Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-22 19:53:51    
Mapishi ya doufu na uyoga kwa mvuke

cri

Mahitaji: Doufu gramu 300, uyoga vipande vitatu, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, nyama iliyosagwa gramu 50, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, maji ya wanga vijiko vitatu, siki kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, kiasi kidogo cha vipande vya tangawizi, na vitunguu maji, vitunguu saumu

Njia :

1. Kata uyoga uwe vipande vipande. Kata doufu iwe vipande vinne, changanya nyama iliyosagwa pamoja na vipande vya tangawizi, vitunguu maji, vitunguu saumu, mchuzi wa sosi, M.S.G, mvinyo wa kupikia, na korogakoroga. Weka nyama iliyosagwa ndani ya vipande vya doufu,.

2. chemsha maji ndani ya sufuria, weka vipande vya doufu kwenye sufuria kasha vichemshe kwa mvuke. Pakua baada ye dakika 10.

3. washa moto tena, tia mafuta kwenye sufuria tia vipande vya uyoga kwenye sufuria korogakoroga, tia mchuzi wa sosi, siki, chumvi, M.S.G, mafuta ya ufuta, maji ya wanga, vipande vya tangawizi, vitunguu maji, vitunguu saumu halafu korogakoroga, mimina maji kidogo, weka kwenye vipande vya doufu. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.