kwenye sherehe alisema, kutia saini kwa mkataba kunaonesha kuzinduliwa kwa "jitihada moja kubwa ya kisayansi katika historia ya binadamu.

"Tuna wajibu wa kufanya utafiti kwa ajili ya suala la nishati linalowakabili vizazi vyetu, na ITER ni mpango muhimu wa utafiti wa kisayansi wenye lengo hilo. Huu ni msaada tunaotoa kwa vizazi vyetu chini ya bendera ya umoja na majukumu."

"Kwanza, ushiriki wa China unaonesha azma ya China ya kutatua masuala ya nishati na mazingira yanayowakabili binadamu kwa ushirikiano wa kimataifa. Pili, tunatarajia ushirikiano huo utaifikisha teknolojia ya nyuklia ya China kwenye kiwango cha kisasa duniani katika muda mfupi ujao. Tatu, mpango wa ITER unahusu aina nyingi za elimu na teknolojia. Hivyo kushiriki kwa China kutasaidia kuinua kiwango cha teknolojia za maeneo mbalimbali. Nne, mpango wa ITER ni mradi mkubwa wa sayansi unaozalisha aina nyingi za teknolojia mpya, ambazo zinafanya kazi muhimu za kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii kwenye maeneo mbalimbali."

Sekta ya sayansi inakadiria kuwa endapo hakutakuwa na utafiti kuhusu aina mpya za nishati, katika miaka 200 ijayo, binadamu watamaliza kabisa nishati zilizolimbikizwa katika miaka milioni mia kadhaa iliyopita. Aidha matumizi ya nishati yana madhara makubwa kwa mazingira. Kinu cha majaribio ya nyuklia cha kimataifa kinaweza kuzalisha nishati mpya isiyo na uchafuzi kwa mazingira. Mwanasayansi mkuu wa kamati ya wanasayansi wa mradi wa ITER ya China Bw. Huo Yuping alifahamisha umaalumu wa nishati hiyo mpya.

"Kuna aina mbili za kugonganisha chembe za nyuklia kwa nishati ya atomiki, aina ya kwanza ni kama ya bomu la atomiki yaani kuzalisha nishati kwa hyper fission, ambayo itazalisha pia takataka za nyuklia zinazotoa mionzi; na aina nyingine ni kugonganisha chembe za nyuklia kama ya ndani ya jua, ambayo haitoi takata za nyuklia wala hewa inayofanya hali ya hewa ya dunia kubadilika kuwa joto."

Kutokana na kuwa malighafi ya nyuklia haiwezi kuisha wala haina madhara kwa mazingira, kwa hiyo nishati inayozalishwa kutokana na fusion ya nyuklia, itakuwa matarajio ya binadamu kuhusu nishati mpya katika siku za baadaye. Mpango wa ITER uliotolewa mwaka 1985 uliitikiwa na nchi husika. Kutokana na mkataba uliotiwa saini na nchi 7 safari hiyo, mpango wa nyuklia wa kimataifa utatumia Euro bilioni 9.9 katika miaka 35 ijayo. Huu ni mradi wa kisayansi unaochukua nafasi ya pili kwa ukubwa duniani unaofuata mradi wa kituo kinachojengwa kwenye anga ya juu, na pia ni mradi mkubwa kabisa wa ushirikiano wa kimataifa ambao China inashiriki.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-22