Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-30 18:59:01    
Wataalamu wazungumzia juhudi za usuluhishi zilizofanywa na pande mbalimbali kwa kurudisha mapema mazungumzo ya pande 6

cri

Ili kuyawezesha mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yarudishwe mapema, viongozi wa ujumbe utakaohudhuria mazungumzo hayo wa China, Korea ya kaskazini, Marekani, Korea ya kusini na Japan wamefanya majadiliano ya pande mbili mbili au ya pande nyingi hivi karibuni hapa Beijing. Wataalamu husika wamesema, hizi ni juhudi zilizofanywa na pande mbalimbali ili kurudisha mapema iwezekanavyo mazungumzo ya pande 6.

Tarehe 29 Novemba, wizara ya mambo ya nje ya China ilitoa habari ikisema, tarehe 28 na 29 mwezi huu viongozi wa ujumbe wa China, Korea ya kaskazini na Marekani walifanya mkutano usio rasmi hapa Beijing, baada ya kufanya majadiliano ya pande mbilimbili au pande nyingi, viongozi hao wamebadilishana maoni kwa kina na unyoofu, wakaongeza maelewano, ambapo pande hizo tatu zimekubaliana kufanya juhudi za pamoja ili mazungumzo ya pande 6 ya kipindi kijacho yafanyike mapema na kupata maendeleo. Mtafiti wa Taasisi ya masuala ya kimataifa ya China Bwana Jin Linpo anaona kuwa, mkutano huo usio rasmi kati ya nchi 3 za China, Korea ya kaskazini na Marekani una umuhimu mkubwa sana. Alisema:

Katika muda wa mwaka mmoja baada ya kusimamishwa kwa mazungumzo ya pande 6, mabadiliko makubwa yametokea katika hali ya Korea ya kaskazini, ambapo Korea ya kaskazini ilifanya majaribio ya makombora, na ilitangaza kwa dunia kwamba ilifanya majaribio ya nyuklia. Katika hali hiyo amani na utulivu wa kikanda ulikabiliwa na changamoto kubwa, hivyo ni lazima kueleza malalamiko juu ya suala hilo. Ingawa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la lazima juu ya Korea ya kusini kufanya majaribio ya makombora na majaribio ya nyuklia, lakini kama pande mbalimbali hazitafanya juhudi mpya za kidiplomasia kuhusu suala hilo, ni vigumu kuona matumaini mapya ya kutatua suala hilo. Kutokana na maana hii, juhudi za kidiplomasia zinazofanyika hivi karibuni ili kurudisha mazungumzo ya pande 6, hasa mkutano wa pande tatu za China, Marekani na Korea ya kaskazini una umuhimu mkubwa.

Mbali na hayo, viongozi wa ujumbe wa Japan na Korea ya kusini pia walifika Beijing tarehe 26 na 27, ambapo wamefanya majadiliano ya pande mbilimbili na pande zinazohusika. Viongozi wa ujumbe mbalimbali wa nchi 5 wamekusanyika pamoja hapa Beijing, hii inafuatiliwa sana na vyombo vya habari. Hata vyombo fulani vya habari vinasema, huenda kwenye majadiliano hayo, pande mbalimbali zinazohusika zitafikia maoni ya pamoja kuhusu tarehe halisi ya kurudishwa kwa mazungumzo ya pande 6. Lakini kutokana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya China, pande mbalimbali zinazohusika bado hazijaamua tarehe halisi ya kuanzishwa kwa mazungumzo hayo.

Bwana Jin Polin anaona kuwa Korea ya kaskazini na Marekani na wahusika wakuu katika suala la nyuklia la peninsula ya Korea, lakini katika siku zote zilizopita pande hizo mbili hazikuaminiana, hata hivi sasa bado zinapambana kimsingi kuhusu masuala kadhaa muhimu, hivyo hata baada ya kufanyika juhudi mpya za kidiplomasia, tarehe halisi ya kuanzishwa tena mazungumzo ya pande 6 bado haijaweza kuamuliwa. Bwana Jin alisema:

Sababu ya kutoweza kuamuliwa kwa tarehe halisi ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya pande 6, kubwa ni kwamba bado kuna migongano mikali kati ya Korea ya kaskazini na Marekani kuhusu ajenda ya mazungumzo ya duru jipya ya pande sita na malengo yanayopaswa kufikiwa, migongano hiyo bado ni mikubwa.

Ingawa juhudi za kidiplomasia kuhusu kurudisha tena mazungumzo ya pande 6 bado zinakabiliwa na taabu kadhaa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Jiang Yu hivi karibuni alisema kuwa, China siku zote inatetea kufanya mazungumzo ili kutimiza lengo la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia, na kuzitaka pande mbalimbali zitumie fursa na kuwa na msimamo wenye unyumbufu ili mazungumzo ya pande 6 yarudishwe mapema.

Bwana Jin amesema, maneno yaliyosemwa na msemaji huyo yameonesha kuwa China itaendelea kuonesha umuhimu wake katika kuhimiza mazungumzo hayo yarudishwe mapema.