Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-01 19:31:27    
Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za Afrika na Amerika ya Kusini wamalizika

cri

Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za Afrika na Amerika ya Kusini ulimalizika tarehe 30 Novemba mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria. Wajumbe kutoka nchi 47 za Afrika na nchi 11 za Amerika ya Kusini wakiwemo marais wa nchi 23 walihudhuria mkutano huo. "Taarifa ya Abuja" iliyopitishwa katika mkutano huo inazitaka nchi za Afrika na Amerika ya Kusini ziimarishe ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ili kutafuta maendeleo ya haraka kwa pamoja.

Kwenye mkutano uliofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 uliowashirikisha wataalamu na mawaziri, ulijadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara, kilimo na usalama. Na kwenye mkutano wa wakuu uliofanyika tarehe 30 wajumbe na wakuu wa nchi mbalimbali wamekubaliwa kuhusu mpango wa kuimarisha ushirikiano na utekelezaji wake. Kwenye mkutano huo rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria alisema nchi za Afrika na Latin Amerika zote zina historia ya karne kadhaa ya kuwa makoloni, kukaliwa na nchi za nje, kunyonywa na kupuuzwa, na sasa nchi hizo zinakabiliana na changamoto za namna moja. Alisema huu ni msingi wa ushirikiano kati ya mabara hayo mawili. Katika hotuba yake alizitaka nchi zote za mabara hayo mawili zitumie vya kutosha maliasili za watu na maumbile, ili kuufanya moyo wa ushirikiano uwe kwa vitendo. Bw. Obasanjo alisema nchi za Afrika na Latin Amerika zina maslahi ya pamoja katika nyanja za maendeleo ya kilimo, uwekezaji wa biashara, nishati, miundombinu, safari za ndege, upashanaji habari, ukomeshaji wa umaskini na usalama wa kikanda, na kuna haja kwa nchi hizo kuaminiana na kuimarisha ushirikiano. Rais Lula da Silva wa Brazil alizitaka nchi zote zilizoshiriki kwenye mkutano huo ziungane ili kupambana na vizuizi vya kibiashara vya nchi zilizoendelea. Rais Muamar Gadaffi wa Libya alisema 80% ya malighafi duniani zinatoka Afrika na Amerika ya Kusini, kwa hiyo nchi za mabara hayo mawili zinapaswa kuendeleza viwanda badala ya kusafirisha nje malighafi. Rais Eva Morales wa Bolivia kwenye hotuba yake alizitaka nchi za mabara hayo mawili zizingatie kulinda haki za wananchi.

Mkutano wa wakuu ulipitisha "Taarifa ya Abuja". Taarifa hiyo inasema mkutano huo ulikumbuka historia ya namna moja na umegundua fursa ya kihistoria, na kuona kwamba Umoja wa Afrika na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa yameweka msingi imara wa ushirikiano wa uchumi na usalama, na kwamba nchi za Afrika na Amerika ya Kusini zina maliasili za kutosha za nguvu kazi na maliasili nyingi nyingine katika uhusiano wa kiwenzi ili kuhakikisha amani, usalama na maendeleo ya uchumi.

Wakuu walioshiriki kwenye mkutano huo pia wameamua kujenga mfumo wa baraza kati ya Afika na Amerika ya Kusini. Baraza hilo litafanyika kila baada ya miaka miwili katika mabara mawili kwa kubadilishana, ili kutimiza mpango uliotolewa katika "Taarifa ya Abuja" na kuufanya moyo wa mkutano huo uwe maslahi ya uchumi, siasa na maendeleo ya jamii, kuimarisha majadiliano na ushirikiano wa ngazi mbalimbali na hasa ushirikiano wa kilimo, uwekezaji wa biashara, nishati, teknolojia, utalii na maliasili ya maji, kuimarisha maingiliano ya kiutamaduni, kutekeleza makubaliano kuhusu biashara, safari za ndege na kilimo.