Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-29 20:11:51    
Mapishi ya uyoga mweusi na nyama ya ng'ombe

cri

Mahitaji: Nyama ya paja la ng'ombe gramu 250, uyoga mweusi gramu 100, spinachi gramu 25, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, chumvi vijiko viwili, M.S.G kijiko kimoja, vipande vya vitunguu maji na tangawizi, na mchuzi wa sosi kijiko kimoja.

Njia:

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, osha uyoga mweusi na ukate uwe vipande, osha spinachi.

2. washa moto na tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi na korogakoroga, halafu tia vipande vya nyama ya ng'ombe korogakoroga, mimina mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, tia chumvi, na korogakoroga, halafu tia vipande vya uyoga mweusi, mimina maji kidogo, korogakoroga, tia spinachi, korogakoroga halafu tia M.S.G, na kasha korogakoroga, na uipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.