Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-29 15:19:07    
Uchunguzi kuhusu kifo cha jasusi wa Russia aliyekufa kutokana na sumu na uhusiano kati ya nchi za magharibi na Russia

cri

Tarehe 28 waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair alisema, katika uchunguzi kuhusu kifo cha jasusi wa zamani wa Russia Bw. Alexander Litvinenko aliyekufa kutokana na sumu, Uingereza hairuhusu kuwekewa vizuizi vyovyote katika mambo ya diplomasia na siasa. Alisema tukio hilo ni nyeti sana na Uingereza imedhamiria kugundua ukweli wake na kuthibitisha ni nani atawajibika. Alisema, kama kuna haja atajadiliana uso kwa uso na rais Putin wa Russia. Huu ni msimamo wazi kabisa uliooneshwa na serikali ya Uingereza baada ya jasusi wa zamani wa Russia kufa kutokana na sumu.

Tukio la ajabu la kufa kutokana na sumu kwa Bw. Litvinenko linawakumbusha tukio jingine la ajabu lililotokea katika kipindi cha vita vya baridi nchini Uingereza. Mwaka 1978 mwandishi mashuhuri wa vitabu wa Bulgaria Bw. Markov aliyekimbia nchini Uingereza alichomwa kwa mwavuli na kufariki baada ya siku tatu, polisi ilithibitisha kuwa muuaji ni wa shirika la kijasusi la Russia. Tukio hilo ilikuwa nusura livunje uhusiano wa kibalozi kati ya Uingereza na Russia. Serikali za Uingereza na Russia zitalishughuliaje kifo cha Litvinenko, huu ni mtihani mwingine kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Ingawa kwenye wosia alioacha, Litvinenko alisema Putin ni mwendeshaji wa "nyuma ya pazia" katika tukio hilo, lakini polisi ya Uingereza kwa hivi sasa inasema "sababu ya kifo bado haijafahamika", wala haijasema kama ni "mauaji ya kupangwa". Tarehe 28 Bw. Tony Blair alipozungumzia tukio hilo pia hakusema wazi kwamba Russia ni lazima iwajibike kwa tukio hilo, ila tu alisema atajadiliana na rais Putin. Ni dhahiri kwamba serikali ya Uingereza inachukua msimamo tahadhari kuhusu tukio hilo. Lakini hata hivyo, kwa vyovyote vile tukio hilo hakika litaathiri uhusiano kati ya Russia na nchi za magharibi.

Baada ya "tukio la Septemba 11" serikali ya Russia iliwahi kuwa na uhusiano mzuri na nchi za magharibi. Lakini katika siku za karibuni uhusiano huo umekuwa wa wasiwasi kutokana na kuwa nchi za magharibi kuikosoa Russia "kuelekea kwenye utawala wa kiimla". Kutokea kwa kifo cha Litvinenko kumekuwa kama msumari wa moto kwenye kidonda, na huenda uhusiano huo utakuwa na wasiwasi zaidi. Wachambuzi wanaona kuwa ingawa nchi za magharibi hazitaigeuka kabisa Russia, lakini tukio hilo litakuwa ni wingu jeusi katika uhusiano kati ya nchi za magharibi na Russia, na siku hizi makala chungu nzima kwenye magazeti ya nchi za magharibi kuhusu "mauaji ya aina ya KGB" ya Russia zimechangia kuongezeka kwa wasiwasi wa uhusiano huo.

Hata hivyo pia kuna watu wenye akili tulivu, wanasema ukweli ni kwamba wakati huu serikali ya Putin haikuwa na haja kabisa ya kumwua Litvinenko, kwa sababu Bw. Litvinenko alikwisha maliza yote aliyotaka kusema na aliyotaka kufanya, "thamni yake ya kupinga Russia" ilikuwa imepotea au iliisha kwa kuandika kitabu chake. Mbunge mmoja wa baraza la chini la Russia alisema, Russia haitaambua chochote kutokana na kifo cha Litvinenko, tukio hilo limefanywa na adui wa serikali ya Russia ili kuhamishia lawama kwenye serikali ya Russia na kujipatia manufaa ya kisiasa.

Wachambuzi wanaona kuwa nchi za magharibi zimenufaika kutoka tukio hilo. Kutokana na tukio hilo nchi za magharibi zimepata "sababu zinazoeleweka kwa umma" za "upanuzi wa NATO", "kuingia kwenye mapambano dhidi ya ugaidi katika Asia ya kati" na "kusaidia serikali zinazopinga Usovieti nchini Russia". Kutokana na maana hiyo, kifo cha Litvinenko aliyepoteza thamani yake ni "msaada mkubwa" kwa nchi za magharibi.

Kadhalika, wachambuzi wengine wanasema, kuna uwezekano wa kumwua kwa ajili ya kunyamazisha kauli. Bw. Litvinenko alipokuwa jasusi wa Russia alishughulika na uhalifu unaohusiana na madaraka na fedha, katika kazi yake hiyo pengine alikuwa na uadui na watu husika, kwa hiyo kumwua inawezekana kulikuwa na lengo la kumnyamazisha.

Kwa ufupi, watu wana maoni tofauti kuhusu chanzo cha kifo chake. Lakini kabla ya ukweli kugunduliwa, serikali ya rais Putin haiwezi kukwepa lawama, na uhusiano kati ya Russia na nchi za magharibi utaathirika.