Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-28 16:46:42    
Akiba ya fedha za kigeni ya China yazidi dola za kimarekani trilioni 1

cri

Ilipofika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, akiba ya fedha za kigeni ya China ilifikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni moja. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Benki ya Wananchi wa China zinaonesha kuwa, akiba ya fedha za kigeni ya China hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba ilifikia dola za kimarekani bilioni 987.9, na ni dola za kimarekani bilioni 12.1 zilikuwa zimebaki hadi kufikia trilioni 1. Kwa kufuata wastani wa ongezeko la dola za kimarekani bilioni 18.77 kwa mwezi, akiba ya fedha za kigeni ya China ingefikia dola za kimarekani trilioni 1 mwishoni mwa mwezi Oktoba na mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Kufikia thamani ya dola za kimarekani trilioni 1 kwa fedha za kigeni ya China kunafuatiliwa na watu. Hiyo ni tofauti kubwa sana ikilinganishwa na akiba ya fedha za kigeni ya China katika kipindi cha mwanzoni baada ya China kuanza kutekeleza sera za mageuzi na ufunguaji mlango: akiba ya fedha za kigeni ya China katika mwaka 1978 ilikuwa dola za kimarekani milioni 167. Pamoja na kuendelezwa kwa sera za mageuzi na ufunguaji mlango, uchumi wa China unakuzwa kwa mfululizo, shughuli za biashara na akiba ya fedha za kigeni za China vinaongezeka kwa kasi. Katika miaka miwili iliyopita, akiba ya fedha za kigeni iliongezeka kwa Yuan bilioni 200 kwa mwaka, na akiba ya fedha za kigeni ya China ilizidi ile ya Japan katika mwezi Februari mwaka huu, na kuchukua nafasi ya kwanza kwa wingi wa akiba ya fedha za kigeni duniani.

Akiba ya fedha za kigeni ni limbikizo la mali za taifa moja, ambayo inaonesha kuimarika kwa nguvu yake. Akiba ya dola za kimarekani trilioni 1 inaonesha uwezo mkubwa wa ununuzi wa China duniani, na kwa kiwango fulani inaweza kuathiri uchumi wa dunia. Tangu mageuzi kuhusu utaratibu wa uthibitishaji wa kiwango cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni uanze mwezi Julai mwaka 2005, kitendo chochote cha usimamizi wa fedha za kigeni nchini China kinafuatiliwa sana na soko la sarafu duniani.

Akiba kubwa ya fedha za kigeni ya China inaonesha kuimarika kwa nguvu ya udhibiti kwa uchumi wa taifa. Mwishoni mwa mwaka 2003, serikali ya China iliamua benki ya China na benki ya Ujenzi ya China kufuata utaratibu wa hisa, ambapo serikali ilitumia dola za kimarekani bilioni 45 za akiba kuongeza mitaji ya benki hizo, na kufanya sekta ya benki ya China kupiga hatua muhimu ya mageuzi.

Akiba kubwa ya fedha za kigeni inaonesha kuimarika kwa nguvu ya taifa, lakini kuongezeka bila kikomo na kwa muda mrefu siyo jambo zuri, na itapunguza ufanisi wa matumizi ya rasilimali, hata kuleta changamoto kwa maendeleo ya uchumi wa taifa.

Katika miaka 2 iliyopita, thamani ya bidhaa za China zilizosafirishwa kwa nchi za nje ilikuwa kubwa kuliko bidhaa zilizoagizwa na China kutoka nje, hivyo China ilikuwa na pato kubwa la fedha za kigeni, hali ambayo imeleta mazingira bora ya mitaji kwa kuongeza utoaji mikopo wa benki, na kuongeza shida kwa udhibiti wa mambo ya fedha wa serikali. Kuongeza au kupungua kwa akiba ya fedha za kigeni kwa hivi sasa, pia kunahusiana na marekebisho ya sera za pande nyingi zikiwemo za kiasi cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni na shughuli za biashara.

Kuongezeka kila siku ipitayo kwa akiba ya fedha za kigeni ya China kunafuatiliwa na nchi nyingi duniani, tena kumeleta kisingizio kwa baadhi ya nchi kutoa shinikizo kwa shughuli za biashara ya China, na ni rahisi kuleta mikwaruzano mingi katika mambo ya biashara. Hali ya akiba ya fedha za kigeni ya China kuwa zaidi ya dola za Kimarekani trilioni 1 ni rahisi kugusa hisia ambazo tayari jumuiya ya kimataifa inazo.

Kutokana na kuathitiwa na mambo mengi yaliyotajwa hapo mwanzo, thamani ya dola za Kimarekani trilioni 1 ya fedha za kigeni za China imeleta masuala yenye shida kubwa yakiwa ni pamoja na hatua gani zingechukuliwa ili kupunguza hatua kwa hatua ongezeko kubwa la akiba ya fedha za kigeni, na kudumisha uwiano kati ya mapato na matumizi duniani? Namna ya kuepusha mgogoro wa soko la fedha, kutumia ipasavyo akiba kubwa ya fedha za kigeni na kulinda usalama wa uchumi wa taifa.

Kuwa na akiba ya fedha za kigeni ya dola za kimarekani trilioni moja ni jambo zuri na pia ni jambo baya, ambalo idara ya usimamizi ya fedha za kigeni ililizingatia kutoka siku nyingi zilizopita, na imethibitisha mwelekeo wa sera mpya za kupunguza ongezeko la akiba ya fedha za kigeni, kutumia ipasavyo akiba hiyo na kuboresha usimamizi wa fedha za kigeni.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-28