Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-05 16:32:54    
Je, Iran, Uturuki na Syria zinaweza kutatua suala la Iraq kwa ushirikiano?

cri

Mwenyekiti wa Kamati ya Maslahi ya Taifa ya Iran Bw. Rafsanjani tarehe 3 jioni alipokutana na waziri mkuu wa Uturuki Bw. Erdogan aliyekuwa ziarani nchini Iran alisema, ushirikiano wa nchi tatu za Iran, Uturuki na Syria utaisaidia Iraq kutimiza usalama na ukamilifu wa ardhi. Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na hali ya kuongezeka kwa mawasiliano kati ya nchi hizo tatu, imeonesha kuwa kila nchi inataka kupunguza shinikizo kwa kutumia fursa ya kutatua suala la Iraq. Nchi hizo zikiwa nchi za Kiislamu na nchi jirani za Iraq kama zikiweza kuimarisha ushirikiano hakika zitasaidia utatuzi wa suala la Iraq. Lakini suala lenyewe ni kuwa ufanisi wa ushirkiano huo unategemea kama Marekani itaweza kukidhi mahitaji ya nchi hizo tatu.

Katika muda wa miaka zaidi ya mitatu iliyopita tokea vita vya Iraq vimalizike, hali ya Iraq haijawahi kuwa nzuri, na jeshi la Marekani limezidi kuzama katika hali mbaya. Makosa ya Marekani kuhusu suala la Iraq yamesababisha kushindwa kwa chama cha Ripublican katika uchaguzi wa kipindi cha katikati. Hivi sasa nchi za Marekani na Uingereza zimetambua kwamba kama zisiporekebisha sera kuhusu Iraq nchi hizo mbili zintakuwa na matatizo makubwa zaidi. Wanasiasa wa Marekani na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair wote wanaona ni afadhali nchi za Iran na Syria zishiriki kwa masharti kwenye utatuzi wa suala la Iraq na Mashariki ya Kati.

Sambamba na hayo, nchi za Iran na Syria mara kwa mara zinaitaka Marekani isimamishe shinikizo kwa Iraq na huku zikiahidi kuwa zitaisaidia Marekani kutimiza amani ya Mashariki ya Kati. Rais wa Iran Bw. Mohamed Ahmadinejad kwa mara kadhaa alisema, kama Marekani itabadilisha sera zake za ubabe kwa Iran, Iran itaisaidia Marekani kutuliza hali ya Iraq. Waziri wa mambo ya nje wa Syria Bw. Walid Mualem alipofanya ziara nchini Iraq mwezi Novemba alisisitiza kwamba Syria itaiunga mkono serikali ya Iraq na kupenda kushirikiana na serikali ya Iraq ili kurudisha hali ya amani na utulivu nchini humo. Hali kadhalika serikali ya Uturuki kwa mara kadhaa iliiashiria Marekani kwamba kama haitasaidia Uturuki kutuliza vurugu kwenye mpaka wa mashariki kati yake na Iraq na kupambana na vikosi vya chama cha wafanyakazi cha Kurd, Uturuki itapambana yenyewe na vikosi hivyo. Ni dhahiri kwamba nchi za Iran, Syria na Uturuki kila moja imepata matakwa yake kwa Marekani katika utatuzi wa suala la Iraq. Ili kufanikisha malengo yao, nchi hizo tatu siku hizi licha ya kuimarisha shughuli zao za kidiplomasia pia zimeongeza ziara nchini Iraq.

Hivi sasa mgogoro kati ya madhehebu ya Suni na Shia nchini Iraq umekuwa mkali, matukio ya utekaji nyara yameongezeka, kama Syria na Iran zikisaidia Iraq hakika mgogoro huo utapungua.

Kuhusu matakwa ya nchi hizo tatu Marekani inaelewa wazi, kama haitakidhi mahitaji yao, suala la Iraq itakuwa vigumu kutatua suala la Iraq, na badala yake pengine litazidi kuwa baya zaidi. "Kikundi cha utafiti wa sera kuhusu suala la Iraq" nchini Marekani tarehe 6 kilitoa ripoti rasmi kwa rais Bush, na kupendekeza kwamba serikali ya Marekani iwasiliane moja kwa moja na Iran na Syria. Lakini Marekani ikiitikia matakwa mahitaji ya nchi hizo tatu itakuwa ni sawa kukubali kushindwa kwa sera za Marekani kuhusu nchi hizo tatu, hivyo Marekani haitakubali. Rais George Bush wa Marekani tareh 4 alipokutana na kiongozi wa Muungano wa Umoja wa Iraq Bw. Aziz al Hakim alisema, anatumai kuwa nchi jirani za Iraq, Iran na Syria ziheshimu mamlaka ya Iraq na kusimamisha "vitendo vya uharibifu" kwa serikali ya Iraq. Huu ni msimamo mkali kwa nchi tatu za Iran, Syria na Uturuki katika utatuzi wa suala la Iraq.

Idhaa ya Kiswahili 2006-12-05