Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-23 21:50:27    
Iran imefanya juhudi mpya za kidiplomasia kuhusu suala la nyuklia

cri

Suala la nyuklia la Iran siku zote ni suala linalofuatiliwa zaidi na jumuiya ya kimataifa. Hivi karibuni Iran imefanya vitendo kadhaa vya kidiplomasia vinavyovutia ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa.

Kitendo cha kwanza kilichofanywa na serikali ya Iran ni kuomba rasmi msaada wa kiteknolojia kutoka kwa shirika la nishati ya atomiki duniani katika ujenzi wake wa kinu cha nyuklia. Inasemekana kuwa hivi sasa baraza la wakurugenzi la shirika hilo limekubali tu kutoa msaada wa kiteknolojia kwa ujenzi wa Iran wa kinu cha maji mepesi, na halitaki kuisaidia Iran kuanzisha kinu cha maji mazito cha Arak ambacho ni rahisi kubadilishwa kwa matumizi ya kijeshi. Kwa kweli Iran ilikuwa inajua matokeo hayo, lakini ni kwa nini iliendelea kufanya juhudi hiyo ya kidiplomasia? Wachambuzi wanaona kuwa, huenda kitendo hicho cha Iran ni kwa ajili ya kuonesha msimamo wake wa kidiplomasia.

Iran siku zote inasisitiza kuwa mpango wake wa kuendeleza nyuklia unatokana na lengo la amani, haina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia. Kuhusu shutuma za Marekani dhidi yake kuhusu kuendeleza silaha za nyuklia, Iran inachukulia kuwa shutuma za Marekani ni maoni yake pekee yanayoisinzia Iran kutokana na maslahi yake yenyewe. Hivyo ndivyo Iran inavyotetea mara kwa mara kuwa, mpango wake wa kuendeleza nishati ya nyuklia ni haki isiyonyimika ambayo ilipewa kutokana na mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia.

Vyombo vya habari vya Iran pia vinashirikiana na serikali yake katika suala hilo. Mkuu wa Radio ya Taifa ya Iran tarehe 20 alisema Radio hiyo inaweza kutangaza moja kwa moja majibizano kati ya rais wa Iran na rais wa Marekani. Barua aliyoandika rais Mahmoud Ahmadinejad kwa rais Bush wa Marekani mwezi Mei mwaka huu imewapa walimwengu picha ya kwamba, rais Ahmadinejad ni mtu mwenye nia imara hata katika wakati nchi yake inapokabiliwa na msukosuko wa kimataifa.

Kitendo cha pili cha kidiplomasia cha Iran ni kwamba, rais Ahmadinejad tarehe 18 Novemba alipofanya mazungumzo na spika wa bunge la Korea ya Kaskazini Bwana Choe Thae Bok aliitaka Korea ya Kaskazini iache shughuli za kutengeneza silaha za nyuklia, akitetea kupunguza silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea. Vyombo vya habari vinaona kuwa, kitendo hicho cha rais Ahmadinejad kilijaribu kueleza msimamo wake kwa jumuiya ya kimataifa kuwa, Iran haifanyi ushirikiano na Korea ya Kaskazini katika suala la nyuklia, pia haikubali nia ya Korea ya Kaskazini ya kutengeneza silaha za nyuklia, shughuli za kuendeleza nishati ya nyuklia za Iran zinalenga kutumia nishati hiyo kwa njia ya amani tu.

Kitendo cha tatu cha Iran ni kuitumia Iraq kuizuia Marekani isiiwekee zaidi shinikizo. Suala la Iraq ni tatizo kubwa kwa Marekani, sababu muhimu ya chama cha Republican cha Marekani kushindwa katika uchaguzi wa kipindi cha katikati ni kwamba, watu wa Marekani wanasikitishwa sana na sera ya serikali ya Bush nchini Iraq. Kwa upande mwingine, waziri mkuu wa Uingereza Bwana Tony Blair muda si mrefu uliopita alizitaka hadharani Iran na Syria zishiriki katika kutatua suala la usalama a Iraq. Hayo yote yameonesha kuwa, Iran inakabiliwa na fursa fulani. Habari zinasema Iran imewaalika marais wa Iraq na Syria kukutana na rais wa Iran mjini Tehran hivi karibuni, ili kujadiliana nao kuhusu jinsi ya kuboresha hali ya usalama nchini Iraq.

Vyombo vya Ulaya vimeona kuwa, kwa sababu Iran haikuacha shughuli za kusafisha uranium kabla ya tarehe 31 Agosti kwa kufuata azimio No. 1696 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Iran iliwahi kuingia katika hali ya kuwekewa vikwazo. Lakini imeonesha kuwa juhudi za kidiplomasia zinazofanywa na Iran zimeonesha kuwa, mustakabali wa maendeleo ya suala la nyuklia la Iran bado haujaweza kuthibitishwa wazi.