Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-29 20:07:35    
Wachina wengi wapata ajira katika sekta ya biashara ya kitarakimu

cri

Kutokana na kuinuka kwa kiwango cha teknolojia ya mtandao wa internet na kuenezwa kwa matumizi ya mtandao wa internet, hivi sasa nchini China biashara ya kitarakimu imekuwa njia kuu ya biashara, na wafanyabiashara wenye busara wamepata ajira kwa kutumia teknolojia hiyo, na baadhi yao wanaendesha maduka kwenye mtandao wa internet na kujipatia faida, wengine wanatangaza kazi zao zenye uvumbuzi kupitia mtandao wa internet na kujipatia faida kwa kazi za kiakili.

Takwimu zilizotangazwa na kituo cha taarifa kuhusu mtandao wa Internet cha China zinaonesha kuwa, hivi sasa zaidi ya watu milioni 1000 wanatumia mtandao wa internet nchini China, na zaidi ya kompyuta milioni 50 zimeunganishwa kwenye mtandao wa internet. Hali hiyo imewezesha watu kujipatia ajira kwa kutegemea teknolojia hiyo. Bi. Liu Yingying ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu alianzisha duka moja kwenye mtandao. Alisema:

"wasichana wanapenda kununua nguo mara kwa mara, zamani nilipenda kwenda kwenye maduka ya nguo kununua nguo, lakini hivi sasa nimegundua kuwa wanafunzi ni soko kubwa sana, basi niliamua kuanzisha duka langu mwenyewe kwenye internet."

Kwa kuwa katika biashara ya kitarakimu wafanyabiashara na wateja hawawezi kuonana uso kwa uso, hivyo namna ya kuhakikisha usalama wa biashara hiyo ni jambo linalofuatiliwa sana duniani. Hivi sasa ulipaji wa biashara ya kitarakimu unaofanywa na watu binafsi unaendeshwa na upande wa tatu wa kampuni ya mtandao, yaani wateja wanalipa kwa upande wa tatu wa kampuni ya mtandao, baada ya bidhaa kufikishwa na kukubaliwa na wateja, kampuni hiyo inalipa fedha kwa mwenye duka. Hali hiyo inaweza kutokea kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia ya mtandao wa internet.

Kuanzisha duka kwenye mtandao wa Internet hakuhitaji mtaji mikubwa na wala hakuhitaji wakati mwingi, unapiga mause tu na kuweza kuwa na duka lako mwenyewe. Watu wengi wanaona kuwa shughuli hiyo inawasaidia sana watu kupata uzoefu na uwezo wa kibiashara mbali na fedha. Na kwa kuwa jambo hilo linaweza kuwa kazi ya ziada na kuleta pato jingine, shughuli hiyo inapendwa sana na vijana wa China. Uchunguzi umeonesha kuwa, hivi sasa maduka ya mtandao nchini China yanauza bidhaa za aina mbalimbali. Kama pato la duka hilo likizidi pato la ajira rasmi, wenye maduka wengi wanaacha rasmi kazi zao na kuweka mkazo katika biashara yao kwenye mtandao.

Kundi la kwanza la maduka kwenye mtandao nchini China lilianzishwa mwaka 1999. Hivi sasa kuna maduka ya namna hiyo zaidi ya laki nne, na wengi wa wenye maduka hayo wanachukulia kazi hiyo kuwa ajira yao rasmi na zaidi ya nusu wanapata pato la zaidi ya wastani wa Yuan elfu 30 kila mwaka. Kote nchini China, watu zaidi ya milioni 15 wanafanya biashara kwa njia ya mtandao wa Internet. Lakini ni kwa nini maduka ya mtandao wa Internet yanaweza kupata faida kubwa namna hii? Mwenye duka mmoja alipoelezea maarifa yake ya biashara. Alisema:

"mimi nauza vipodozi. Naona kuwa mafanikio yangu yanatokana na kutuma bidhaa zangu haraka iwezekanavyo mara baada ya mteja kukubali bidhaa zangu. Katika biashara kwenye mtandao, wateja wanaogopa udanganyifu, hivyo wakipata bidhaa haraka watakuwa na uaminifu zaidi. Hatua hiyo inawavutia wateja wengi kuja kwenye duka langu kununua tena vitu."

Ukisema kuwa wenye duka hao wanahamisha biashara ya kawaida kwenye mtandao wa internet, basi hivi sasa watu wanaoitwa Witkey wanabadilisha kikamilifu sekta ya shughuli za uvumbuzi. Watu hao badala ya kufanya kazi ofisini, hivi sasa wanafanya kazi nyumbani.

Wazo la Witkey lilitolewa mwezi Julai mwaka 2005, na limekuwa njia mpya ya kuwapatia fedha watu wenye umaalum, ujuzi na busara kwa utaratibu wa kuuliza na kujibu kwenye mtandao wa internet. Utaratibu huo ni kuwa watu binafsi au makampuni wanatangaza mahitaji yao pamoja na mshahara kwenye mtandao wa internet kama vile usanifu wa bidhaa fulani za uvumbuzi, hivyo ma-Witkey kote nchini China wanaweza kugombea kazi hiyo. Kazi hiyo ni pamoja na kazi ndogo ya kuwapatia watu jina hadi kazi kubwa ya usanifu wa bidhaa maalum. Malipo yake pia yanategemea ugumu wa kazi hiyo.

Bi. Chen Yi ni Witkey maarufu mjini Beijing. katika nusu ya mwaka iliyopita, alifanikiwa kupata kazi kama hizo zaidi ya 10 kwenye mtandao wa internet, na kupata Yuan zaidi ya elfu 10. alisema:

"Katika kazi hizo, nilisanifu nembo za makampuni mbalimbali, tovuti na matangazo. Nilipoanza shughuli hiyo niliweza kupata Yuan elfu mbili hadi elfu nne tu, lakini wateja wengi wakikugundua na pato pia linaongezeka."

Baada ya maendeleo ya mwaka mmoja, hivi sasa kuna tovuti zaidi ya 40 ya Witkey za aina mbalimbali nchini China, na idadi ya wanachama wa tovuti hizo yaani ma-Witkey imefikia laki sita, wakiwemo wahandisi, wasanifu, waandishi wa makala, wanafunzi wa vyuo vikuu hata walemavu.

Hivi sasa wimbi la kujipatia ajira kwenye shughuli hizo za mtandao wa internet nchini China linapamba moto. Watu walioshiriki kwenye shughuli hizo si kama tu wanajipatia fedha, bali pia wanaleta faida kwa jamii kutokana na kazi zao. Kwa uhakika pamoja na kuenezwa zaidi kwa matumizi ya mtandao wa internet nchini China, na maendeleo ya teknolojia ya mtandao, itatoa athari kubwa zaidi kwa maisha ya watu wa China.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-29