Kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu kuheshimu na kuhimiza haki za binadamu na kujenga dunia yenye masikilizano limefungwa tarehe 24 hapa Beijing. Wataalamu na wasomi zaidi ya 70 kutoka nchi na sehemu 20 wamejadili kwa kina kuhimiza haki za binadamu na kujenga uhusiano wenye masikilizano duniani.
Mwezi Septemba mwaka 2005, kwenye mkutano wa wakuu wa kuadhimisha miaka 60 ya Umoja wa Mataifa, rais Hu Jintao wa China alitoa hotuba muhimu kuhusu "Kujitahidi kujenga dunia yenye masikilizano ambapo kuna amani ya kudumu na usitawi wa pamoja". Wazo la kujenga dunia yenye masikilizano limekuwa suala linalofuatiliwa na wasomi wa China na wa nchi za nje. Kwenye kongamano hilo la kimataifa, wajumbe wamefanya majadiliano ya kina kuhusu suala hilo.
Profesa wa Chuo kikuu cha Nankai Bwana Chang Jian akiwa kwa niaba ya wataalamu na wasomi wa China alifafanua maoni husika akidhihirisha kuwa, uhakikisho wa haki za binadamu na mambo muhimu na msingi wa kujenga dunia yenye masikilizano, na dunia yenye masikilizano ni lengo na sharti la kuhakikisha haki za binadamu. Bwana Chang Jian alisema, ushindani wa zana za kijeshi, siasa ya kimabavu, msimamo wa upande mmoja, ugaidi, unaze wa aina mpya, pengo kubwa la umaskini na utajiti kati ya kusini na kaskazini, na uharibifu wa mazingira, yote hayo ni vikwanzo kwa kujenga dunia yenye masikiizano. Kujenga dunia yenye masikilizano kunatakiwa kufanya mazungumzo badala na mapambano, kunahitaji kufanya ushirikiano badala ya migogoro. Alisema:
Tukitaja kujenga dunia yenye masikilizano, kanuni za usawa za kuheshimu mamlala ya kila nchi ni muhimu kabisa. Kuheshimiana katika mambo ya siasa, kuhimizana katika mambo y uchumi, kufundishana katika mambo ya utamaduni, kufanya ushirikiano katika mambo ya usalama, kutambua hali halisi ya kihistoria na kuhakikisha haki za binadamu hatua kwa hatua.
Mjumbe wa Baraza la Taasisi ya utafiti wa haki za binadamu ya China Bwana Li Yunlong alisema kwenye kongamano hilo kuwa, kujenga dunia ya masikilizano kunazitaka nchi mbalimbali duniani zifanye mazungumzo na ushirikiano katika sekta ya haki za binadamu, na mazungumzo hayo pia yanasaidia kutimiza dunia yenye masikilizano.
Profesa Roberto Saba kutoka Algentina alikubalina na maoni hayo. Alisema:
Tunaona kuwa, lazima kubadilisha vitendo fulani katika sekta ya haki za binadamu duniani, zamani kwa kawaida nchi kadhaa zilikuwa hulaumiwa kuhusu hali yao isiyo nzuri ya haki za binadamu, hivi sasa ni lazima kuweka mkazo katika kufanya mazungumzo kuhusu kulinda haki za binadamu. Sababu ya kushambuliwa kwa haki za binadamu ni kukosa fursa ya kupashana habari na kukosa maelewano, kufanya mazungumzo ni msingi na njia ya kutatua suala hilo, ambayo inasaidia kuhimiza jumuia ya kimataifa iheshimu haki za binadamu.
Mtaalamu wa haki za binadamu kutoka Vietnam Bwana Dang Dung Chi pia alisema, lengo la kuheshimu haki za binadamu ni kuhakikisha kila mtu anaweza kuishi maisha kwa heshima, na lazima kuimarisha elimu kuhusu haki za binadamu na kufanya mazungumzo ili kuwa na ufahamu kuhusu haki za binadamu.
Naibu mkurugenzi wa taasisi ya haki za binadamu ya China Bwana Jin Jian alipotoa hotuba ya kuhitimisha kwenye ufungaji wa kongamano alisema:
Wajumbe wameona kuwa, kujenga dunia yenye maskilizano kuna maana mengi ya kisayansi, dunia yenye masikilizano ni matumaini ya maisha ya binadamu, ambayo inastahili kupiganiwa kwa juhudi na wananchi wa nchi mbalimbali duniani. Hali nyingi zisizo za masikilizano duniani huwa ni kutokana na haki za binadamu hazikuheshimiwa au kuhakikishwa ipasavyo, kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu ni njia yenye ufanisi ya kuondoa hali isiyo ya masikilizano na kutimiza lengo la kujenga dunia yenye masikilizano.
Idhaa ya Kiswahili 2006-11-24
|